Hizo kazi maalum za Prof. Mark Mwandosya ni zipi?

Badala ya kujibu hoja ya Mkosamali kuhusu kazi maalum ya mh. Mwandosya yeye amemjibu Mkosamali kuwa amekufuru. Na kaongezea msemo kuwa hujafa hujaumbika. Je, hili ndo jibu alilopaswa kujibiwa na waziri huyu? Je kuuliza swali ni kukufuru?

mwandosya kuwa hana wizara maalum kumbe ni kufa sijui ni kisiasa au ni kiafya au kajikwaa kuitetea nafasi hiyo ya uwaziri?
 
huyu mama namuona anazeeka vibaya. Badala ya kujibu hoja yeye kakazana'hujafa haujaumbika'. Ha hivi ndio jibu nalo?
 
jamani Baba Sekela alikuwa anaumwa sasa ndo anarecover mwacheni aanze na kazi nyepesi kwanza ,atapewa wizara tu.
Habari wana jf, kutoka bungeni jioni hii.

Mh. Mkosamali amehoji juu ya kazi gani maalumu aliyonayo "waziri wa nchi,ofisi ya raisi kazi maalumu" profesa mark mwandosya.

Profesa alipopata nafasi ya kuchangia hoja alianza kwa kujibu hoja ya mkosamali kwa kusema "kazi niliyonayo ni maalumu".

Mkosamali alihoji suala hilo kwa kua haoni ulazima wa kua na wizara hiyo kwa kua pesa inayotumika kuendesha wizara ni nyingi na akashauri ifike wakati serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima.

Mwana jf, wewe unadhani hiyo kazi maalum ya mh.mwandosya ni ipi ambayo haiwezi kutekelezwa na wizara nyingine ama taasisi nyingine za serikali?
 
Ukiona vyaelea ujue vimeubwa!taasisi ya uraisi lazima iwe na maofisa wanaosadia utendaji kazi,nadhani ili kupunguza gharama za kiutawala ni vyema ingeudwa taasisi ya uraisi na kazi zake ziwekwa wazi ili wanachi tufahamu
 
Mwandosia hana shida ya kubebwa. Angekaa pembeni akawa mtaalamuvmshauri atapata zaidi ya hizo fadhila anazodhalilishwa nazo mbele ya kadamnasi. Kombani hakujibu ila ameonyesha udhaifu mkubwa kuwa mwandosi kapewa huo uwazir kama fadhila/msaada.
 
Sio Kweli Kazi Maalum zinaweza Kuwaiti ht USA wapo mfano SPECIAL ENVOYS na ht UN wapo Ninyi Hamjui Anachofanya URAIS NI TAASISI Hivyo Rais Hawezi Fanya Kazi Zote lazima awe na MTU wa Kumsaidia Wakati mwingine Tusikosoe tu ILI tuonekane Tumesema au Wajuaji Saana TAIFA LA MANUNG'UNIKO
Nani kakwambia special envoy maana ni kazi maalumu..bila maelezo kama ya mwandisya..ww ndo unaleta ujuaji usiokuwa na mpango
 
Wewe unayejua Maana ya " Special" no nini Tatizo ni kujifanya Miungu Watu na Chuki tu wewe unalolijua lipi??? Ndio Maana ht Majina yenu GERESHA TUU ETI " SIAFU JIKE" Ukiwa na jina Fake ht mawazo yk Yatabaki Fake tuuu
 
FEBRUARY 2011

CUF yalia na CHADEMA

*Yashutumu kuwatenga katika Kambi Rasmi Bungeni

*Yadai CHADEMA na wabaya wao watakufa na kuiacha

Na Rabia Bakari - Majira

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuhujumiwa na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana 'kauli za kichochezi' zinazotolewa dhidi yake kuhusu sababu za kukataa kushirikiana nao bungeni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema kuwa licha ya kuhujumiwa na CHADEMA lakini pia wanasikitishwa na kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa kwa kudai kuwa CUF sio chama cha upinzani nchini.

"Tunasikitishwa na kauli hiyo ya Dkt. Slaa na nikimnukuu anasema kuwa 'CUF siyo chama cha upinzani Tanzania tena, eti kwa sababu kiko serikalini Zanzibar' na kwa hiyo CHADEMA hawawezi kushirikiana na CUF katika kuunda kambi ya pamoja bungeni.

"CHADEMA wanaishambulia sana CUF hivi sasa, wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kitendo cha CUF kuwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni dhambi kubwa mno na kuwa Watanzania wasiiunge mkono CUF Tanzania bara, jambo ambalo ni ndoto za alinacha na kamwe halitatokea kwani Watanzania wa sasa hawadanganywi kwa propaganda zisizo na maana,"aliongeza.

Kauli ya Bw. Mtatiro inatokana na Tamko la Kamati kuu ya CHADEMA lililotolewa na Dkt. Slaa, kuwa CC ya chama hicho imemuagiza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli kwa kuhusisha wabunge wa CHADEMA pekee.

Akitoa tamko hilo, Dkt. Slaa alisema: "Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, kamati kuu imezingatia kuwa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na CCM kuunda Serikali ya Umoja Wa kitaifa.

"Na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za muungano na kwa kuwa vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge vimo katika ushirikiano na CUF, Kamati Kuu imeona kuwa CHADEMA haiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo.

"Sasa kwa mfano tukiazimia kitu kinachopingana na serikali, Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye Makamu wa kwanza wa Rais huko Zanzibar unategemea atakubaliana nacho ili apingane na serikali, hivi vyama vingine navyo tayari vimeshakuwa sehemu ya watawala maana wameamua kushirikiana na CUF katika kamati yao," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumzia maazimio hayo, Bw. Mtatiro alisema kuwa CUF haiwezi kuwalamba miguu viongozi wa CHADEMA kwani hakuna faida yoyote wala umuhimu ambao wao wameonesha tangu walipojaribu kila namna kuwafanya wafanye kazi kwa umoja na vyama vingine na kugonga ukuta.

"Mara zote CHADEMA wamekuwa na historia ya kuvisaliti vyama vingine vya upinzani huku wakikimbilia kwa umma kuomba waungwe mkono wao peke yao," alidai.

Aliongeza kuwa CHADEMA kina matatizo mengi sana tangu mwaka 2007, na waliwavumilia kwa kiasi kikubwa na hata baada ya uchaguzi mkuu kuisha mwaka jana, CUF iliiomba CHADEMA iweze kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuwa na kambi ya upinzani imara zaidi na yenye nguvu.

"CHADEMA walikataa kabisa suala hili kwa maelezo kuwa “wao wako tayari kuungana na CUF tu katika kambi ya upinzani na kuwa hawaviamini vyama vya NCCR, TLP na UDP, na tulijaribu kuwasihi lakini hawakutaka kubadili msimamo huo.

"Lakini baada ya yote hayo, jana (juzi) CHADEMA wametoa kauli ya kinafiki,- eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza dola, yaani CUF na kuwa wao CHADEMA wako tayari kushirikiana na NCCR-Mageuzi," aliongeza.

Bw. Mtatiro alisema kuwa hivi karibuni NCCR ndio walikuwa kikwazo kwa CHADEMA kushirikiana na vyama vingine, hata mwezi haujapita wamegeuka na kudai CUF ndiyo adui.

"CHADEMA ni chama popo sana, hawajui wanachofanya, wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20 Tanganyika, sasa hawana haja na CUF na vyama vingine, wanadhani majimbo 20 ndio Ukombozi wa Tanzania umemalizika.

“Ni sawasawa na maskini sana anayeamka ghafla anajikuta tajiri, hajui namna gani atatumia utajiri wake, anaanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umaskini wao, anawatukana majirani huku anaendelea kuponda mali na wasichana warembo katika kijiji hichohicho, siku moja mali zinaisha……hadithi ya tajiri mjinga inaishia hapo," aliongeza Bw. Mtatiro kwa jazba.

Aliendelea kukishutumu chama hicho kuwa kinafanya kusudi kutoa kauli za kichochezi, wakiamini kuwa CUF ikifa bara wao watapumua mno.

Alisema ni wazi CHADEMA wanaiogopa CUF, huku wakifahamu fika kuwa chama hicho kina mtandao mkubwa na kina mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi.

Bw. Mtatiro alidai kuwa kitendo cha CHADEMA kuwadharau Wazanzibari, kudharau maamuzi ya wananchi wa Zanzibar katika nchi yao, kudharau katiba ya Zanzibar ni kitendo cha kijinga mno.

"Wazanzibar ndio walioamua kwa kupiga kura kuwa wanahitaji serikali yao, ya umoja wa kitaifa kwa maslahi ya nchi yao ya Zanzibar kwa kujali amani maendeleo na ustawi wa taifa lao.

"Wazanzibari ndio walioamua kuwa chama kitakachoongoza katika uchaguzi kitatoa rais na mawaziri na cha pili kitatoa pia makamu wa kwanza wa rais na mawaziri. Wakapiga kura, wakatoa maamuzi haya, wakayaingiza katika katiba yao ya Zanzibar katika mabadiliko ya 10 ya katiba," aliongeza.

Alisema ni ujinga kudai CUF kuwa katika mfumo wa serikali iliyoamuliwa na wananchi katika upande mmoja wa nchi ni dhambi.
--
Alihoji kuwa, CUF ilipopata nafasi ya pili Zanzibar CHADEMA walitaka ikiuke matakwa ya wananchi na kukataa kuingia serikalini ili iwafurahishe CHADEMA ambao Zanzibar hawana hata mjumbe wa mtaa wala tawi?

"Nani asiyejua kuwa CUF ni chama chenye nguvu na mtandao Zanzibar na Tanganyika na ni chama cha pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande zote za muungano? Nani asiyejua kuwa CHADEMA ni chama kilichoko Tanganyika peke yake?

"Nani asiyejua kuwa CHADEMA kinaumizwa sana na mafanikio na utulivu wa kisiasa Zanzibar yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na busara na viongozi wa CUF ambao hawakuweka maslahi ya chama mbele katika kulinda uhai na maisha ya Wazanzibar?" alihoji.

Bw. Mtatiro aliyewania ubunge katika Jimbo la Ubungo na kushindwa na Bw. John Mnyika wa CHADEMA, alidai kuwa CUF kama chama chenye nguvu kubwa Zanzibar watazidi kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi kila mara bila kujali kama CHADEMA watakasirika au la.

Aliongeza kuwa chama kipi ili kuwatumikia Watanzania, kuwatetea katika madhila yote na manyanyaso wanayofanyiwa.

"Tutaendelea kuwa katika SUK na kulinda maamuzi na matakwa ya wananchi wa Zanzibar lakini kwa upande wa Tanzania bara ambako katiba iko wazi, kuna chama kimoja kinachoongoza dola na vingine vyote vikiwa vyama vya upinzani, tutaendelea kuheshimu matakwa ya kikatiba yaliyopo Tanzania bara," alisema.

Aliwataka CHADEMA wafahamu kuwa CUF kitazidi kuwa chama cha kitaifa kwa kuzidi kupata wabunge wengi kutoka Bara na Zanzibar, kujiimarisha pande zote za nchi hadi waione njema inayosubiriwa na Watanzania wote.

Bw. Mtatiro aliongeza: "CHADEMA na watu wote wanaoitakia mabaya CUF watakufa na kukiacha chama hiki kikishamiri kama tegemeo la pekee la Watanzania," alisema.
 
Sio Kweli Kazi Maalum zinaweza Kuwaiti ht USA wapo mfano SPECIAL ENVOYS na ht UN wapo Ninyi Hamjui Anachofanya URAIS NI TAASISI Hivyo Rais Hawezi Fanya Kazi Zote lazima awe na MTU wa Kumsaidia Wakati mwingine Tusikosoe tu ILI tuonekane Tumesema au Wajuaji Saana TAIFA LA MANUNG'UNIKO
special envoy ni mawaziri?
 
Usiangalie Cheo Angalia "Dhana" Kuwa "KAZI MAALUM" Jukumu NHYABINGI!, mmeambiwa mpk Mnalalamika Kuwa Ana Staffs wangapi??? Na Bajeti??? Pengine Anatumia Resources Hizo Hizo za Staffs wa Ikulu??? Yeye ni Kama yeye Anatumwa KAMA JUZI ALIPOMWAKILISHA RAIS RWANDA KWENYE GENOCIDE??? tuache Assumptions Za JF
 
Back
Top Bottom