HLRC kuiburuza serikali mahakamani kuhusu NSSF

hiki ni kipimo cha mshikamano wa wafanyakazi...wanaosapoti swala hili ntawashangaa sana
 
Kwa kweli ndiyo nimegundua ndio maana yule kijana wa tunisia ndiyo maana alijichoma moto hivi Tucta wako wapi?
 
Nakwambia tutauana kwa swala hili,haiwezekani kodi wanatukamua kiasi kile halafu na hii hela wanaitaka,kwa kweli hata kwa fikra za kawaida hii si haki hata kidogo hatuwezi kukubali,LHRC tusaidieni hawa mafisadi wanataka kutumaliza
 
ila huu ni utapeli wa wazi wazi jamani..io miaka 60 kwa magonjwa ya saiz nani atafika jamani, huu ni wizi kwa watu wasio na hatia kabisa. kweli mwenye nacho hujiongezea na hasie kua nacho uporwa ata iko kidogo chenyewe
 
Mkandara, tupo Tanzania, siyo Marekani. Mara ya kwanza ilipopitisha sheria ya kufuta NPF na kuanzisha NSSF walipitishwa sheria hiyo ya kutokujitoa kwa mwananchama ambaye hajafikisha retirement age, wafanyakazi walienda serikali na walishinda. Hivyo kukawa na schemes mbili zilizokuwa zikienda sambamba, ile inayoruhusu kujitoa na ile ya pension. Safari hii tena wanataka wawajaribu wafanyakazi, nina hakika serikali kutokana na nia yake ovu, lazima itashindwa.
Samahani. sijakuelewa vizuri.. Unaposema ilifutwa NPF na kuanzishwa NSSF wakatoa mwanya kwa wale ambao hawajafikisha umri wa ku retirement wanaweza kuchukua fedha zao sio? Je, ilikuwa hata baada ya kujiunga na NSSF, bado utakuwa unajitoa NPF... au kama hukujitoa baada ya unafuata sheria mpya za NSSF.. Sidhani kama sheriaa inaweza kuwa ina hang kusubiri watu wa NPF ilokufa, wafanye maamuzi wakati wanachangia NSSF shirika jipya..

Na zaidi ya hapo karibu kila mfanyakazi alikuwa member wa NPF sasa sielewi unaposema wana scheme mbili zinazoenda sambamba wakati NPF ilishakufa. Hii kidogo haijakaa sawa.. kuchukua miaka yako ya ajira sawa lakini bado unaruhusiwa kuacha kazi na ukachukua mafao yako wakati wowote hii mkuu wangu kuna walakin..
- Nielimishe zaidi.
 
ukiwa 65yrs old, na umeshakula mafao yako unakuwa mzigo kwa private sector au jamii?
acha kutoa majibu ya kifisadi....na je nikipunguzwa kazi ndani ya miaka 30? kwa hiyo nisubiri hadi miaka 55? pamoja na hayo yiote hiyo ni jasho langu nina haki ya kuidemand mda wowote nnaotaka..
 
Busara itumike, fedha niyetu, vipi wanasiasa wanatupangia tuchukue lini fedha zetu?

Mbona wakulima wakizeeka serikali haijawawekea bima yoyote? Au wakulima wazee hawahitaji bima?

Kikwete na chama ccm ni wezi tu. Wameifilisi serikali, sasa wanatugeukia mpaka kwenye hifadhi zetu.
 
Mnajua maana ya Social Security?

Mtu anaweza kujikopesha na kisha kuirudishia hiyo hela. In other word, mtu anaweza kwenda NSSF kuomba mkopo wa fedha yake lakini anatakiwa kuirudisha kwa kipindi fulani. Lakini suala la kuwazuia watu kutochukuwa kabisa pesa yao huku mashirika yakizifanyia biashara bila wanachama kupata faida, kweli hai-make sense.
 
Kituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kimesema kinaandaa taratibu za kuiburuza serikali mahakamani kwani kumkatalia mwanachama kuchukua hela zake kwa vile hajafikisha miaka 60 ni ukiukwaji wa haki za binadamu.Hii ni kwa sababu hakuna makubaliano yaliyofanyika kati ya mifuko husika na wanachama ili kuleta sheria hii ambayo ni mbaya na haramu hasa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
HLRC imeomba ushirikano wa wafanyakazi wote kufanikisha azma hii.

Source:Habari BBC Jioni.

Way to go HLRC; tunaomba leadership jinsi ya kusonga mbele.
 
Busara itumike, fedha niyetu, vipi wanasiasa wanatupangia tuchukue lini fedha zetu?

Mbona wakulima wakizeeka serikali haijawawekea bima yoyote? Au wakulima wazee hawahitaji bima?

Kikwete na chama ccm ni wezi tu. Wameifilisi serikali, sasa wanatugeukia mpaka kwenye hifadhi zetu.
Serikali DHAIFU inakwepa jukumu la kuwahudumia wazee uzeeni...kwa hili la mafao yetu...LIWALO NA LIWE....
 
Mnajua maana ya Social Security?

Kobello, hicho ndicho kinakosenakana. Kwa muda hizi social sucrity funds ziliziba hilo pengo -walau kwa watu wanaofanya kazi kwenye formal sector. Sasa wameondoa and people are left with nothing! In theory pension maana yake ni malipo ya uzeeni lakini kumuambia mtu mwenye umri wa miaka i.e 35yrs atapata hela zake mara atapofikia umria wa miaka 55 wakati hajui atapata wapi chakula kesho ni utani mbaya sana. In typical fashion, serikali yetu iko zaidi kwenye 'reactive', sheria imekuja ghafla, wafanyakazi hawakuambiwa in advance!

Kwa bahati mbaya kuna wafanyakazi wengi sana wako kwenye ajira ambazo zinaweza kukatika anytime i.e mining, na hakuna uhakika wa kupata kazi nyingine given the situation ya employment ilivyo nchini. Kupitia hii 'withdrawal benefit' wengi wao wanachukua na kuanzisha biashara. Sasa hivi wanaambiwa wasubiri hadi wafikie umri wa miaka 55!

Huu mpango is the worst thing the government can do right now. Na kusema waisitishe hii sheria nako si salama maana hii mifuko inaelekea kuzimu, serikali imekopa sana, they simply cannot maintain the status quo. Hawawezi kuendelea kulipa mafao ya kujitoa at the same wakopeshe serikali, and on top of that kuna uwekezeji unasukumwa na nguvu za kisiasa. Total Nightmare!
 
wanaanzia wapi?

Nataka nikawachangia na mchango wa mafuta ya gari lol

yaani PAYE haiwatoshi sasa NSSF?
 
Kituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kimesema kinaandaa taratibu za kuiburuza serikali mahakamani kwani kumkatalia mwanachama kuchukua hela zake kwa vile hajafikisha miaka 60 ni ukiukwaji wa haki za binadamu.Hii ni kwa sababu hakuna makubaliano yaliyofanyika kati ya mifuko husika na wanachama ili kuleta sheria hii ambayo ni mbaya na haramu hasa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
HLRC imeomba ushirikano wa wafanyakazi wote kufanikisha azma hii.

Source:Habari BBC Jioni.

naunga mkono kwa asilimia mia tatu,maana hizi zote ni njama za ccm kutafuta fedha za kampeni.maana upande wa pili tunakubali kukatwa mishahara yetu ili unapokuwa huna kazi zikusaidie. Jk unasainisaini document bila kuangalia mbele we ndiye mwenye mikataba yetu na mungu? Kama mbwaimbwai bwana, Raisi ***** kweli hili sijui linawaza nini kichwani kwake
 
acha kutoa majibu ya kifisadi....na je nikipunguzwa kazi ndani ya miaka 30? kwa hiyo nisubiri hadi miaka 55? pamoja na hayo yiote hiyo ni jasho langu nina haki ya kuidemand mda wowote nnaotaka..
Hiyo ni tax exempted, ni ahadi yako kwa jamii kuwa utaweza kujitegemea pindi mgongo ukianza kupinda, ukipunguzwa kazi ujanani tafuta nyingine. Hiyo siyo savings account.
 
MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI. . . ni vile tu naiogopa ban la sivyo ningewatus hawa mafisadi mpaka server ingekuwa slow. angalia PAYE walivyoipandisha, haitosh na NSSF & PPF zetu pia watupangie muda wa kuzichukua jaman jaman jaman tumechoka kunyanyasika.

Hapo bado unaambiwa uwe mzalendo kwa kuipenda nchi yako. ukisoma nje ya nchi unaambiwa urudi kuitumikia nchi yako. wallah kwa style hii ngoja tu nifanye mchakato wa kwenda kufanya kaz nje ya nchi.

Nikifikisha 55yrs ntarud kuchukua vijisent vyangu!
 
Back
Top Bottom