Mkuu wa Wilaya awataka Maafisa Ugani na Watendaji wa Vijiji watoke ofisini waende wakatoe elimu ya Kilimo Bora

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amewataka Maafisa Ugani na Maafisa Watendaji wa Vijiji kuhakikisha wanawafikia Wakulima ili kuendelea kutoa elimu ya kilimo bora.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Onesmo Buswelu ameyasema hayo wakati Kikao cha Maendeleo cha Wilaya kilichohusisha Watumishi wa Serikali pamoja na Wadau mbalimbali ambapo lengo kuu ni kuelekea katika msimu wa 2023/2024 mbapo amewataka Maafisa Ugani na Maafisa Watendaji wa Vijiji kutoka ofisini na kwenda kutoa elimu ya kilimo bora.

Philemon Mwita ni Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema msimu wa 2023/2024 wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha inazalisha mazao ya chakula zaidi ya Tani Laki Tatu huku akiwahakikishia Wakulima kufikiwa na mbolea za ruzuku kwa wakati.

Alfred Kipawa ni mzee maarufu katika wilaya hiyo ameiomba Serikali kuhakikisha utoaji wa elimu katika sekta ya kilimo kupewa kipaumbele ili wakulima waweze kujua namna bora ya matumizi ya mbolea za ruzuku lakino pia wawe wakulima wa kisasa zaidi.

Aidha Buswelu amewataka wazabuni wa kusambaza mbolea za ruzuku pamoja na mbegu za mazao mbalimbali kuhakikisha inawafikia wakulima kwa wakati sahihi.

Bugoma Wa Bugoma, Katavi.
 
Awapatie pikipiki, magari na mafuta.
 
Hii wizara ni heri ifutwe tu maana pesa haipati kwa uhakika
Pelekeni pesa wagani wataenda kila shamba. Kila siku kauli tu
 
Back
Top Bottom