Kiongozi, hii mifuko ina idara za masoko na wanasaka wanachama kama insurance salesmen. Na wakifika kwako watakuelezea mafao wanayotoa na why you should choose mfuko wao na sio wa mwingine. Hiyo withdrawal benefit ipo na wanakuelezea in great details, kwa hiyo mtu anajiunga akiwa na fahamu kamili. Kumbuka hili fao lilikuwepo kisheria.
Bado kuna jambo sijelewa kwenye hii sheria mpya ikoje. Kila benefit ina sifa/criteria zake. Na fao la pension (malipo ya uzeeni) ni lazima uwe umechangia kwa miaka si chini ya 10. Chini ya hapo huwezi kupata malipo ya pension. Sasa kama wanasema kila mtu atachakuwa pension how about those ambao hawajachangia kwa miaka 10? Kwa mfano mtu alipoteza ajira akiwa amechangia kwa miaka 6 au 7 na hakupata tena ajira, what will happen?