Mbowe tena, DC ampiga marufuku kulima shamba lake

Mbowe tena, DC ampiga marufuku kulima shamba lake

COLE

Member
Joined
Oct 21, 2006
Posts
89
Reaction score
80
Mkuu wa Wilaya ya Hai amepiga marufuku kuendeleza kilimo kwenye Shamba la Mbowe ambalo ni shamba la urithi, sababu kubwa
shamba hilo liko kwenye chanzo za mtu weruweru

Source: Mtanzania
 
Kwani hilo shamba tangu awali lilikuwa halijaendelezwa? sijaelewa hapo
 
Kama mnakumbuka Mbowe aliwahi kuonesha misimamo miwili tofauti kuhusu migogoro ya ardhi katika wilaya za Bagamoyo na Hai...
Mnamo Mei 19, 2016 katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mbowe alitaka kufahamu ni kwa nini serikali imeshindwa kuliendeleza shamba la miwa la Bagamoyo ambalo lingeweza kusaidia kuzalisha sukari.
Majibu ya Mh. Waziri Mkuu yalikuwa hivi:
"Mradi wa kilimo cha miwa Bagamoyo ungeweza kuyakausha maji ya MTO wami ambapo ingehatarisha maisha ya binadamu pamoja na viumbe wengine waliopo katika hifadhi ya taifa ya Saadani".

Wakati mbowe anaitaka serikali kuwaondoa wanabagamoyo katika ardhi yao ili kupisha mradi wa kuzalisha sukari,hapo hapo mbowe anaonekana kupinga mradi wa serikali wa kuwahamisha baadhi ya wanaHai na wanaMERU ili kupanua uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA).
Jambo ambalo linaonekana mradi wa kupanua uwanja wa KIA ulikuwa unapigiwa debe na mafisadi kwa lengo la kunufaika na ardhi kupitia mradi huo.

Sasa DC wa Hai amemfuata mbowe nyumbani kwake kwa kuzuia shughuli za kilimo katika shamba la mbowe linalodaiwa kuwa lipo katika chanzo cha MTO Weruweru...

My take:
Kama lengo la DC huyu wa Hai ni muendelezo wa kupambana na shughuli zinazoharibu vyanzo asili vya maji litakuwa ni jambo jema..
Ila kama ni muendelezo wa hii serikali kuwafilisi viongozi wa upinzani watambue kuwa nyuma ya upinzani kuna wananchi zaidi ya million 8 wakihitaji mabadiliko ya kweli.
 

Attachments

Mkuu hakuna cha wananchi milioni 8 nyuma ya upinzani wanaotaka mabadiliko ya kweli. Watanzania walishawafahamu mafisadi ni akina nani na sasa wameshajitoa kwao. Mafisadi waliojinasibu kuwa wanataka mabadiliko ya kweli ndo hao akina Mbowe, Lowasa, Sumaye, Kingunge, Msigwa, Lisu and team. Mwaka 2020 ndo msemakweli. Tusubiri.

TUMEWASHTUKIA NA TUMEWAKATAA.
 
Halafu baadaye watamnya'anganya kwa kigezo cha shamba pori
 
Back
Top Bottom