Hizo kazi maalum za Prof. Mark Mwandosya ni zipi?

Habari wana jf, kutoka bungeni jioni hii.

Mh. Mkosamali amehoji juu ya kazi gani maalumu aliyonayo "waziri wa nchi,ofisi ya raisi kazi maalumu" profesa mark mwandosya.

Profesa alipopata nafasi ya kuchangia hoja alianza kwa kujibu hoja ya mkosamali kwa kusema "kazi niliyonayo ni maalumu".

Mkosamali alihoji suala hilo kwa kua haoni ulazima wa kua na wizara hiyo kwa kua pesa inayotumika kuendesha wizara ni nyingi na akashauri ifike wakati serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima.

Mwana jf, wewe unadhani hiyo kazi maalum ya mh.mwandosya ni ipi ambayo haiwezi kutekelezwa na wizara nyingine ama taasisi nyingine za serikali?

Kinachogomba ni double standard ya kusimamia Kanuni NA Taratibu, hapo mtoa Hoja ndiyo ili bidi asimamie NA Hakukuwa NA kukufuru KITU, sisi Wote tuna mwisho haba duniani
 
Anaweza ku exercuse hizo ministerial power zake akiwa nje ya Baraza la mawaziri au angempeleka wizara soft kama Habari, Kazi na ajira au wanawake na watoto kuliko kumrundika kwenye kabinet kuongeza gharama unnecessarily
Una mawazo ya chekechea.
Jipe muda wa ku google ili ujiridhishe kama kuna political appointees duniani ambaowana ministerialowers halafu so cabinet members.
Au kwa ufupi jiridhishe kwa ufahamu kazi za waziri ni zipi.
 
Madhara ya Katiba mbovu inayompatia fursa rais kuteua mtu yeyote na idadi yoyote ya mawaziri wakati mwingine kadri anavyoshauriwa au kadri ya maslahi na matakwa ya mke wake au hata watoto wake.
No wonder wanaCCM wanataka tutunge Katiba nyingine mpya MBOVU ili waendelee kufanya u.puuzi walouzoea!!!!
 
Profesa na taaluma yake anakubari kudharirishwa kwa kupewa kazi maalum!!?

Mkuu hapo umenena. Hili ndilo jambo ambalo huwa nashindwa kuelewa. Afadhali kurudi darasani kuendelea na fani kuliko kulewa siasa na majina ya vyeo. Nadhani with time haya mambo yatabadilika tu. Ona kina Condoleeza Rice, wamerudi kufundisha baada ya muda wa kupiga siasa.
 
Wizara ya nishati na madini ivunjwe mara mbili, upande wa nishati apewe mwandosya badala ya kuwa na wizara kubwa yenye manaibu wawili. Utaalam wa mwandosya kwenye masuala ya nishati --------- east and southern africa, world bank pia wanamtumia sana, journal kubwa kuliko zote duniani juu ya masuala ya nishati "energy policy", mwandosya ni mdau mkubwa sana, kyoto protocol, anatambulika, kwanini tusimtumie nchini kwa upuuzi tu wa kisiasa?

He made millions of dollars 1994 - 2005 kutokana na elimu, uwezo na uzoefu wake katika masuala ya nishati. Hana haja ya siasa kupata chakula, siasa kwake ni wito tu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hata Kawawa alishawahi pewa hiyo kazi maalum kwa kipindi kirefu sana... na kingunge pia nadhani... ukishaingia kwenye system si lahisi kuachiwa... ni aina tu ya system kama zuwa Jambazi huwezi acha kirahisi tu
 
Hapa tatizo si JK bali ni Katiba mbovu jumlisha watanzania wengi wanaopenda bora liende!
 
Huyu mh ametangaza nia ya kugombea Urais! Muda mwingi yuko ofisi ya Rais,waziri asiyekua na wizara maalum mwenye kazi maalum.
Kwanini tusiamini kwamba huyu mh tayari alikua anaandaliwa kurithi ofisi hiyo? Tunafaham mpaka sasa anaifahamu vizuri ofisi hiyo!Huyu mzee anakubalika sana katika jamii kwa kutoa ushauri, Ni mtu wa watu, hana hata chembe ya kashfa ya aina yeyote ndani ya utumishi wake wote japo naye sio Malaika.
Naikumbuka sana ile siku mheshimiwa huyu alipoingia bungeni baada ya kutoka kwenye matibabu India jinsi ambavyo Ukumbi wa bunge ulirindima!
Nakumbuka jinsi alivyoguswa na lile sakata la ESCROW na kusimama kutoa msimamo wake jinsi alivyochukizwa na suala hilo.
Ila wasi wasi wangu ni kufanya maamuzi magumu kwa masuala mbali mbali na makubwa yahusuyo taifa! Ni mpole sana.
 
Huyo Mwa.... Aliwekwa backbench ndo maana alipewa wizara isiyo na ofisi
 
Mi sijawahi kuzielewa kazi za wizara hyo ya prof M Mwandosya. Nadhani ni athali ya katiba mbovu inayompa Rais madalaka makubwa yasiyo na tija kwa taifa letu.
 
Cha muhimu kwa sasa ni afya yake itengemae. Sijui kazi maalumu ndio nini ila Ikulu kuna kazi nyingi hata kusoma makaratasi yanayoletwa kutoka kila kona inaweza ikawa kazi maalumu pia.
Mwenye koneksheni tafadhali...

Hii kazi ya kusoma makaratasi sio ngumu, ila ngoja nikajinoe kwa Ras Simba kwanza
 
Back
Top Bottom