Hiyo link sio sahihi. Ni ya watumishi wa serikali ambao kwa hapa Tanzania wapo chini ya GEPF. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Pension fund and provident fund. Kwa wenzetu hata watumishi wa serikali hawapeleki michango provident kwa vile mafao ni madogo wanapeleka pension scheme maalum ndio maana ina hizo sheria. Kama hufahamu serikali huwa haipeleki michango kwenye pension scheme licha ya makato ila wanalipa kwa fungu la bajeti wakishajua idadi ya watu wanaostaafu mwaka huo.
Dah ama kweli nyie wagumu sana kuelewa poicha nzima mnaliwa vipi.. Nikuulize NSSF ni chombo cha serikali au sio? Ni mpango wake ni private pension plan au umepitishwa na serikali?. mbona mnajipinga wenyewe kwa kila hatua au hamfahamu kilichopo mbele yenu..
Serikali ipo juu ya watumishi wa Umma na mashirika binafsi maadam kuanzishwa kwa NSSF kumetokana na serikali na sheria kutungwa na bunge. Ndio maana HLRC wanaona uvunjaji wa sheria kwa mtazamo wa zile pension schemes wakati NSSF sio private corporate ni mali ya serikali (shirika la Umma) linalomilikiwa na serikali na linatakiwa kutoa huduma sio kufanya biashara.
Private Pension plan zipo za kila aina huku kuna za walimu (Teachers Pension Plan) na hata mashirika kama la simu Bell lina Pension plan zake. Mabenki na financial institution kibao zinafanya biashara kupitia michango ya watu ktk malipo ya uzeeeni lakini haya ni mashirika binafsi - Corporates. Hawa huchagua Board of Directors, wana vikao, na mikutano yao na siku shirika likienda chini insurance company za benki kubwa ndio huwajibika kulipa madeni na sio serikali..Hakuna kitu kinajadiliwa bungeni wala kusubiri saini ya rais ili iwe sheria.. they are private. Ukirudi kwa NSSF unakuta story tofauti kabisa..Hili ni serikali kupitia shrika la Umma linaloendesha biashara ya uwekezaji for profit kama private corporate kinyume kabisa..
Tatizo sio kwamba NSSF inashughulika na kina nani.. iwe watumishi wa mashirika binafsi au ya Umma swala ni NSSF yenyewe ni shirika gani na linamilikiwa na kudhaminiwa na nani kama sio serikali?..Mashirika yote haya nyumbani ni ya serikali na ndio maana sheria zake zinapitishwa bungeni, hizi ni SOCIAL SECURITY programs zinayoandaliwa na serikali kutokana na michango na earnings ya raia waajiriwa na hapa ndipo mliposhindwa kuona ndani..
Kwa hiyo HLRC wana kesi kwa sababu sheria za chombo chochote cha serikali ktk maswala ya social security ni lazima sheria zipitishwe na bunge, na wakati mwingine huhitaji kura za maoni ya wananchi kubadilisha sheria hizo wengine huweka 2/3 ya population lakini katika hili la NSSF hatukuona utaratibu huo ukifanywa isipokuwa tunaona kwamba sheria imepita na kuwekwa saini na rais. Tuna ushahidi to support hizi claims ? sina hakika maadam walipitisha bungeni, kisha rais akaweka saini na hivyo kuwa sheria kuna cha ziada kilizokiukwa?.. Na maadam katiba inampa mamlaka makubwa sana rais kuchezea sheria na taratibu sijui kama kuna sheria itakayo pindua maamuzi ya rais ikiwa bunge lilikwisha pitisha..Mahakama ni sehemu tu ya utawala ule ule ulotunga sheria hizi..
Mkuu wangu NSSF na hizo PPF zina operate kama private pension plan wakifanya biashara na fedha ya watu na mlaliwa kweli vile. Kifupi serikali inafanya biashara badala ya MSSF kuwa private co, au basi ingekuwa mfuko unaotoa huduma ya uzeeeni na sio biashara..Badala ya Insurance companies kuwa wadhamini wa scheme hii unakuta serikali ndio wamiliki na wadhamini ikifa sisi ndio tutaingia ktk deni hilo.. Mawili NSSF ikienda chini tutalazimika Watanzania wote kulipia au wanachama wake kuzikwa maana utaenda ishitaki wapi serikali inapofanya biashara?..
Hizi vyombo vyote vya serikali vinavyofanya biashara wakati uongozi wake na board of directors ni watu waliochaguliwa wengine wabunge na mawaziri ni mchezo mchafu sana kwa Taifa..Ni rahisi ksuema mtaishitaki NSSF lakini wakati huo huo hamkujua kama ni mradi wa serikali ambayo ndio mnataka kuiweka kizimbani..