Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,743
Juzi hapa ilitangazwa kwamba Prof. Mwandosya ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa EWURA. Wengi walishangaa kwa nini Prof. Mwandosya kaletwa kutoka hali ambayo wengi wetu tulidhani ni ustaafu na kurudi kuwa Mwenyekiti wa EWURA.

Lakini hatupaswi kushangaa. Uteuzi wa Prof. umetukumbusha pia kwamba wakati Mkapa akikabiliwa na sakata la ununuzi wa rada toka Uingereza, ni Prof. Mwandosya alipewa jukumu la kuliweka sawa jambo hilo, hadi kukawa na joke kwamba Prof. Mwandosya alim-charm yule mwanamke wa Uingereza aliyekuwa akitutuhumu vikali hadi akabadilika na kusema "it wa a very wise decision by Tanzania to buy the radar!"

Na pia kwa mlio na ufahamu, wakati uhusiano kati ya Kiwete na Kagame umeharibika sana hadi Kagame kutishia kumpiga Kikwete ni Prof. Mwandosya alitumwa Rwanda kwenda kuweka mambo sawa.

Na labda niwaambie siri nyingine, wakati Kikwete anaona anashambuliwa kila kona kwa kuwa raisi dhaifu, ni Prof. Mwandosya aliitwa ofisi ya Raisi kama waziri asie na wizara maalum na kuwa mshauri wa karibu wa Kikwete. Matokeo tukayaona, ghafla Kikwete akaanza kuonekana kuwa na busara sana nchini na nje ya nchi. Ilifikia hatua watu wakasema unajua Kikwete aliwahi kugombea uraisi angegombea awamu ijayo maana busara zimekuja mwishini mwa awamu yake, bila kutambua kuwa kulikuwa na busara za Prof. Mwandosya nyuma ya utendaji wa Kikwete katika sehemu kubwa ya awamu ya mwisho ya uraisi wake.

Na hivi, ni Watanzania wangapi wanatambua kuwa dira ya maendeleo aliyotumia Raisi Mkapa kutukwamua kiuchumi (TANZANIA DEVELOPMENT VISION 2025) ni matokeo ya kazi ya Prof. Mwandosya baada ya kuambiwa na Raisi Mkapa asimamie utayarishaji wake? Najua wengi hawakujua hili kwa sababu ilipokamilika iliandikwa imeandaliwa chini ya Planning Commission, bila kueleza iliandaliwa chini ya usimamizi wa Prof. Mwandosya

Na tunaomfahamu Prof. Mwandosya, tunajua kwamba katika nyanja za kimataifa, alikuwa kinara wa majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi ulioitwa Kyoto Protocol, kiasi kwamba alisifiwa sana juu ya uwezo wake wa kuchambua mambo na Raisi Clinton wa Marekani, pamoja na Al Gore. Wakati huo Prof. Mwandosya alikuwa msemaji wa kundi la G77 & China, lakini hakuwa na madaraka yoyote serikalini Tanzania, jambo ambalo lilimfanya Raisi Clinton wa Marekani amshangae sana Mkapa kutomtumia ipasayo Prof. Mwandosya katika serikali yake - na ndipo Prof Mwandosya "alipoamriwa" na Mkapa akagombee ubunge.

Ndio maana imesemwa kwamba katika mambo ambayo hutakaa umdanganye Prof. Mwandosya ni mambo ya mikataba. Hapo kina Prof. Kabudi na degree za sheria zao weka kando kabisa!

Na wakati fulani Prof. Mwandosya akiwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, kulikuwa na mbinu za nchi ya Misri kubadilisha makubaliano ya matumizi ya mto Nile ili kuinufaisha zaidi Misri. Ilibaki kidogo sana nchi za Mto Nile kutia sahihi mkataba huo mpya pale ambapo Prof. Mwandosya aliibuka tena na kuziamsha nchi nyingine juu ya vipengele kwenye makubaliano hayo mapya ambavyo vingezikandamiza. Kwa sababu ya uchambuzi wake huo, nchi zote za Mto Nile ziliwagomea Misri kuweka sahihi makubaliano hayo mapya. Hadi leo Misri hawataki kabisa kusikia habari za Prof. Mwandosya kwa kuwa wanamuona kuwa mtu aliewanyang'anya tonge mdomoni!

Na labda pia wengi waligundua kwamba mara tu baada ya Prof. Mwandosya kuteuliwa kuwa Mweyekiti wa EWURA, bei ya mafuta ilishuka kiasi tofauti na matarajio ya wengi, na wengi wamekuwa wakijiuliza kama ilikuwa ni utendaji wake kama Mwenyekiti wa EWURA uliosababisha kutoa ahueni kwenye bei za mafuta nchini.

Sasa kuna mengi juu ya Prof. Mwandosya naweza kusema hapa, lakini acha haya yatoshe kwa sasa ili kuweka backdrop ya swali langu. Kwa nini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi?

Swali langu pia linaendana na maoni ndani ya humu JF juu ya uteuzi wa Dr. Mpango kama Makamu wa Raisi. Kwa ujumla wengi wa wana JF hawaridhishwi kabisa na Dr. Mpango kuwa Makamu wa Raisi, hasa ukizingatia matukio ya hivi karibuni yaliyomhusu Dr. Mpango.

Sasa je, Kikwete hakukumbuka kwamba angalau Makamu wa Raisi wa Samia awe mmojawapo wa wagombea wa uraisi wa awamu ya Magufuli? Maana kama Prof. Mwandosya angekuwa Raisi badala ya Magufuli, hadi leo hii angekuwa ni raisi katika awamu yake ya mwisho. Je, inawezekana pia Kikwete hakumpendekeza Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi kutokana na ile issue ya "majina ya mfukoni"?

Kwa tunaomfahamu Prof. Mwandosya, ukiachia mbali porojo za humu JF, kama angekuwa ndio Makamu wa Raisi chini ya Raisi Samia, Tanzania tungeenda mbali sana na uongozi wa Raisi Samia ungeonekana ni bora na ungemfanya maarufu kwa scale ile ya Nyerere - mama wa Taifa! Na naweza kudiriki kusema inawezekana kabisa, Kikwete alitambua wazi kama Prof. Mwandosya angekuwa Makamu wa Raisi wa Samia, basi Kikwete angekuwa na influence kidogo sana kwa Samia, au asingekuwa na influence yeyote!

Kwa hiyo naweza kusema kwamba katika hili ni wazi ubinafsi ulizidi maslahi ya nchi. Raisi Samia alipigwa chenga katika kuteua Makamu wa Raisi. Prof. Mwandosya angemfaa sana na tusingekuwa na habari za kulishwa samaki waliooshwa kwenye maji ya maiti!

Samia anapaswa kuelewa kwamba Watanzania tunakesha tukimwombea uzima na afya tele, na sio tu kwa sababu tunampenda kama Raisi wa Tanzania.
 
Kwa hiyo mleta mada, unataka kutuambia mambo haya ya kufikirika.

1. Kikwete alimshauri Samia kuhusu Philip Mpango awe makamu wake wa Rais. Umejuaje?

2. Kikwete hakumshauri Samia kuhusu Professor Mwandosya kuwa makamu wake wa Rais. Umejuaje?

3. Kikwete huwa yuko busy kumshauri Samia kuhusu nani ashike nyazifa nyeti za serikali yake. Umejuaje?

4. Kitu chochote Kikwete anachomshauri Samia, ni lazima Samia afuate. Umejuaje?

Msingi wa hoja yako uko kwenye dhana ya kusadikika (assumption)
 
Kwa hiyo mleta mada, unataka kutuambia mambo haya ya kufirika.

1. Kikwete alimshauri Samia kuhusu Philip Mpango awe makamu wake wa Rais. Umejuaje?

2. Kikwete hakumshauri Samia kuhusu Professor Mwandosya kuwa makamu wake wa Rais. Umejuaje?

3. Kikwete huwa yuko busy kumshauri Samia kuhusu nani ashike nyazifa nyeti za serikali yake. Umejuaje?

4. Kitu chochote Kikwete anachomshauri Samia, ni lazima Samia afuate. Umejuaje?

Msingi wa hoja yako iko kwenye dhana ya kusadikika (assumption)
Mkuu, wewe umesema hayo, sio mimi. Mimi nilichofanya ni kuuliza kwa nini Kikwete hakumshauri,kwa sababu najua Samia huwa kuna wakati anapata ushauri wa Kikwete, toka zamani akiwa na Magufuli. Sasa huko ulikoenda wewe ni kwingine kabisa. Kama Kikwete alitoa ushauri huo Samia akakataa basi sema
 
Mwandosya alikuwa na proffessional arrogance Akiwa katibu mkuu wizara ya Nishati na Madini wakati Kikwete akiwa Waziri!! Wake!!! Boss wake

Alikuwa hamheshimu Kikwete kivileee!! Kifupi alikuwa akimdharau ndio sasa Kikwete akaja kuwa Raisi wakamwacha na Proffessional arrogance yake abaki nayo kijijini kwake aitumie kijijini sio mjini kwa watoto wa mjini akina Kikwete
 
Mwandosya alikuwa na proffessional arrogance Akiwa katibu mkuu wizara ya Nishati na Madini wakati Kikwete akiwa Waziri!! Wake
Alikuwa hamheshimu Kikwete kivileee!! Kifupi alikuwa akimdharau ndio sasa Kikwete akaja kuwa Raisi wakamwacha na Proffessional arrogance yake abaki nayo kijijini kwake nitumie kijijini sio mjini kwa watoto wa mjini akina Kikwete
Acha kupotosha na ushabiki. Prof. Mwandosya hakuwahi kutemwa na Kikwete kwenye baraza la mawaziri na kurudi kijijini. In fact, hata alipoumwa karibu miezi sita Kikwete alisema nafasi yake ya uwaziri itamsubiri.

Licha ya hiyo, yale yalikuwa mambo ya ujana. Kumbuka KIkwete alimfanya Prof. Mwandosya kuwa mtu wake wa karibu sana katika uraisi wake. Na kwa taarifa yako, KIkwete alimuomba Mwandosya wasahau yaliyopita, na hata alikuwa tayari kusuluhishwa na kina Malechela, Mwambulukutu ikibidi. Prof. Mwandosya alijibu kuwa hakuona jambo la kusuluhisha na yeye alikuwa fresh kabisa na Kikwete na wakasahau yaliyopita.

In any case, Prof. Mwandosya alichokuwa akilalamika wakati wakiwa Nishati pamoja ni Kiwete kuingilia kazi za Katibu Mkuu. Lakini kama una habari za ndani utakumbuka kwamba climax ya yote ilikuwa ni Prof. Mwandosya kuamrisha meli iliyoleta mafuta machafu ya TIPER iondoke nchini ndani ya masaa 24, kitu ambacho Kikwete alipinga akidai wasamehewe. Na ilikuja kujulikana Kikwete alikuwa akisimamia maslahi ya nani pale Nishati. Sasa Prof. Mwandosya hakuwa arrogant, alitaka kuwa professional tofauti na waziri wake ambae wakati huo professionalism was a foreign word too difficult to understand its meaning.

Na by the way, ili Prof. Mwandosya akuheshimu inabidi ustahili heshima yake, hilo kwake ni la msingi sana. Na nitakuambia wazi, Prof. Mwandosya hakuona kama Magufuli alistahili heshima yake. Kikwete alikuja kutambua Prof. Mwandosya alisimamia wapi
 
Yale yalikuwa mambo ya ujana. Kumbuka KIkwete alimfanya kuwa mtu wake wa karibu sana katika uraisi wake.

In any case, Prof. Mwandosya alichokuwa akilalamika wakati wakiwa Nishati pamoja ni Kiwete kuingilia kazi za Katibu Mkuu. Lakini kama una habari za ndani utakumbuka kwamba climax ya yote ilikuwa ni Prof. Mwandosya kuamrisha meli iliyoleta mafuta machafu ya TIPER iondoke nchini ndani ya masaa 24, kitu ambacho Kikwete alipinga akidai wasamehewe. Na ilikuja kujulikana Kikwete alikuwa akisimamia maslahi ya nani pale Nishati. Sasa Prof. Mwandosya hakuwa arrogant, alitaka kuwa professional tofauti na waziri wake.
Nashukuru walau umekubali kuwa Mwandosya alikuwa akipigana ubavu na Waziri wake Kikwete kuonyeshana misuli yaani tag of war kuwa nani zaidi wizarani kati ya katibu mkuu Mwandosya na Waziri wake Kikwete!!! Anyway kwenye hiyo vita baadaye Kikwete aliibuka kuwa Raisi!!! Sasa hapo nani zaidi katiya Mwandosya Proffessional katibu mkuu na Raisi waliyekuwa kwenye tag of war?
 
Acha kupotosha na ushabiki. Prof. Mwandosya hakuwahi kutemwa na Kikwete kwenye baraza la mawaziri na kurudi kijijini. Infact, hata alipoumwa mwezi sita Kikwete alisema nafasi yake ya uwaziri itamsubiri.

Licha ya hiyo, yale yalikuwa mambo ya ujana. Kumbuka KIkwete alimfanya Prof. Mwandosya kuwa mtu wake wa karibu sana katika uraisi wake. Na kwa taarifa yako, KIkwete alimuomba Mwandosya wasahau yaliyopita, na hata alikuwa tayari kusuluhishwa na kina Malechela, Mwambulukutu ikibidi. Prof. Mwandosya alijibu kuwa haukuna la kusuluhisha yeye alikuwa fresh kabisa na Kikwete na wakasahau yaliyopita.

In any case, Prof. Mwandosya alichokuwa akilalamika wakati wakiwa Nishati pamoja ni Kiwete kuingilia kazi za Katibu Mkuu. Lakini kama una habari za ndani utakumbuka kwamba climax ya yote ilikuwa ni Prof. Mwandosya kuamrisha meli iliyoleta mafuta machafu ya TIPER iondoke nchini ndani ya masaa 24, kitu ambacho Kikwete alipinga akidai wasamehewe. Na ilikuja kujulikana Kikwete alikuwa akisimamia maslahi ya nani pale Nishati. Sasa Prof. Mwandosya hakuwa arrogant, alitaka kuwa professional tofauti na waziri wake. Kikwete alikuja kutambua Prof. Mwandosya alisimamia wapi
Seems unamjua sana huyu mtu.

Nimejifunza jambo leo.
 
Nashukuru walau umekubali kuwa Mwandosya alikuwa alipigana ubavu na Waziri wake Kikwete kuonyeshana misuli yaani tag of war kuwa nani zaidi wizarani kati ya katibu mkuu Mwandosya na Waziri wake Kikwete!!! Anyway kwenye hiyo vita baadaye Kikwete aliibuka kuwa Raisi!!! Sasa hapo nani zaidi katiya Mwandosya Proffessional katibu mkuu na Raisi waliyekuwa kwenye tag of war?
Huo ni ushabiki unaoleta. Any damn fool or dictator can be president of a country depending on the circumstances at play. Sio wenye hekima au nguvu au akili wanaoshinda wakati wote.
 
Juzi hapa ilitangazwa kwamba Prof. Mwandosya ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa EWURA. Wengi walishangaa kwa nini Prof. Mwandosya kaletwa kutoka hali ambayo wengi wetu tulidhani ni ustaafu na kurudi kuwa Mwenyekiti wa EWURA.

Lakini hatupaswi kushangaa. Uteuzi wa Prof. umetukumbusha pia kwamba wakati Mkapa akikabiliwa na sakata la ununuzi wa rada toka Uingereza, ni Prof. Mwandosya alipewa jukumu la kuliweka sawa jambo hilo, hadi kukawa na joke kwamba Prof. Mwandosya alim-charm yule mwanamke wa Uingereza aliyekuwa akitutuhumu vikali hadi akabadilika na kusema "it wa a very wise decision by Tanzania to buy the radar!"

Na pia kwa mlio na ufahamu, wakati uhusiano kati ya Kiwete na Kagame umeharibika sana hadi Kagame kutishia kumpiga Kikwete ni Prof. Mwandosya alitumwa Rwanda kwenda kuweka mambo sawa.

Na labda niwaambie siri nyingine, wakati Kikwete anaona anashambuliwa kila kona kwa kuwa raisi dhaifu, ni Prof. Mwandosya aliitwa ofisi ya Raisi kama waziri asie na wizara maalum na kuwa mshauri wa karibu wa Kikwete. Matokeo tukayaona, ghafla Kikwete akaanza kuonekana kuwa na busara sana nchini na nje ya nchi. Ilifikia hatua watu wakasema unajua Kikwete aliwahi kugombea uraisi, bila kutambua kuwa kulikuwa na busara za Prof. Mwandosya nyuma ya utendaji wa Kikwete katika sehemu kubwa ya awamu ya mwisho ya uraisi wake.

Na hivi, ni Watanzania wangapi wanatambua kuwa dira ya maendeleo aliyotumia Raisi Mkapa kutukwamua kiuchumi (TANZANIA DEVELOPMENT VISION 2025) ni matokeo ya kazi ya Prof. Mwandosya baada ya kuambiwa na Raisi Mkapa asimamie utayarishaji wake? Najua wengi hawakujua hili kwa sababu ilipokamilika iliandikwa imeandaliwa chini ya Planning Commission, bila kueleza iliandaliwa chini ya usimamizi wa Prof. Mwandosya

Na tunaomfahamu Prof. Mwandosya, tunajua kwamba katika nyanja za kimataifa, alikuwa kinara wa majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi ulioitwa Kyoto Protocol, kiasi kwamba alisifiwa sana juu ya uwezo wake wa kuchambua mambo na Raisi Clinton wa Marekani, pamoja na Al Gore. Wakati huo Prof. Mwandosya alikuwa msemaji wa kundi la G77 & China, lakini hakuwa na madaraka yoyote serikalini Tanzania, jambo ambalo lilimfanya Raisi Clinton wa Marekani amshangae sana Mkapa kutomtumia ipasayo Prof. Mwandosya katika serikali yake - na ndipo Prof Mwandosya "alipoamriwa" na Mkapa akagombee ubunge.

Ndio maana imesemwa kwamba katika mambo ambayo hutakaa umdanganye Prof. Mwandosya ni mambo ya mikataba.

Na wakati fulani Prof. Mwandosya akiwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, kulikuwa na mbinu za nchi ya Misri kubadilisha makubaliano ya matumizi ya mto Nile ili kuinufaisha zaidi Misri. Ilibaki kidogo sana nchi za Mto Nile kutia sahihi mkataba huo mpya pale ambapo Prof. Mwandosya aliibuka tena na kuziamsha nchi nyingine juu ya vipengele kwenye makubaliano hayo mapya ambavyo vingezikandamiza. Kwa sababu ya uchambuzi wa ke huo, nchi zote za Mto Nile ziliwagomea Misri kuweka sahihi makubaliano hayo mapya. Hadi leo Misri hawataki kabisa kusikia habari za Prof. Mwandosya kwa kuwa wanamuona kuwa mtu aliewanyang'anya tonge mdomoni!

Na labda pia wengi waligundua kwamba mara tu baada ya Prof. Mwandosya kuteuliwa kuwa Mweyekiti wa EWURA, bei ya mafuta ilishuka kiasi tofauti na matarajio ya wengi, na wengi wamekuwa wakijiuliza kama ilikuwa ni utendaji wake kama Mwenyekiti wa EWURA uliosababisha kutoa ahueni kwenye bei za mafuta nchini.

Sasa kuna mengi juu ya Prof. Mwandosya naweza kusema hapa, lakini acha haya yatoshe kwa sasa ili kuweka backdrop ya swali langu. Kwa nini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi?

Swali langu pia linaendana na maoni ndani ya humu JF juu ya uteuzi wa Dr. Mpango kama Makamu wa Raisi. Kwa ujumla wengi wa wana JF hawaridhishwi kabisa na Dr. Mpango kuwa Makamu wa Raisi, hasa ukizingatia matukio ya hivi karibuni yaliyomhusu Dr. Mpango.

Sasa je, Kikwete hakukumbuka kwamba angalau Makamu wa Raisi wa Samia awe mmojawapo wa wagombea wa uraisi wa awamu ya Magufuli? Maana kama Prof. Mwandosya angekuwa Raisi badala ya Magufuli, hadi leo hii angekuwa ni raisi katika awamu yake ya mwisho. Je, inawezekana pia Kikwete hakumpendekeza Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi kutokana na ile issue ya "majina ya mfukoni"?

Kwa tunaomfahamu Prof. Mwandosya, ukiachia mbali porojo za humu JF, kama angekuwa ndio Makamu wa Raisi chini ya Raisi Samia, Tanzania tungeenda mbali sana na uongozi wa Raisi Samia ungeonekana ni bora na ungemfanya maarufu kwa scale ile ya Nyerere - mama wa Taifa!

Kwa hiyo naweza kusema kwamba katika hili ni wazi ubinafsi ulizidi maslahi ya nchi. Raisi Samia alipigwa chenga katika kuteua Makamu wa Raisi. Prof. Mwandosya angemfaa sana na tusingekuwa na habari za kulishwa samaki waliooshwa kwenye maji ya maiti!
Yaan hii nchi imechoka sana.Kikwete ni failure wa muda wote .Yupo tu kwa ajili ya katiba mbozi ya Nyerere.Leo ndio awe mshauri ?Tunazid kuanguka kwa ajili ya huyi Mzee asiyejitambua
 
Hivi hii dhana ya kufikirika kua Mama Samaia anashauriwa na Kikwete mliitoa wapi?
Mbona magu hamkua na hii dhana ya kushauriwa na kikwete na wengineo?

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
Hahahah! Magu ashauriwe? Alifikia mahali kutamba haambiwi la kufanya na yeyote. Washauri waliambiwa wanaropoka. Makamba alijifanya kutumia kiswahili chake kumshauri akapewa open kabisa sitaki ushauri wako, niache. Mbona hata Mkapa aliyekuwa chanzo cha kupaa kwake alitukanwa hadi akamzira alipotaka kumshauri? Kama unakumbuka, kuna Wakati Mkapa alisusia mialiko yote ya serikali - na ushauri pekee Magufuli aliowahi kuusikiliza ni kuambiwa nenda kamuombe msamaha Mkapa, for your own good.
 
Kwa hiyo mleta mada, unataka kutuambia mambo haya ya kufikirika.

1. Kikwete alimshauri Samia kuhusu Philip Mpango awe makamu wake wa Rais. Umejuaje?

2. Kikwete hakumshauri Samia kuhusu Professor Mwandosya kuwa makamu wake wa Rais. Umejuaje?

3. Kikwete huwa yuko busy kumshauri Samia kuhusu nani ashike nyazifa nyeti za serikali yake. Umejuaje?

4. Kitu chochote Kikwete anachomshauri Samia, ni lazima Samia afuate. Umejuaje?

Msingi wa hoja yako uko kwenye dhana ya kusadikika (assumption)
Maswali mazuri sana aisee maana watu wanakurupuka sana kila mtu mjuaji lakini Rais Samia Suluhu anachagua wale anaowaona watasaidia kuleta maendeleo tuache makasiliko jamani
 
Yaan hii nchi imechoka sana.Kikwete ni failure wa muda wote .Yupo tu kwa ajili ya katiba mbozi ya Nyerere.Leo ndio awe mshauri ?Tunazid kuanguka kwa ajili ya huyi Mzee asiyejitambua
Kwa taarifa yako Kikwete ndio rais bora nchi hii kuwahi kua nae na sidhani kama atatokea kama yeye miaka ya karibuni,

Alikua rais msikivu,
Aliekubali kukosolewa,
Na hata kwenye chaguzi zake hakukua na mauza uza kama tuliyoyaona 2020,
Alikubali tz ipate katiba mpya, ila aliefuata ukizungumzia katiba wasiojulikana halali yako, katiba ilivunjwa vunjwa kama vile nchi haina katiba wala sheria
Vyombo vya habari vilikua na uhuru na mengineyo mengi tu.

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom