Hizi ni timu 5 duniani zilizowahi kucheza mechi nyingi zaidi za ligi bila kupoteza

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,913

5. Al Ahly SC - Misri - 71​

Al Ahly

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Al Ahly mabingwa wa kistoria wa Misri ni moja ya klabu kubwa na tishio barani Afrika, ikiwa na rekodi ya kutwaa mataji 42 ya ligi kuu ya nchini Misri na mataji 10 ya ligi ya mabingwa Afrika.
Ikiwa na makao yake katika jiji la Cairo klabu hii iliweka rekodi ya kucheza michezo 71 bila kupoteza katika msimu wa mwaka 2004- 2007. Ikiwa ni sawa sawa na misimu mitatu rekodi hii haijavunjwa mpaka leo.

4. Esperance Sportive de Tunis-Tunisia – 85​

Esperance Sportive de Tunis

Esperance ni moja ya vilabu maarufu barani Afrika,ikianzishwa mwaka 1919 ni miongoni mwa vilabu vikongwe zaidi nchini Tunisia ikishabihishwa na jezi yake yenye mistari ya njano na nyekundu,imefanikiwa kutwaa mataji 32 ligi kuu ya Tunisia na kimataifa ikiwa na jumla a mataji 13 yakiwemoa mataji 4 ya ligi ya mabingwa Afrika.
Esperance imewahi kucheza karibu misimu ya ligi kuu Tunisia bila ya kupoteza ikicheza michezo 85 kati ya mwaka 1997 -2001.

3. Lincoln Red Imps Fc – Gibraltar – 88​

lincolnredimpsfc

CHANZO CHA PICHA,LINCOLNREDIMPSFC
Hawa ni mabingwa mara 24 wa ligi kuu ya Gibraltar ikitumia uwanja wa Victoria, uwanja ambao unatumiwa na karibu timu zote kubwa zinazoshiriki ligi ya nchini humo.
Ukiacha kucheza michezo 88 ya ligi kuu bila ya kufungwa kati ya mwaka 2009 mpaka 2014 pia klabu hii inarekodi ya kutwaa mataji 14 ya ligi katika misimu 14 mfululizo kuanzia mwaka 2003 -2016.
Mwaka 2014 ilikuwa klabu ya kwanza kutoka Gibraltar kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya .

2. FC Steaua Bucureşti - Romania - 106​

FC Steaua Bucureşti

CHANZO CHA PICHA,FC STEAUA BUCUREŞTI
FC Steaua Bucureşti ya Romania ni moja ya vilabu maarufu nchini humo, na ilifahamika zaidi katika soka la Ulaya baada ya kutwaa kombe la Ulaya mwaka 1986 ilipoichabanga Barcelona.
Ilikuwa haishikiki katika miaka ya 1980's. Iliwahi kucheza mechi 104 bila kufungwa kwa miaka zaidi ya minne kuanzia June 1986 mpaka Septemba 1989.
Katika kipindi hicho imefanikiwa kutwaa mataji manne ya ligi kuu. Inatajwa ndio klabu bora kuwahi kutokea Romania.

ASEC Mimosa – Ivory Coast – 108​

ASEC

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Arthur Pierre (katikati) wa Asec Mimosa akizingirwa na wachezaji wa Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia, katika moja ya mechi za mabingwa Afrika, iliyopigwa Julai 24, 2005 kwenye uwanja wa Felix Houphouet Boigny mjini Abidjan


Les Mimos, kama wanavyofahamika kwa jina la utani, ni moja ya vilabu vikongwe barani Afrika ikitwaa mataji 24 ya ligi kuu ya nchini Ivory Coast. Ikiwa na maskani yake Abidjan ina historia isiyozingatiwa sana ya kucheza michezo 108 ya ligi bila kupoteza. Ilifanya hivyo kati ya mwaka 1989-1994. Mpaka sasa rekodi yake haijawahi kuvunjwa.
ASEC ilizuiwa kuweka rekodi zaidi ya kutopoteza kwenye ligi kwa kuchapwa na wapinzani wao, klabu ya SO de l’Armée, ilikuwa mwaka 1994.
Kwa miaka 28 sasa, rekodi yake haijavunjwa na inabaki katika historia ya soka duniani ya kuwa timu iliyocheza michezo mingi zaidi ya ligi ya nyumbani bila kupoteza.
 
Yanga kelele nyingi kama chiriku, wapuuzi sana.
 
Back
Top Bottom