Hofu ya CCM kwa vyama vya upinzani ni ya kweli?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
CCM na hata Mwl Nyerere RIP hofu Yao kuu kwa vyama vya upinzani ni kuvurugika kwa umoja, amani na mshikamano wa watanzania, kuvunjika kwa muungano na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Je, hofu hii ni ya kweli na dhahili?

Je, wanasiasa wa vyama vya upinzani wanao uwezo wa kudumisha mshikamano, amani, utulivu na muungano?

Kifup,i wanasiasa wa upinzani wanao uwezo wa kuiongoza nchi kwa miaka 5 mfululizo kama wakiaminiwa na wananchi? Wana ajenda gani juu ya mshikamano, utulivu, amani na muungano? Wana ajenda gani juu ya uchumi na hali za watu, ni nini vitakuwa vyanzo vyao vya fedha, watajitegemea au watategemea zaidi wazungu?

Haya ndiyo maswali ambayo CCM Bara na CCM Zanzibar inaweza kusita kufanya siasa za kistaarabu, wazi na za haki.

Ni kazi ya vyama vya upinzani kuyajibu maswali haya yote kila wanapopata nafasi ya kupanda jukwaani kuongea na umma. Tunachokiona Sasa ni kila mwanasiasa wa upinzani aliyepatiwa nafasi na wananchi kuwa mbunge au kiongozi kujilimbikizia mali ili kuhakikisha kuwa hawi maskini tena kwa kutumia nafasi yake.

Kuna wahisani wengi wanachomba visima, wanajenga madarasa, nk. Je, vyama vya upinzani vimewahi japo kuchimba Rambo moja pahali kama trailer wakati wananchi wakisubiri sinema kamili watakapoishika dola?

Je, hofu ya CCM kwa wapinzani ni ya bure?
 
CCM na hata Mwl Nyerere RIP hofu Yao kuu kwa vyama vya upinzani ni kuvurugika kwa umoja, amani na mshikamano wa watanzania, kuvunjika kwa muungano na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Je, hofu hii ni ya kweli na dhahili?
Hakuna hofu yoyote
Je, wanasiasa wa vyama vya upinzani wanao uwezo wa kudumisha mshikamano, amani, utulivu na muungano?

Kifup,i wanasiasa wa upinzani wanao uwezo wa kuiongoza nchi kwa miaka 5 mfululizo kama wakiaminiwa na wananchi? hi wakisubiri sinema kamili watakapoishika dola?

Je, hofu ya CCM kwa wapinzani ni ya bure?
 
Hueleweki kbs! Yaani unataka kusema ccm ndo wanajua zaidi watanzania wanachotaka kuliko hata watanzania wenyewe!?

Au mi ndo sijakufahamu!?
 
Upinzani hawana nia ya dhati ya kuongoza nchi, na uwezo huo hawana .
Wanachofanya ni kuendelea kuwa wapinzani bila kuwa na dira wala muelekeo wa kupeleka nchi mbele kimaendeleo.

Wao wanataka wawe na nafasi tu fulani hasa ubunge na fursa zingine za kulamba asali wao na familia zao waishi vizuri na kujilimbikizia mali.

Hivyo CCM hawana hofu ya upinzani hata kidogo ikizingatia mikono yao imeshika kisu kwenye mpini.

Imagine kiongozi mkuu wa kile chama anapanda jukwaani kalewa bwiii...kwenye uzinduzi Mwanza.
 
Hueleweki kbs! Yaani unataka kusema ccm ndo wanajua zaidi watanzania wanachotaka kuliko hata watanzania wenyewe!?

Au mi ndo sijakufahamu!?
Swali langu kuu ni kwanini CCM inatawala kwa miaka 60 Sasa? Shida ni CCM, wananchi au vyama vya upinzani? Kama shida ni CCM kwanini iwe ni CCM, kama shida ni vyama vya siasa kwanini iwe vyama vya siasa na kama ni wananchi kwanini iwe ni wananchi? Kwanini CCM inafanya kila kitu kushinda uchaguzi, kwanini vyama vya siasa vya upinzani na wananchi hawafanyi kila kitu kushinda uchaguzi?
 
Una akili fupi sana. Ulisikia bashiru akisemaje kuhusu dola?
 
Una akili fupi sana. Ulisikia bashiru akisemaje kuhusu dola?
Akili fupi wanayo wapinzani. Katiba inawaruhusu kufanya siasa na hata kuandamana ikibidi lakini wanasubiri ruksa kutoka Chama Cha siasa kingine.
 
Back
Top Bottom