Ingekuwa Kuna nafasi ya kujaribu urais tungewapa miaka mitano upinzani ya kuwajaribu ila kwakuwa ni matarajio ya watu CCM inatosha

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Kuongoza nchi si kitendo Cha kusema tumpe nani nafasi tujaribu kuona atafanya nini ila kitendo Cha kuwa na Imani nani kabeba matarajio ya wapiga kura na wananchi Kwa ujumla.

Vyama vya upinzani Bado ni vichanga kiuongozi na ni mapema mno kutaka kuaminiwa Kwa Urais nafasi inayoamua hatima ya Taifa lolote Lile.

Nikitazama waliopo upinzani ambao kama wakishinda ,ndio wanaweza kuwa viongozi wa juu wa nchi naona ni kama kufanya majaribio ya uongozi. Bado wengi wao wanahitaji kukua na kubadilika.

Kutokana na udhaifu mkubwa inaonekana ndani ya upinzani ,nasisitiza ni mapema mno mno kuomba kupewa Urais.

Mambo kama :
i) kukosekana Kwa ukomo wa madaraka kwa nafasi za uongozi ndani ya vyama vyao yanapelekea Imani ya wanaamini ukomo wa madaraka kupunguza.

ii)Kukosekana Kwa ajenda kunafanya watu wapate mashaka kama watakuwa ajenda ya kusimamia wakipewa nchi.

iii) vyama kujikita katika maandamano nacho ni kuashiria Cha hofu waliyonayo wapenda amani.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanaonesha Bado upinzani ni mchanga na kupewa nchi ni kufanya jaribio la uongozi Kwa miaka mitano.

Kwa kuwa hakuna uongozi wa majaribio basi CCM INATOSHA.
 
Kwani nyinyi mliokaa madarakani kwa miaka zaidi ya 60 sasa mna maajabu gani? Hii nchi mpaka mlipoifikisha, hata kichaa anaweza kuitawala tu na siku zikaendelea kusonga.
 
Back
Top Bottom