Hizo kazi maalum za Prof. Mark Mwandosya ni zipi?

Mnamo tarehe 22 ya Mwezi huu wa Tano, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alimwapisha mpinzani wake wa karibu katika mchakato wa kupata mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (C.C.M) mwaka 2005 Prof. Mark Mwandosya kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais kwa KAZI MAALUM.

Swali langu ni hapo kwenye red, hizo kazi maalum ni zipi? As political analyst ( Mchambuzi wa Masual ya Kisiasa) kuna swali moja tu ambalo bado linakosa jibu la uhakika.swali hilo ni hili hapa chini.

Kwanini Prof. Mwandosya?

Ikizingatiwa hayo yafuatayo

1. Afya ya Prof. Mwandosya bado haijaimarika. Na yeye alikiri kuwa kwa kusema " Afya Kwanza"
2.Prof. Mark Mwandosya alitoa upinzania mkali kwa Mr. President katika ule mchakato wa kupata mgombea wa Urais kupitia CCM mwaka 2005. Alishika nafasi ya tatu nyuma ya Dkt. Salim Mohamed Salim na Dkt. Kikwete.

WASEMAVYO WASHIKA DAU

Wapo miongoni mwa wataalamu wa masual ya siasa nchini wanaoamini kuwa Mark Mwandosya na Jakaya Kikwete ni maswahiba wakubwa, na ushiriki wa Prof. Mark katika ule mchakto wa 2015 ulikuwa ni mpango kazi " strategic move" kupunguza na kugawa kura ambazo zingeenda kwa Dkt. Salim Ahmed Salim, kwahiyo Prof. Mark alishiriki kwa kiwango kikubwa sana kurahisisha ushindi na uteule wa Dkt. Kikwete. Wapo wanaoamini Ushiriki wa Prof. Mark ni zaidi ya ule uliokuwa unaitwa mtandao.

Wapo wanoamini kuna kitu ndani ya hizo kazi maalum za Prof. Mark Mwandosya. Lakini hatuwezi kufanya hitimisho ambalo halijafanyiwa utafiti. Jambo muhimu ni kwanza kujua hizo Kazi Maalum ni Zipi?





" As Africans our last hope is Scientific Socialism"

The Late Comrade Siad Barre





swali zuri,kwani hadi sasahivi keshafanya shughuli gani za kiserikali?
 
Ili usizijue ndio maana zikaitwa kazi maalum
Kila shimo lina mchimbaji wake wewe kaa utulie
 
Zawadi za kisiasa tu, hakuna jipya hapo. Safari zote yeye, misiba yote yeye, huyo mwenye kazi maalum atafanya nini. Kugawana ulaji tu.
 
Habari wana jf, kutoka bungeni jioni hii.

Mh. Mkosamali amehoji juu ya kazi gani maalumu aliyonayo "waziri wa nchi,ofisi ya raisi kazi maalumu" profesa mark mwandosya.

Profesa alipopata nafasi ya kuchangia hoja alianza kwa kujibu hoja ya mkosamali kwa kusema "kazi niliyonayo ni maalumu".

Mkosamali alihoji suala hilo kwa kua haoni ulazima wa kua na wizara hiyo kwa kua pesa inayotumika kuendesha wizara ni nyingi na akashauri ifike wakati serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima.

Mwana jf, wewe unadhani hiyo kazi maalum ya mh.mwandosya ni ipi ambayo haiwezi kutekelezwa na wizara nyingine ama taasisi nyingine za serikali?
 
Hili suala la Mwandosya watu waliliona mapema sana tuseme ni roho ngumu tu ya Rais kufanya vile .
 
Hiyo ni wizara ya kuwalea na kuwalipia watu fadhira si ajabu hata kingunge anaimudu
 
Sio Kweli Kazi Maalum zinaweza Kuwaiti ht USA wapo mfano SPECIAL ENVOYS na ht UN wapo Ninyi Hamjui Anachofanya URAIS NI TAASISI Hivyo Rais Hawezi Fanya Kazi Zote lazima awe na MTU wa Kumsaidia Wakati mwingine Tusikosoe tu ILI tuonekane Tumesema au Wajuaji Saana TAIFA LA MANUNG'UNIKO
 
Kazi maalum ni ipi kama sio kujaza washauri wengi wasio na lolote la maana wakati kila kitu kinaenda shaghara bagala.

Walafi na wanakula kodi zetu ovyo kiasi kwamba hata mwenyewe mwandosya hajuwi job description yake yaani nikupeana tu kazi, bora wanagawana uchumi wetu.
 
Na bado, zitaendelea kuliwa mpaka mkome. Na mimi nasema wazile tu, tena nasema wale mpaka mishahara yenu, eeeh manake tumechoka sasa. Mliambiwa na nani muwachague. Hata mimi ningekuwepo kule ningekula tu. Eeeeeh manake dawa ya watu wasiojitambua ni kuliwa tu mpaka watakapojitambua.
 
Badala ya kujibu hoja ya Mkosamali kuhusu kazi maalum ya mh. Mwandosya yeye amemjibu Mkosamali kuwa amekufuru. Na kaongezea msemo kuwa hujafa hujaumbika. Je, hili ndo jibu alilopaswa kujibiwa na waziri huyu? Je kuuliza swali ni kukufuru?
 
Ukiwa CCM lazima uwe chizi, vinginevyo huwezi. Kwa majibu haya anamaanisha Mwandosya kapewa hiyo kama msaada ili angalau apate chochote maana ugonjwa umempunguzia uwezo. Je, serikali itabeba wangapi kwa staili hii?
 
Back
Top Bottom