HLRC kuiburuza serikali mahakamani kuhusu NSSF

Nijuavyo mimi huwezi ku retire kazi ukataka kuchukua fedha yako NSSF unapopenda. Kuna mashatri ya Umri wako na miaka ulolitumikia..Kama mfanyakazi haja qualify ktk makundi haya tuseme unaaxcha kazi ukiwa na umri wa miaka 45 na hujalitumikia taifa kwa miaka inayotakiwa - Huwezi kuchukua hata kama ukienda mahakama gani. Muhimu sana tuelewe vifungu vya sheria za NSSF kabla hatujaunga mkono maana unapojaza makaratasi na kujiunga kuna vipengele ambavyo watu wengi sana huwa hawavisomi..
Ebu pitieni site hii muone mfano.. Bofya

wewe chizi nini?
 
Nimeisoma sheria mpya hapo juu na kuona wapi mmesimama. Nadhani mnayo kesi maadam swala hili limepitishwa kinyemela...again kumbuka tu kwamba Ufisadi ndio unaendesha maisha ya watu nchini hivyo itakuwa kazi ngumu sana kushinda na hata kwenda mahakama za kimataifa sidhani kama watawaeleweni..

Nimecheck website ya NSSF wameshaondoa hilo fao kwenye list mafao yao. Lakini angalia PPF, (link) bado withdrawal benefit ipo! :: PPF Pensions Fund ::-

Kiini cha hii sheria mpya ni hali survival ya hii mifuko inakuwa shaky kutokana na serikali kukopa huko. NSSF wamekuwa kimbilio la wanasiasa, kila mradi wapo! Sasa 40 zimefika. Kisiasa, Mkandara hili litakuwa na madhara makubwa sana sana.
 
Kobello, hicho ndicho kinakosenakana. Kwa muda hizi social sucrity funds ziliziba hilo pengo -walau kwa watu wanaofanya kazi kwenye formal sector. Sasa wameondoa and people are left with nothing! In theory pension maana yake ni malipo ya uzeeni lakini kumuambia mtu mwenye umri wa miaka i.e 35yrs atapata hela zake mara atapofikia umria wa miaka 55 wakati hajui atapata wapi chakula kesho ni utani mbaya sana. In typical fashion, serikali yetu iko zaidi kwenye 'reactive', sheria imekuja ghafla, wafanyakazi hawakuambiwa in advance!

Kwa bahati mbaya kuna wafanyakazi wengi sana wako kwenye ajira ambazo zinaweza kukatika anytime i.e mining, na hakuna uhakika wa kupata kazi nyingine given the situation ya employment ilivyo nchini. Kupitia hii 'withdrawal benefit' wengi wao wanachukua na kuanzisha biashara. Sasa hivi wanaambiwa wasubiri hadi wafikie umri wa miaka 55!

Huu mpango is the worst thing the government can do right now. Na kusema waisitishe hii sheria nako si salama maana hii mifuko inaelekea kuzimu, serikali imekopa sana, they simply cannot maintain the status quo. Hawawezi kuendelea kulipa mafao ya kujitoa at the same wakopeshe serikali, and on top of that kuna uwekezeji unasukumwa na nguvu za kisiasa. Total Nightmare!

Hivi kweli wameshindwa kukusanya kodi kikamilifu kwenye madini,misitu,bahari,PAYE na vyanzo vingine vya uhakika?? kweli Late Mwalimu Kambarage alishalisema hili serikali legelege haikusanyi kodi inabaki kukimbizana na walala hoi tu!!
 
Kweli sio savings account, lakin

1. Kama serikali inaamanisha kujali tukifika uzeen je imewawekea bima wakulima wangapi? Na kiasi gani?

2. Kwa alieachishwa kazi akiwa na miaka 30 wakati akingojea kufika miaka 60

a) unamuhakikishia atakula wapi? Kumbuka hana kazi na mtaji wa biashara mmeuzuia

b) serikali inamkataba na mungu kujua urefu wa maisha ya watu au mtayalipa mkaburi?

3. Je nikwahuduma gan kwetu serikali inatoa kutuwezesha kufika huko kwa matumain? Afya hovyo, elimu hovyo, kila kitu hovyo.

Tushawishi kwa hoja sio kubwabwaja kishabiki. Kodi wanatukata zaid ya 30% huduma duni, hata hii akiba yetu wanaichuku pia.

4. Wazee wa afrika mashariki wamelipwa? Kama bado why? Hawajatimiza 55?

ACHA KUTETEA UFISADI
1. Wakulima wanahusikaje?
2. a)Mtaji wa biashara kivipi? ...huo si mtaji au savings account.
b)Mungu yupi? Kwani nani kasema mungu ndiye anayeua?

3)Tatizo ni retirment age au mfumo wa mfuko?
Acha kulalamika. Chacharika.
 
Nimecheck website ya NSSF wameshaondoa hilo fao kwenye list mafao yao. Lakini angalia PPF, (link) bado withdrawal benefit ipo! :: PPF Pensions Fund ::-

Kiini cha hii sheria mpya ni hali survival ya hii mifuko inakuwa shaky kutokana na serikali kukopa huko. NSSF wamekuwa kimbilio la wanasiasa, kila mradi wapo! Sasa 40 zimefika. Kisiasa, Mkandara hili litakuwa na madhara makubwa sana sana.
Hata mimi kabla ya kuja nilipitia NSSF nikaona mbona kila kitu kama huku majuu, hawa watu hawafahamu malipo ya uzeeni?.. ndio ngoma ilipoanzia.
 
Kweli sio savings account, lakin

1. Kama serikali inaamanisha kujali tukifika uzeen je imewawekea bima wakulima wangapi? Na kiasi gani?

2. Kwa alieachishwa kazi akiwa na miaka 30 wakati akingojea kufika miaka 60

a) unamuhakikishia atakula wapi? Kumbuka hana kazi na mtaji wa biashara mmeuzuia

b) serikali inamkataba na mungu kujua urefu wa maisha ya watu au mtayalipa mkaburi?

3. Je nikwahuduma gan kwetu serikali inatoa kutuwezesha kufika huko kwa matumain? Afya hovyo, elimu hovyo, kila kitu hovyo.

Tushawishi kwa hoja sio kubwabwaja kishabiki. Kodi wanatukata zaid ya 30% huduma duni, hata hii akiba yetu wanaichuku pia.

4. Wazee wa afrika mashariki wamelipwa? Kama bado why? Hawajatimiza 55?

ACHA KUTETEA UFISADI

Great Thinker
 
Hata mimi kabla ya kuja nilipitia NSSF nikaona mbona kila kitu kama huku majuu, hawa watu hawafahamu malipo ya uzeeni?.. ndio ngoma ilipoanzia.

Zamani NSSF ilikuwa inachukuwa wafanyakazi toka Private sector wakati PPF ikichukuwa toka public sector. Lakini sasa hivi sheria ilishabadilishwa na PPF anachukuwa kila upande, wakati huo huo tuna PSFP, LAPF. Siasa na biashara huwa haviendani vizuri sana, tumoena ATC, reli, sasa kinachotokea kwenye pension funds ni uendeshaji wa mifuko hii kwa pressure kubwa sana ya wanasiasa.
Hii sector ina mapungufu sana sana.
 
Well uchizi kila mtu anao wala sii sifa mbaya. Kama sheria ilikuwa vile na sasa imebadilishwa kuwa kama huku sijui mnachogombea maana sisi tunafukuzwa kazi kila siku na huchagia tunapopata kazi nyingine. Tz hakuna ajira, mfumo ulokwisha ulikuwa ulaji kwa watu na huu unaokuja ni ulaji vile vile..Chizi ni yule anayeweka fedha zake NSSF wakati anajua wazee wa EAC hawakulipwa ukifika miaka 60 kutakuwa na sheria nyingine tena.

Mkuu, labda sijakuelewa uko upande gani? Kama ni hivyo samahani sana. Hii sheria ya kipumbavu mimi siitaki na hata iliyopita zote haziko sawa. Hela yangu wanaikopesha serikari for what???? CCM na mlaaniwe na kizazi chenu chote. Hii kitu imeniuzi sana
 
1. Wakulima wanahusikaje?
2. a)Mtaji wa biashara kivipi? ...huo si mtaji au savings account.
b)Mungu yupi? Kwani nani kasema mungu ndiye anayeua?

3)Tatizo ni retirment age au mfumo wa mfuko?
Acha kulalamika. Chacharika.

Wakulima wakizeeka.
Nin maana ya bima hii?

Wakulima wanachangia pato la taifa kwa asilimia kubwa wawapo na nguvu

Kama serikali inahuruma na wafanyakazi wakizeeka wasipate shida kwa bima, je wakulima hawaihitaji hiyo huruma kwa maana ya kuwekewa bima?
Kumbuka tunaangalia uhalali wa hii huruma ya serikali.

Kijana aliyetimliwa kazin akichukua akiba yake nimtaji tosha kuanza maisha mapya endapo hajabahatika kazi nyingine, ukimzuia afanye nin? Akaibe?
umeelewa?
 
Katika nchi hii kuna mambo ya ajabu sana, na hili ni mojawapo. Wafanyakazi katika sheria hii mpya wana mambo muhimu ya kujiuliza:

Upitishwaji wa Sheria Hii Mpya
Sheria zote zinazopelekwa bungeni ikiwa pamoja na marekebisho yake, wadau hupewa na nafasi ya kuzijadili na kutoa maoni yao kabla ya kujadiliwa bungeni. Kwa nini mabadiliko ya sheria hayakujadiliwa, yakapitishwa kinyemela bila ya kupata maoni ya wenye mifuko yao? Wamiliki wa mifuko hii ni wafanyakazi, wala si serikali maana serikali haichangii chochote katika mifuko hii.

Uzuri ya Mabadiliko Haya
Wafanyakazi ni watu wenye akili timamu, si punguani wala si watoto kiasi cha kuonekana kuwa kuna watu wengine wanaojua uzuri na faida ya mabadiliko haya zaidi ya wafanyakazi wenyewe. Wafanyakazi wana haki ya kuamua kwa utashi wao juu ya nini kilicho na manufaa kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye, haki hiyo haipo kwa serikali wala bunge au chombo kingine chochote. Kama mabadiliko haya yanafanywa kwa manufaa ya wafanyakazi kwa nini manufaa hayo yasipelekwe kwa wafanyakazi ambao ndiyo wadau wakubwa, wakayadili na kuona faida badala ya kuyapitisha kwa siri?

Wafanyakazi Kunyang'anywa Pesa Yao
Mifuko hii inatunza fedha za Wafanyakazi, si fedha ya serikali. Lakini mifuko inavyoendeshwa hapa Tanzania, imefanywa kuwa ni pesa za serikali na hivyo serikali kuamua kuzitumia pesa hizo kadiri inavyotaka au hata kuiwekea sheria na kanuni bila ya ushiriki kamilifu wa Wafanyakazi ambao ndiyo wachangiaji wa mifuko hii.

Serikali imeifanya mifuko hii ndiyo hela ya serikali ya kuendeshea miradi mikubwa ya maendeleo bila kuangalia faida watakayopata wachangiaji wa mifuko hii kwenye hiyo miradi ya maendeleo.

Mifuko hii haipo kwaajili ya kuendesha serikali au kugharamia miradi ya serikali, jukumu lake la kwanza ni kuangalia manufaa ya wanachama wake ambao ni Wafanyakazi lakini haki hii ya msingi ya wanachama wa mifuko hii imeporwa na serikali.

Njama za Kuwaibia Wafanyakazi
Faida zinazotajwa na wanaotetea mabadiliko haya ni za kinadharia sana. Katika nchi ambayo ni 6% tu ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi ndiyo walioajiriwa kwenye sekta rasmi, uhakika wa mfanyakazi kuwa katika ajira wakati wote mpaka kufikia umri wa miaka 55 au 65 ni mdogo sana.

Wafanyakazi wengi kwenye sekta binafsi wanafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, na baada ya kumaliza mikataba yao hakuna uhakika wa kupata ajira tena. Mathalani mfanyakazi ameajiriwa mara moja kwa kipindi cha miaka 2, ni vipi atanufaika na mabadiliko haya?

Na wakati huo atakapofikisha miaka 55 (kama atafika) atapata nini wakati thamani ya shilingi inaporomoko kila siku na huku mfumko wa bei ukikua kwa kasi ya ajabu? Ndiyo maana mabadiliko haya hayana manufaa kwa wanachama wa mfuko bali ni njia nyingine ya kupokonya hela ya mfanyakazi kwa kutumia lugha ya udanganyifu.

Kilio cha wafanyakazi wa Tanzania ni kodi kubwa ya PAYEE, badala ya serikali kusikiliza kilio hiki cha wafanyakazi, imezidi kuwapokonya hata kile kidogo walichokuwa nwakipata wamalizapo mikataba yao ya kazi.

Baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakitumia mafao haya kuanzishia miradi midogo midogo, wengine huyatumia kwa kujisomesha na wengine hata kuwasomesha watoto wao ambao kwa vipato vyao vya mwezi wanashindwa kufanya hivyo.

Serikali kwa sasa inachukua karibu 20-30% ya mshahara wa mfanyakazi kama PAYE, sasa imeamua kuchukua tena 20% ya mshahara wa mfanyakazi. Hii ina maana sasa serikali itakuwa ikichukua karibu 40-50% ya pesa yote ya mfanyakazi.

Hoja ya Kuiga Mfumo wa Mataifa Mengine
Kati ya sababu zinazotolewa ni kuwa mfumo huu mpya unafuata maelekezo ya ILO na jinsi nchi nyingine zinavyofanya. Undumilakuwili wa serikali ni kama ifuatavyo. Tumekuwa tukiongelea matumizi mabaya ya fedha za umma yanayofanywa na serikali na watendaji wake.

Kwa mfano katika serikali kukifanyika kikao wanalipana posho ya malazi na chakula, na posho ya kukaa. Posho hii ya kukaa hailipwi na nchi yoyote iliyoendelea, ukiwauliza kwa nini wasifuate taratibu zinazofuatwa na mataifa mengine, jibu ni kuwa 'sisi ni taifa jingine na hivyo hatulazimiki kufuata taratibu za mataifa mengine'.

Mataifa ya wenzetu kiongozi yeyote ambaye taasisi yake inakumbwa na kashfa, lazima mkuu wa kitengo hicho huwajibika, lakini hapa kwetu ukiwauliza kwa nini tusifuate mfumo huo wa wenzetu, tunaambiwa hutulazimiki kufuata mifumo hiyo maana sisi ni Taifa huru ambalo halilazimiki kufuata taratibu za mataifa mengine, na yapo mengi ya namna hiyo.

Inapokuja kwenye suala la kumkamua mfanyakazi, ukiuliza juu ya kodi kubwa anayokatwa kwenye PAYE, utapewa takwimu za kodi za mataifa mengine (hapo haielezwi tena kuwa sisi ni Taifa huru lisilohitaji kufuata juu ya nini mataifa mengine yanafanya). Kwenye hili la mifuko ya jamii nalo wafanyakazi wanaambiwa kuwa ndivyo mataifa mengine yanavyofanya.

Wakati katika uhalisia mataifa hayo yana uhakika mkubwa wa ajira kwa watu wake, yana umri mkubwa zaidi wa tegemeo la kuishi, sarafu zao ni imara, na mfumko wa bei upo chini sana ukilinganisha na Tanzania.

Serikali iache kuendekeza mambo yanayowadhulumu wafanyakazi wakati huo huo ikiyatetea yale yenye kuwanufaisha viongozi wa serikali.

Wafanyakazi Wanatakiwa Kufanya Nini?

Wafanyakazi Wamiliki Mifuko Yao
Wafanyakazi, katika katiba mpya wahakikishe inaingizwa kwenye katiba mpya kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni mali ya wafanyakazi na itasimamiwa na wafanyakazi wenyewe kwa kupitia vyama vyao vya wafanyakazi.

Mifuko hii itakapokuwa chini ya wafanyakazi wenyewe itaweza kufanya kazi kwa manufaa ya wanachama wake, itaweza kuanzisha vitega uchumi ambavyo vitamwezesha mwanachama kuwa na gawio la faida maisha yake yote kwa kutegemeana na kadiri alivyochangia.

Kwa kiasi cha pesa kinachopatikana kwenye mifuko hii kuna uwezekano mkubwa wa wafanyakazi wanapoondoka kazini kupewa pesa yao yote waliyochangia, na bado wakaendelea kushikilia hisa katika vitega uchumi kutokana na faida zilizopatikana.

Hili litaondoa wajumbe wa bodi na wakurugenzi wanaoweza kuteuliwa kwa manufaa ya kisiasa na kisha wakaamua kuwatumikia waliowateua kuliko wanachama wa mifuko.

Kudai Ripoti ya Mchakato wa Mabadiliko ya Sheria
Wafanyakazi kwa kupitia vyama vyao vya wafanyakazi wadai taarifa juu ya mchakato wa namna mabadiliko yalivyofikiwa. Kama ikigundulika kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi walishirikishwa lakini wao hawakuwashirikisha wafanyakazi, viongozi wote wa wafanyakazi wafukuzwe kwenye nafasi zao.

Kama hilo halitawezekana, basi wafanyakazi wote wajitoe kwenye uanachama wa vyama vyote vya wafanyakazi na kuunda vyama vingine vyenye kufanya kazi kwa manufaa ya wanachama wake na siyo kwa manufaa ya serikali.

Njia za Kisiasa
Wenzetu katika mataifa yaliyoendelea, ikifika wakati wa uchanguzi makundi mbalimali huweka bayana matakwa ya kundi lao, na hutoa tamko kuwa, 'sisi kama kundi mojawapo la kijamii, tutamchagua kiongozi au chama kitakachosimamia au kufanya mambo 1) -----, 2) ----n.k.'. Wafanyakazi wa Tanzania, sasa ni wakati wa kuungana na kuachana na ushabiki wa kisiasa na badala yake kama kundi mojawapo la kijamii kuangalia maslahi ya kundi letu.

Ifike mahali, kama wafanyakazi wa Tanzania tutamke kuwa, 'wafanyakazi wote tutakiunga mkono chama au mgombea ambaye atashusha PAYE kwa 25% kutoka ilipo sasa na kwa namna yeyote ile mtu asilipe PAYE inayozidi 20% ya mshahara wake.

Pili tuseme kuwa tutamchagua kiongozi au chama kitakachokuwa tayari kuiachia mifuko ya kijamii irudi kwa wanachama wake na iendeshwe na wanachama wenyewe.

Wafanyakazi wa Tanzania tukiendekeza siasa na ushabiki wa vyama, wanasiasa wataendelea kuwachezea wafanyakazi miaka yote huku wao wasiozalisha wakijipangia maslahi mazuri na mazingira ya malipo starehe huku mchangiaji mwenyewe akibakia hoi bin taabani.
 
Nimeisoma sheria mpya hapo juu na kuona wapi mmesimama. Nadhani mnayo kesi maadam swala hili limepitishwa kinyemela...again kumbuka tu kwamba Ufisadi ndio unaendesha maisha ya watu nchini hivyo itakuwa kazi ngumu sana kushinda na hata kwenda mahakama za kimataifa sidhani kama watawaeleweni..

Hakuna sababu ya kukata tamaa mapema. Mara ya kwanza wafanyakazi walishinda. Na ni kutokana na maamuzi ya mahakama ndiyo maana mifuko hii ililazimika kuendesha schemes mbili kwa wakati mmoja. Sina uhakika ni kwa namna gani serikali imejilinda katika sheria hii mpya ili kuweza kushinda mahakamani.

Tatizo kubwa hapa siyo huu mpango bali ni dhamira chafu ya serikali na mifuko yenyewe iliyojificha nyuma ya mpango wenyewe. Kwa muda mrefu, serikali imekuwa na matumizi ya ovyo, wizi, ubadhirifu na ufisadi kiasi kwamba kila mara imekuwa haina fedha za kutekelezea miradi ya maendeleo. Mahali pekee ambapo wamekuwa na uhuru wa kuchota fedha kadiri wapendavyo ni kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Sasa imefikia mahali mpaka mifuko hii kuanza kuwa na hofu ya kushindwa kuwalipa wanachama wao wanapoacha kazi. Ili kukabiliana na hilo serikali imeleta hii sheria mpya ambayo ina maneno matamu lakini dhamira yake ni kuhakikisha wafanyakazi wengi hawapati mafao yao, maana inajulikana kuwa wanachama wengi hawana uhakika wa ajira.

Mathalani mtu ambaye amefanya kazi miaka 5, akachangia kiasi cha sh. milioni 10 kutokana na mshahara wake wa 450,000 kwa mwezi, akaachishwa kazi akiwa na umri wa miaka 30, atalazimika kukaa miaka 30 kabla ya kupata mafao yeyote ya mfuko, na itakpofika hiyo miaka 30, hii milioni 10 kwa wastani wa inflation ya 20%, itakuwa ni sawa sawa na sh. 100,000 ya sasa. Mwanachama huyu baada ya miaka 30 ule mshahara wake wa sh 450,000 kwa mwezi utakuwa ni sawa na sh. 45,000. Mafao yake kwa mwezi itakuwa ni 60% ya mshahara ule alioachia kuchangia. Hivyo atakachokipata itakuwa ni sawa na 60% ya sh. 45,000 ya leo ambao ni sh. 27,000 ya leo. Mwanachama huyu hata akibahatika kuishi miaka 10 zaidi atakachokipata ni sawa na sh. 27,000 x 12 x 10; ambayo ni sawa na TSH. 3,240,000 ya sasa. na hivyo NSSF/Serikali wana uhakika wa kupata karibu 7 milioni ya bure lakini ukweli ni kuwa ni wachache sana watafikia miaka hiyo ya 60 achilia mbali kuishi miaka 10 baada ya 60. Kwenye mpango huu kwa mazingira ya Tanzania, ni kuipora hela ya mwanachama.

Kwa kuujua ukweli huu ndiyo maana wanachama wengi hawataki ile scheme ya pension, na hivyo huamua kuchukua kiasi walichochangia na kwenda kuanza maisha yao mapya, maana hata ukisema uiache, hela hiyo haitaweza kukusaidia chochote siku za mbeleni maana itakuwa haina thamani. Hela ambayo leo mfanyakazi akiichukua angeweza kununua mabati 10 baada ya miaka 30 itaweza kununua mikate 20. Ni mtu mpumbavu pekee yake anayeweza kukubali hela yake ikae mahali kwa miaka zaidi ya kumi kwenye uchumi wenye inflation ya zaidi ya 20% halafu ukaamini kuwa nina akiba. Aheri uwekeze kwenye miradi uchwara ambayo itakuwa inakupa mapato madogo madogo lakini yanayoendana mfumko wa bei wa wakati huo.

Mimi mafao yangu ya kwanza yalikuwa sh. 20 milioni, kutokana na hela hiyo nilinunua eneo la ekari 7. Baada ya miaka 4 serikali ililichukua eneo hilo kwa kutangaza kuwa eneo hilo siyo la mashamba tena bali ni la makazi. Kwa fidia ya serikali nililipwa sh. 70 milioni, na nikaachiwa kiwanja kimoja ndani ya eneo hilo. Hivi ningeiacha hiyo 20 milioni mpaka leo, ingenisaidia nini? Mafao yangu ya pili nilipata kama millioni 50 hivi, pamoja na mambo mengine, nimeweza kupata shamba la ukubwa wa ekari 200. Hapa najua nimewekeza, na thamani ya hela yangu inazidi kukua kila siku kuliko mtu yeyote aliyefungia pesa yake NSSF. Mimi hela ya kwangu ina appreciate wakati yule aliyeiacha NSSF ina depreciste.

Jambo linaloudhi zaidi, wafanyakazi wa NSSF kuanzia mameneja wa matawi wamekuwa wakijikopesha mpaka milioni 300 (huku wachangiaji wakinyimwa)ili waweze kutetea sera za wizi wa mifuko hii mbele ya wachangiaji.
 
To make the matter simple, kujiunga na mifuko hiyo isiwe lazima. Kila mtu aamue mwenyewe. Katika nchi ambayo social security iko largely family oriented, ukimwambia mtu unakaa na pesa zake mpaka afikishe miaka 60 ni dhuluma ya wazi kweupe!!! Unajua kitakachofuata? watasema hata ukifisha hiyo miaka 60 hupewi pesa zako kwa mkupuo, unapewa kiasi fulani kila mwezi. Kinachofanyika sasa hivi katika hii mifuko ni kutoka kuzuri kuelekea kubaya, tulipokuwa ni bora zaidi kwa mfanyakazi kuliko tunakoelekea...
 
serikali haina pesa na huwa inaponea kwenye mifuko hii ya hifadhi kwa kukopa.so dawa hapa nikuanzisha mifuko tutakayosimamia wenyewe.kama ni wafanyakazi wa viwandani tuwe na mifuko yetu, wa madini vilele, wakulima vilele , wavua samaki ,wafanyakazi waserikali wao wabaki na sheria inayowapa umri huo wa kustafuu maana ajira zao ni za kudumu .
 
serikali haina pesa na huwa inaponea kwenye mifuko hii ya hifadhi kwa kukopa.so dawa hapa nikuanzisha mifuko tutakayosimamia wenyewe.kama ni wafanyakazi wa viwandani tuwe na mifuko yetu, wa madini vilele, wakulima vilele , wavua samaki ,wafanyakazi waserikali wao wabaki na sheria inayowapa umri huo wa kustafuu maana ajira zao ni za kudumu .

Good Idea iwe kama vile Saccos zinazofanya kwenye makampuni kwamba mfanyakzai unaweza kukopa kwenye saccos na kufanya mambo>
 
Kituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kimesema kinaandaa taratibu za kuiburuza serikali mahakamani kwani kumkatalia mwanachama kuchukua hela zake kwa vile hajafikisha miaka 60 ni ukiukwaji wa haki za binadamu.Hii ni kwa sababu hakuna makubaliano yaliyofanyika kati ya mifuko husika na wanachama ili kuleta sheria hii ambayo ni mbaya na haramu hasa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
HLRC imeomba ushirikano wa wafanyakazi wote kufanikisha azma hii.

Source:Habari BBC Jioni.

My take:
Sheria hii ya NSSF ni kitanzi kwa wafanyakazi kote nchini hasa wa sekta binafsi kutokana na ukweli kwamba makampuni mengi binafsi yamekuwa yakiwaachisha mara kwa mara wafanyakazi wake huku kukiwa hakuna utetezi wowote wa serikali.Ni vigumu sana wafanyakazi kuunga mkono sheria hii kutokana na ukweli kwamba mtu akiacha kazi akiwa na miaka 30 itampasa kusubiri miaka 25 ili apate mafao yake.Huo ni uendawazimu.

Na ukichunguza zaidi life expectance ya mTZ ni miaka 53 sasa sijui hizo hela wanataka wajekumfaidisha nani hapo baadae
 
acha kutoa majibu ya kifisadi....na je nikipunguzwa kazi ndani ya miaka 30? kwa hiyo nisubiri hadi miaka 55? pamoja na hayo yiote hiyo ni jasho langu nina haki ya kuidemand mda wowote nnaotaka..

Gazeti la Nipashe na Daily News ya leo yameandika habari hii. Eti wanadai ilipitishwa tarehe 13 April mwaka huu na rais ali-sign. Nina uhakika alikupitishwa bungenbi kwani hili ni jambo nyeti na kama lingepita bungeni ni dhaili kwamba watu tungesikia au kupata taarifa. Kwa kweli aingii akilini kabisa!!!! Siku moja tutashinda lakini. Hivyo naunga mkono hoja kwa HLRC kwenda mahakamani kuishitaki serikali.
 
Bams,
Nakuelewa lakini hizo hesabu zako babu kali sana..millioni 10 kwa miaka 5 ni amlost half the salary.. anyway..NSSF na mifuko mingine yote ya uzeeni ni catch 22. Ni wizi mbaya sana kwa jamii tena naona wewe umetumia vitabu kuliko hali halisi.. Ukweli ni kwambafedha yetu inashuka thamani kuliko maelezo na mifano iko wazi kabisa.

Nakumbuka miaka 10 ya Mwinyi alipoondika Dollar ilikuwa 1 kwa Tsh 500 na Mkapa ilikuwa dollar kwa Tsh 1000, leo tuna JK ni Tsh 1600 bado ana miaka 3 itafika 2000 tu maana fedha yetu hushuka mara 100 kila miaka 10.
Hivyo mchukulie yule mtu alofanya kazi wakati wa Mwinyi na anasubiri hiyo miaka 30 matlan ndiye aliweka hizo Tsh millioni 10 (eq.Usd 20,000) kwa miaka 5 chini ya utawala wa Mwinyi.. Ilipofika 2005 wakati wa Mkapa zilikuwa Usd 10,000 na zitaishia wakati wa JK 2015 kuwa sawa na Usd 5,000 tu..Huyu mtu kweli atalipwa vipi wakati fedha yake ndio imejenga mambo kibao ya kibiahsara kwa thamani ya wakati ule. Na kile walichokijenga NSSF kinapanda thamani kila kukicha lakini sio fedha ya mwekezaji..

I mean hili ni linchi la Wajinga. maadam hakuuuondoa ujinga tunakwenda nao sambamba. Kodi zetu zinalipa mishahara, magari, mafuta, usafiri na posho za waheshimiwa halafu tena fedha mnayowekeza kwa malipo ya uzeeeni ndio inajenga madaraja, majengo ya kibiashara na miundombinu tunakopeshwa ni deni la kizazi kijacho..
 
Back
Top Bottom