Hizo kazi maalum za prof. Mark mwandosya ni zipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizo kazi maalum za prof. Mark mwandosya ni zipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijana Msomali, May 24, 2012.

 1. K

  Kijana Msomali Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mnamo tarehe 22 ya Mwezi huu wa Tano, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alimwapisha mpinzani wake wa karibu katika mchakato wa kupata mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (C.C.M) mwaka 2005 Prof. Mark Mwandosya kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais kwa KAZI MAALUM.

  Swali langu ni hapo kwenye red, hizo kazi maalum ni zipi? As political analyst ( Mchambuzi wa Masual ya Kisiasa) kuna swali moja tu ambalo bado linakosa jibu la uhakika.swali hilo ni hili hapa chini.

  Kwanini Prof. Mwandosya?

  Ikizingatiwa hayo yafuatayo

  1. Afya ya Prof. Mwandosya bado haijaimarika. Na yeye alikiri kuwa kwa kusema " Afya Kwanza"
  2.Prof. Mark Mwandosya alitoa upinzania mkali kwa Mr. President katika ule mchakato wa kupata mgombea wa Urais kupitia CCM mwaka 2005. Alishika nafasi ya tatu nyuma ya Dkt. Salim Mohamed Salim na Dkt. Kikwete.

  WASEMAVYO WASHIKA DAU

  Wapo miongoni mwa wataalamu wa masual ya siasa nchini wanaoamini kuwa Mark Mwandosya na Jakaya Kikwete ni maswahiba wakubwa, na ushiriki wa Prof. Mark katika ule mchakto wa 2015 ulikuwa ni mpango kazi " strategic move" kupunguza na kugawa kura ambazo zingeenda kwa Dkt. Salim Ahmed Salim, kwahiyo Prof. Mark alishiriki kwa kiwango kikubwa sana kurahisisha ushindi na uteule wa Dkt. Kikwete. Wapo wanaoamini Ushiriki wa Prof. Mark ni zaidi ya ule uliokuwa unaitwa mtandao.

  Wapo wanoamini kuna kitu ndani ya hizo kazi maalum za Prof. Mark Mwandosya. Lakini hatuwezi kufanya hitimisho ambalo halijafanyiwa utafiti. Jambo muhimu ni kwanza kujua hizo Kazi Maalum ni Zipi?

  " As Africans our last hope is Scientific Socialism"

  The Late Comrade Siad Barre

   
 2. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  1.Kutembelea hospitali kuwaona wagonjwa kwa niaba ya rais.
  2.Kuonja chakula cha Rais
  3.N.k
   
 3. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ndo mana zikaitwa kazi maalum!we utazijuaje?
   
 4. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  4. kupokea Posho
  5. Mdororo wa uchumi usimuwe mapema ...
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nadhani Ikulu wakiiona hii watatoa tamko faster!
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kazi zipo nyingi tu, Unajua mwandosya ni Profesa , nchi inahitaji sana mchango wake, hivyo naamini rais ameona mbali kama kawaida yake.
   
 7. a

  allydou JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,484
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  sijaona point ya msingi bado. angeachwa mngesema JK amepata nafasi ya kumuacha mpinzani wake. mi nafikiri mtu anapoanzisha mada awe na detailed informations jamani, tusiumizane vicha bila sababu.
  SIO LAZIMA KILA MTU AANZISHE MADA, WENGINE TUNAWEZA KUWA WASOMAJI TU WA MADA. huu ni wangu mtazamo tu, washkaji msikasirike.
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huu ni ufujaji wa pesa zetu bure, huwezi kumchangua MGONJWA ambaye wataalamu (madaktari) wameshauri anahitaji mda mrefu wa kumpumzika kuwa waziri.

  There is no any excuse kwa uteuzi Prof. Kama alishindwa kumtumia wakati akiwa mzima wa AFYA atawezaje kumtumia sasa hivi wakati Prof ni MGONJWA?

  Tukomeshe haya katika KATIBA mpya. Katiba mpya iseme wazi kama USA kwamba tutakuwa na wizara kwa MAJINA na IDADI. Hakutakuwa na wizara isiyo maalumu, ili kukomesha kugawawiana vyeo kwa huruma.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  the citizen la leo wamesema why kikwete retained mwandosya????
   
 10. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Kwa kuwa Prof Mwandosya bado afya yake haijarudi katika hali yake ya awali, na bila shaka atarudi katika hali yake soon panapo majaliwa...

  ...Na kwa kuwa kwa sababu ya changamoto anayoipitia sasa haitakuwa vyema kwa sasa kumpa pilikapilika za kila siku za wizara moja kwa moja...

  ...Lakini kwa kuwa maamuzi ya mambo yote ya msingi ya nchi katika wizara zote yanafanywa na Baraza la Mawaziri...

  ...Na kwa kuwa mawazo na fikra za Prof Mwandosya bado zinahitaji sana katika ufikiaji wa maamuzi hayo muhimu yanayofanywa na Baraza la Mawaziri....

  ....Na kwa kuwa ili Prof Mwandosya aweze kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri ni lazima awe Waziri...

  ....Hivyo, kumpa Uwaziri wa Wizara Maalumu likawa ndilo chaguo bora zaidi....
   
 11. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Afe akiwa na title ya waziri.
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  So the citizen washatoa jibu
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ndo kazi maalum hiyo???
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Bahati mbaya sana unaweza ukatangulia wewe kabla yake, shame...
   
 15. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kazi maalum!!
  Yakula nae pesa za walala hoi
   
 16. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hujui kazi maalumu waliyonayo ccm na serikali yake kwa kifupi ccm ni chama cha matanuzi,hivyo kazi maalum ni kutanua pamoja,usijisumbue kuuliza siku ingine sawa
   
 17. K

  Kijana Msomali Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ni vibaya kumuombea binaadamu mwenzako kifo remember what goes around comes around...take care
   
 18. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Anaijua jk, kamuulize
   
 19. Wild fauna

  Wild fauna JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 427
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  He's like a watch dog,he cut across all ministries and look wht's going on.
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Cha muhimu kwa sasa ni afya yake itengemae. Sijui kazi maalumu ndio nini ila Ikulu kuna kazi nyingi hata kusoma makaratasi yanayoletwa kutoka kila kona inaweza ikawa kazi maalumu pia.
   
Loading...