Hizi ni mbegu za mmea gani?

charminglady

HIZO MBEGU ZINATUMIKA SANA NA KUTENGENEZA UREMBO WA SHANGA. ILA, NARUDIA ILA, HIZO MBEGU NI SUMU NA UKIZIONA WEKA MBALI SANA NA WATOTO NA ZINAWEZA KULETA MADHARA HATA KWA WATU WAZIMA PIA. NA SI MTI NI ILE MIMEA YA KAMBA KAMBA INAOTA KWA KASI SANA NA KUJAZANA SEHEMU MOJA KWA KUTAMBAA.

MAJANI YAKE YANAFANANA NA ILE MIMEA UKISHIKA MAJANI YAKE YANASINZIA HIVI. HIVYO USIJARIBU KUWEKA MDOMONI UTADHURIKA.
Umeona hili ni jukwa la siasa unaleta uongo wako hapa???
 
Wanaosema hizi mbegu ni sumu si kweli, siwezi kuwaita WAONGO kwa Sababu ndio walivyosoma kwenye mnazoziita Link!!

Lakini hizi mbegu binafsi nimemeza sana tu utotoni nikiaminishwa kuwa ni kinga ya macho(red eyes).

Na kweli ule ugojwa sijawahi umwaga!! Labda ni kwa imani tu lakini sikuwahi kuumwa!! Tunaoishi nnje ya mji hapa Dsm tunaweza kuziona kwenye vijiporipori!!

Mpaka sasa nikizifumaniaga nameza tu kwa kuwa hzina madhara yyte na bado naamini ni kinga ya macho!!
Mkuu kwa wenyeji wa Pwani na Dar hizo zinaitwa sipo.Tatizo watu wengi wana google vitu bila kujua reality.Hizo mbegu nimezimeza sana nikiwa mdogo kwa imani ile uliyesema mwanzo kwamba ni kinga ya macho na sikuwahi kupata madhara yoyote.
 
Umeona hili ni jukwa la siasa unaleta uongo wako hapa???



MIMI UONGO WANGU NIMEUSINDIKIZA NA USHAHIDI WEWE USHAHIDI WAKO UKO WAPI?

USIWE UNAROPOKA TU KWANZA UNA BAHATI KUPATA 5MINS ZA MAISHA YANGU KUJIBU UJINGA WAKO.

HALAFU UTAKUTA ETI NA WEWE NI MSOMI HUKU UNACHOANDIKA HAKINA TOFAUTI NA LEVEL YA PANYA ROAD
 
Hizi mbegu mwisho wa siku zitasababisha kifo hapa jamvini, wengine wanasema mbegu hizo zinatokana na miti (hizi sizifahamu, labda zinaweza kuwa salama), lakini hizi zinatoka kwenye mmea unaotambaa kwenye miti mbegu za mmea huo ni sumu.
 
HIZO MBEGU NI SUMU KWELI ZINA PROTEIN AMBAYO NI ABRIN NA NI SUMU KALI SAWA NA RICIN
Hizo mbegu kipindi nikiwa MDOGO tulikuwa tunazichezea sana yaani tulikuwa tunazimeza nzima nzima halafu ukienda kunya unazinya kwetu tulikuwa hatutumii vyoo
Pia hizo mbegu ukizipasua ndani ni kama ilivyo dengu ila ni chungu si chungu
Umenikumbusha mbali sana miaka ya 1990 kurudi nyuma
 
Mi najua kwa jina la mturuturu kwa kigoma kwetu, tiba ya bawasiri unachoma unapaka kwenye kile kinyama kwa nilivyoelekezwa mdogo wangu alipona
 



MIMI UONGO WANGU NIMEUSINDIKIZA NA USHAHIDI WEWE USHAHIDI WAKO UKO WAPI?

USIWE UNAROPOKA TU KWANZA UNA BAHATI KUPATA 5MINS ZA MAISHA YANGU KUJIBU UJINGA WAKO.

HALAFU UTAKUTA ETI NA WEWE NI MSOMI HUKU UNACHOANDIKA HAKINA TOFAUTI NA LEVEL YA PANYA ROAD
Mkuu hizo mbegu nazijua kwa jina simbo hazina sumu yoyote utotoni tulizimeza sana. Labda kama ubishi na matusi ni sehemu ya maisha yako.

Nashangaa sana msomi kama wewe bado unapanic na kutukana hovyo tu, wengine tuko kwenye huu mtandao tukiamini kabisa ni watu wazima na heshima zetu hatuna mtandao mwingine zaidi ya huu.
 
Ni kweli tushameza sana watu tukiwa watoto tulizichezea tukiweka mbele y'a Magari y'a udongo kama t'aa.
 
Mkuu hizo mbegu nazijua kwa jina simbo hazina sumu yoyote utotoni tulizimeza sana. Labda kama ubishi na matusi ni sehemu ya maisha yako.

Nashangaa sana msomi kama wewe bado unapanic na kutukana hovyo tu, wengine tuko kwenye huu mtandao tukiamini kabisa ni watu wazima na heshima zetu hatuna mtandao mwingine zaidi ya huu.

MTU MZIMA MWENYE KUJIHESHIMU ANAJIBU MTU KAMA ULIVYOJIBU WEWE?

MIMI NIMESEMA NI SUMU NA NIWEKA USHAHIDI WA UTAFITI ULIOFANYWA KUHUSU HIZO MBEGU

ILA WEWE UNAASHINDWA KULETA USHAHIDI ILA UNAANZA KUNISHUTUMU MIMI

WEWE ULICHOTAKIWA KUSEMA SIYO KWELI USHAHIDI HUU HAPA BADALA YA KUANZA KUMKOSEA MTU HESHIMA

UWE NA USIKU MWEMA ILA TAMBUA URUHUSIWI KUKOSOWA AU KUTUKANA WATU KAMA HUNA USHAHIDI SAWA

TUNZA HESHIMA NA WEWE UTUNZIWE HESHIMA NDUGU YANGU
 
Huo mmea Usukumani si ndo huwa tunauita Wilulya? Na mmea wake kwa kweli naufahamu huwa unatambaa kwenye miti mingine ila matumizi yake mengine siyajui zaidi ya kuwa ni kwa ajili ya urembo. Wakati tukiwa wadogo machungani tulikuwa tunazichuma sana!
 
Mkuu kwa wenyeji wa Pwani na Dar hizo zinaitwa sipo.Tatizo watu wengi wana google vitu bila kujua reality.Hizo mbegu nimezimeza sana nikiwa mdogo kwa imani ile uliyesema mwanzo kwamba ni kinga ya macho na sikuwahi kupata madhara yoyote.
Kwa waliowahi kuishi kusini wanaziita Numbinumbi na hazina sumu maana zingekua na sumu zingeua mamia kwa maelfu ya watoto, hata hivyo inawezekana kwa aina ya jamii hizo kuwa na sumu. Kwani uyoga si unaliwa lakini aina nyingine si una sumu? Mihogo hii kila mtu anaifaham, lakini kuna mitamu na yenye sumu kali pia. Hivyo haishangazi
 
Habari za mchana mabibi na mabwana jamvini hapa?

Hizi hapa chini ni mbegu za mmea gani na zina kazi gani? Nikiwa mdogo nilikuwa naziona kwa bibi yangu, na alikuwa anazitunza sana.

Sikuwahi kufikiria kuwa ni mbegu za mti, wala sikuwahi kumuuliza kazi yake. Sasa hivi karibuni nikauona huo mmea mahali fulani na mbegu zake hizo, nikagundua kumbe hizo ni mbegu za mme. Bahati mbaya bibi yangu kwa sasa ni marehemu.

Je hizo mbegu ni za mmea wa aina gani na kazi yake ni nini?
Sisi tulikua tukiziita SIPO na hukaa ndani ya ganda linalopasuka likikauka
 
kijijin kwetu ilikuwa ukimeza ka moja huumwi macho mwaka mzima,ukimeza viwili hvyo hvyo miaka miwili sasa cjui kweli au ilikuwa imani tu na ukiiba mazao ya mtu akichoma hyo mbegu ikipasuka na ww tumbo lina burst,unaitwa "kamturuturu"
 
Zinaitwa Sipo, ukimeza mbegu hizo ni kinga ya ugonjwa wa macho!!
Yaani hutaumwa na macho(red eyes) tena!!
Kama ni hizo, ni sawa comment yako. Lkn jinsi mleta uzi alivyozi'zoom, zimekuwa kubwa kama karanga, wakati mbegu zenyewe ni ndogo kama shanga za kinyanwezi.
Hizo ni mbegu za mmea uotao porini ni jamii ya climbers. Hukua kwa kutegemea kukwea mti mwingine kujiimarisha.
Mbegu zake ni kama ulivyoeleza. Humezwa kama kinga ya ugonjwa wa macho. Ukimeza idadi kmf:10, basi utakuwa excused kuugua macho kwa miaka ya idadi ya hizo mbegu.
Pia mizizi yake hutumika kama dawa ya kuongeza nguvu za...me.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom