Nimeisoma sheria mpya hapo juu na kuona wapi mmesimama. Nadhani mnayo kesi maadam swala hili limepitishwa kinyemela...again kumbuka tu kwamba Ufisadi ndio unaendesha maisha ya watu nchini hivyo itakuwa kazi ngumu sana kushinda na hata kwenda mahakama za kimataifa sidhani kama watawaeleweni..
Hakuna sababu ya kukata tamaa mapema. Mara ya kwanza wafanyakazi walishinda. Na ni kutokana na maamuzi ya mahakama ndiyo maana mifuko hii ililazimika kuendesha schemes mbili kwa wakati mmoja. Sina uhakika ni kwa namna gani serikali imejilinda katika sheria hii mpya ili kuweza kushinda mahakamani.
Tatizo kubwa hapa siyo huu mpango bali ni dhamira chafu ya serikali na mifuko yenyewe iliyojificha nyuma ya mpango wenyewe. Kwa muda mrefu, serikali imekuwa na matumizi ya ovyo, wizi, ubadhirifu na ufisadi kiasi kwamba kila mara imekuwa haina fedha za kutekelezea miradi ya maendeleo. Mahali pekee ambapo wamekuwa na uhuru wa kuchota fedha kadiri wapendavyo ni kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Sasa imefikia mahali mpaka mifuko hii kuanza kuwa na hofu ya kushindwa kuwalipa wanachama wao wanapoacha kazi. Ili kukabiliana na hilo serikali imeleta hii sheria mpya ambayo ina maneno matamu lakini dhamira yake ni kuhakikisha wafanyakazi wengi hawapati mafao yao, maana inajulikana kuwa wanachama wengi hawana uhakika wa ajira.
Mathalani mtu ambaye amefanya kazi miaka 5, akachangia kiasi cha sh. milioni 10 kutokana na mshahara wake wa 450,000 kwa mwezi, akaachishwa kazi akiwa na umri wa miaka 30, atalazimika kukaa miaka 30 kabla ya kupata mafao yeyote ya mfuko, na itakpofika hiyo miaka 30, hii milioni 10 kwa wastani wa inflation ya 20%, itakuwa ni sawa sawa na sh. 100,000 ya sasa. Mwanachama huyu baada ya miaka 30 ule mshahara wake wa sh 450,000 kwa mwezi utakuwa ni sawa na sh. 45,000. Mafao yake kwa mwezi itakuwa ni 60% ya mshahara ule alioachia kuchangia. Hivyo atakachokipata itakuwa ni sawa na 60% ya sh. 45,000 ya leo ambao ni sh. 27,000 ya leo. Mwanachama huyu hata akibahatika kuishi miaka 10 zaidi atakachokipata ni sawa na sh. 27,000 x 12 x 10; ambayo ni sawa na TSH. 3,240,000 ya sasa. na hivyo NSSF/Serikali wana uhakika wa kupata karibu 7 milioni ya bure lakini ukweli ni kuwa ni wachache sana watafikia miaka hiyo ya 60 achilia mbali kuishi miaka 10 baada ya 60. Kwenye mpango huu kwa mazingira ya Tanzania, ni kuipora hela ya mwanachama.
Kwa kuujua ukweli huu ndiyo maana wanachama wengi hawataki ile scheme ya pension, na hivyo huamua kuchukua kiasi walichochangia na kwenda kuanza maisha yao mapya, maana hata ukisema uiache, hela hiyo haitaweza kukusaidia chochote siku za mbeleni maana itakuwa haina thamani. Hela ambayo leo mfanyakazi akiichukua angeweza kununua mabati 10 baada ya miaka 30 itaweza kununua mikate 20. Ni mtu mpumbavu pekee yake anayeweza kukubali hela yake ikae mahali kwa miaka zaidi ya kumi kwenye uchumi wenye inflation ya zaidi ya 20% halafu ukaamini kuwa nina akiba. Aheri uwekeze kwenye miradi uchwara ambayo itakuwa inakupa mapato madogo madogo lakini yanayoendana mfumko wa bei wa wakati huo.
Mimi mafao yangu ya kwanza yalikuwa sh. 20 milioni, kutokana na hela hiyo nilinunua eneo la ekari 7. Baada ya miaka 4 serikali ililichukua eneo hilo kwa kutangaza kuwa eneo hilo siyo la mashamba tena bali ni la makazi. Kwa fidia ya serikali nililipwa sh. 70 milioni, na nikaachiwa kiwanja kimoja ndani ya eneo hilo. Hivi ningeiacha hiyo 20 milioni mpaka leo, ingenisaidia nini? Mafao yangu ya pili nilipata kama millioni 50 hivi, pamoja na mambo mengine, nimeweza kupata shamba la ukubwa wa ekari 200. Hapa najua nimewekeza, na thamani ya hela yangu inazidi kukua kila siku kuliko mtu yeyote aliyefungia pesa yake NSSF. Mimi hela ya kwangu ina appreciate wakati yule aliyeiacha NSSF ina depreciste.
Jambo linaloudhi zaidi, wafanyakazi wa NSSF kuanzia mameneja wa matawi wamekuwa wakijikopesha mpaka milioni 300 (huku wachangiaji wakinyimwa)ili waweze kutetea sera za wizi wa mifuko hii mbele ya wachangiaji.