Wafanyakazi wajue maana ya Social Security au wasijue is irrelevant. Jambo la muhimu ni kuwa hela hiyo ni michango ya wafanyakazi. Namna gani itawasaidia, wao ndiyo wanaojua, na serikali haina haki yeyote kuifanya hela ya wafanyakazi kuwa mfuko wa kutekelezea miradi ya maendeleo. No way. Nadhani serikalini bado kuna watu ambao wapo kwenye usingizi mnono wa kukosa fikra, wakifanya kazi ya ku-copy mambo machache kutoka mataifa mengine bila ya kujifunza na kutambua mambo hayo yatafanya kazi vipi katika mazingira yao.
Wewe katika nchi yako, watu wenye ajira rasmi hawafikii hata 10% halafu unasema mfanyakazi asipate mafao mpaka afikishe umri wa miaka 60, wewe una akili au tahira? Nchi ambayo mfumko wa bei ni zaidi ya 20% halafu umwambie mfanyakazi aliyeachishwa kazi akiwa na umri 30, halafu eti asubiri kwenda kuchukua mafao yake mpaka baada ya miaka 30, kweli anayefikiria hivyo ana akili au ni kichaa?