GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,689
- 109,114
"Sisi Yanga SC siyo Timu ya Kulialia na Kudekadeka kama Wengine kuomba Mechi zao za Ligi zisimamishwe wakidhani hivyo Viporo vyao watavila wakati Yanga SC tumejiandaa kuhakikisha Viporo vyao vyote Vinachacha na Vitachacha. Yanga SC tutaendelea kucheza Ligi na kucheza Mechi za Kimataifa ili kuonyesha tofauti yao na yetu" amesema Msemaji wa Yanga SC Ali Kamwe leo akiongea na Waandishi wa Habari na hii Taarifa yake ilirushwa Hewani na EFM Radio katika Kipindi chao cha Michezo cha Saa 2 Usiku cha E-Sport.
Ali Kamwe leo Wewe ni wa kusahau kuwa Uongozi wa Klabu yako kupitia Rais Injinia Hersi Said mwaka jana ( 2023 ) zaidi ya mara Tatu mkiwa mnacheza Mechi zenu za CAFCC mliofika Fainali na hata baadhi ya Mechi za CAFCL mliomba kwa TFF Mechi zenu za Ligi Kuu ya Tanzania ya NBC zisogezwe mbele ili mjiandae vyema na Mechi zenu na muiwakilishe Tanzania vizuri?
Ali Kamwe unachokikosoa Wewe leo kwa Simba SC kuomba TFF Mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar FC ili ijiandae vyema na Mechi yake ngumu ya CAFCL dhidi ya Timu bora na Shindani hasa ya Asec Mimosa FC kina tofauti yoyote ile na kile ambacho Yanga SC ilikifanya mwaka jana na huenda pia ikitokea mkafanya vyema huko mbeleni nanyi pia mtakifanya hiki hiki kilichofanywa na Simba SC?
NI kwanini Watu makini na Msomi mzuri kama Wewe Ali Kamwe mkihamia tu kuwa Watendaji wa hivi Vilabu vikubwa viwili hapa Tanzania vya Simba na Yanga huwa mnabadilika na kuanza kuwa Wapumbavu Wapumbavu huku mkiwa mmetawaliwa na Ushamba, Utoto na Upuuzi?