HLRC kuiburuza serikali mahakamani kuhusu NSSF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HLRC kuiburuza serikali mahakamani kuhusu NSSF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jul 23, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kimesema kinaandaa taratibu za kuiburuza serikali mahakamani kwani kumkatalia mwanachama kuchukua hela zake kwa vile hajafikisha miaka 60 ni ukiukwaji wa haki za binadamu.Hii ni kwa sababu hakuna makubaliano yaliyofanyika kati ya mifuko husika na wanachama ili kuleta sheria hii ambayo ni mbaya na haramu hasa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
  HLRC imeomba ushirikano wa wafanyakazi wote kufanikisha azma hii.

  Source:Habari BBC Jioni.

  My take:
  Sheria hii ya NSSF ni kitanzi kwa wafanyakazi kote nchini hasa wa sekta binafsi kutokana na ukweli kwamba makampuni mengi binafsi yamekuwa yakiwaachisha mara kwa mara wafanyakazi wake huku kukiwa hakuna utetezi wowote wa serikali.Ni vigumu sana wafanyakazi kuunga mkono sheria hii kutokana na ukweli kwamba mtu akiacha kazi akiwa na miaka 30 itampasa kusubiri miaka 25 ili apate mafao yake.Huo ni uendawazimu.
   
 2. S

  Sessy Senior Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ni habari njema kwa wafanyakazi tupo pamoja kwa kweli
   
 3. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Tupo pamoja hata ukamilifu wa dahari MUNGU akiwa upande wetu je, ni nani aliye juu yetu? Hakika mafisadi wanaotuibia fedha hizi kiduchu tulizochuma kwa kuleta visheria uchwara watashindwa, na vichwa vyao ni halali yetu kipindi kikifika naomba MUNGU anifikishe kipindi hicho.
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mnajua maana ya Social Security?
   
 5. m

  mbalapala Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Ni hatua nzuri tuungane kupambana na hili kundi la wala nchi.
   
 6. M

  Mwanamtwa Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tangazeni maandamano ya wafanyakazi nchi nzima mimi nitakuwa mstari wa mbele nabango kubwa 'huu ni wizi na uonezi mkubwa hata mungu hapendi'
   
 7. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  May you please tell what is not known......................

  As an intro.........vijana wa sasa we need to get the wheel turning before retirement mkuu......mambo ya kuja kupewa mihela wakati huna nguvu ni ya nini sasa????? Just a philosophical change
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tuko nyuma yenu bse kwa life expectancy ya tz miaka 60 ni issue kuigonga
  Kama mumefuja ela zetu kwa mambo yasiyo ya msingi imekula kwenu.
  Kuna ambaye anaweza tupa experience ya nchi zingine jamani maana Tz kwa vijambo tuko fiti
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nijuavyo mimi huwezi ku retire kazi ukataka kuchukua fedha yako NSSF unapopenda. Kuna mashatri ya Umri wako na miaka ulolitumikia..Kama mfanyakazi haja qualify ktk makundi haya tuseme unaaxcha kazi ukiwa na umri wa miaka 45 na hujalitumikia taifa kwa miaka inayotakiwa - Huwezi kuchukua hata kama ukienda mahakama gani. Muhimu sana tuelewe vifungu vya sheria za NSSF kabla hatujaunga mkono maana unapojaza makaratasi na kujiunga kuna vipengele ambavyo watu wengi sana huwa hawavisomi..
  Ebu pitieni site hii muone mfano.. Bofya
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  We should use Bunge platform before kimbilia mahakamani , a study lazima ifanyike na kujua nini kilifanyika kwenye Bunge la April 13 kama kifungu hicho kilikuwepo kwenye mswada ama kilichomekewa .......remember issue ya sheria ya gharama za uchaguzi na kifungu cha 10.

  hivi kwa wabunge itakuwaje wale ambao hawana 55 + watasubiria mafao yao? why walipitisha ? we need to do something in between kabla ya Court ......
   
 11. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,612
  Likes Received: 2,993
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi wajue maana ya Social Security au wasijue is irrelevant. Jambo la muhimu ni kuwa hela hiyo ni michango ya wafanyakazi. Namna gani itawasaidia, wao ndiyo wanaojua, na serikali haina haki yeyote kuifanya hela ya wafanyakazi kuwa mfuko wa kutekelezea miradi ya maendeleo. No way. Nadhani serikalini bado kuna watu ambao wapo kwenye usingizi mnono wa kukosa fikra, wakifanya kazi ya ku-copy mambo machache kutoka mataifa mengine bila ya kujifunza na kutambua mambo hayo yatafanya kazi vipi katika mazingira yao.

  Wewe katika nchi yako, watu wenye ajira rasmi hawafikii hata 10% halafu unasema mfanyakazi asipate mafao mpaka afikishe umri wa miaka 60, wewe una akili au tahira? Nchi ambayo mfumko wa bei ni zaidi ya 20% halafu umwambie mfanyakazi aliyeachishwa kazi akiwa na umri 30, halafu eti asubiri kwenda kuchukua mafao yake mpaka baada ya miaka 30, kweli anayefikiria hivyo ana akili au ni kichaa?
   
 12. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Najua kukuzidi hata wewe. Suala hapa unawaandaaje watu kuingia kwenye utaratibu mpya. Hivi wewe mkeo huwa unakurupuka tu na kuanza kumvua nguo bila hata kumwandaa. Acha ujinga, usitufanye sisi mbumbumbu
   
 13. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Social security funds si kwa ajili yako, ni kwa ajili ya serikali.... Once you have that in your head, utaona haya malalamiko hayana nguvu kimataifa.
   
 14. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  na hili la kuchukua mafao yetu aka akiba zetu uzeeni bila kututaarifu ni haki yao pia! makubaliano ni ya pande mbili so chochote wanachobadilisha lazima waweke meazani tuakubaliane si kubaka kila kitu.....hawa vilaza wanatuzoea ipo siku watatupangia hata mda wa kukaa na wake zetu...
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mpango huu ni wa kiuaji,A criminal law for poor people,NASI TUTASEMA HAPANA! INATOSHA,mkopeshane halafu mtunyime hela zetu! EE MUNGU USIWASAMEHE WATU HAWA WENYE HILA,Uwaangushe peupe ila watu wako washuhudie kwa macho yao!
   
 16. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  kivipi mkuu! mimi ni po private sector inakuwaje ya serikali?
   
 17. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,612
  Likes Received: 2,993
  Trophy Points: 280
  Mkandara, tupo Tanzania, siyo Marekani. Mara ya kwanza ilipopitisha sheria ya kufuta NPF na kuanzisha NSSF walipitishwa sheria hiyo ya kutokujitoa kwa mwananchama ambaye hajafikisha retirement age, wafanyakazi walienda serikali na walishinda. Hivyo kukawa na schemes mbili zilizokuwa zikienda sambamba, ile inayoruhusu kujitoa na ile ya pension. Safari hii tena wanataka wawajaribu wafanyakazi, nina hakika serikali kutokana na nia yake ovu, lazima itashindwa.
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Serikali awamu ya 4 imeleta vioja,imeleta urafiki kwenye pesa zetu...wakaanza kuchota na kutekeleza matakwa yao kisiasa kama udom,na kukopa za kulipa mishahara....leo wameshindwa kulipa wanataka kutupa wakati mgumu maishani....ajira tanzania itakuwa kama kifungo ,unawachangia mafisadi wachezee pesa zetu na sisi tunabakia masikini hadi kufa,sekta binafsi hakuna anaeweza kukaa kazini miaka 30 hata siku moja,watu wanakaa maxmum 10yrs wananza kufanya kazi zao binafsi,sio serikalini utakaa milele hapo kusubiri upewe mabati ya kustaafu,yaani nikiacha kazi leo nina 35yrs nisubiri hadi miaka 55? Wakati sijachangia miaka 20??
   
 19. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  We shetani suala hapa sio maandalizi. Soma topic, acha umajinuni.
   
 20. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja!!This time iwe serious tuachane na mambo ya kina Mgaya maana hawatusaidii chochote!!!!
  Pia hakuna sababu ya kuwa na vyama vya wafanyakazi,vinavyosaidia kuwakandamiza wafanyakazi!!!
   
Loading...