Hizi ndio bei za mbolea ambazo wakulima watanunulia kuanzia Agosti 15, 2022 baada ya bilioni 150

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Utashangaa kiukweli hii inaonyesha ni Kwa namna gani serikali inawasikiliza watu wake hasa katika kuhakikisha inawapunguzia makali wakulima kutokana na hali ya kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia si Tanzania pekee bali ni ulimwenguni kote. Zipo sababu kadhaa zilizosababisha bei kupanda ikiwemo ugonjwa wa Covid-19 na mgogoro unaondelea kati ya Ukraine na Russia ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji na upatikanaji wa mbolea.

Kwa jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wakulima wa Tanzania sasa watanunua mbolea hizo kwa bei nafuu licha ya yote yanayoendelea ili tu isiathiri msimu wa kilimo na pia kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

AINA ZA MBOLEA NA BEI ZAKE
1. DAP ingeuzwa sh 131,676 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 70000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 61676.

2. UREA ingeuzwa sh 124,734 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 70000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 54,734.

3. CAN ingeuzwa sh 108,256 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 60,000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 48,156.

4. SA ingeuzwa sh 82,852 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 50,000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 32,852.

5. NPK's ingeuzwa sh 122,695 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 70,000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 52,695.​
 
Mh. Rais wetu anaupiga mwingi sanaa, hakika anaipenda nchi hii na kuwajali wananchi anaowaongoza, amekonga nyoyo za wakulima, amegusa maisha yao, amewapa furaha na matumaini makubwa sana. Ni shujaa wa watanzania, wakulima, watanzania wazalendo, na uchumi shirikishi.
 
"Ingeuzwa"......"ingeuzwa"/...."ingeuzwa"......blah blah

Hakuna kitu kama hicho

Ingeuzwa chini ya hizo bei zenu nyie mmezipandisha na ku act eti "ingeuzwa 131,676/=" ya kutunga

Cartel ya mbolea hii wakishirikiana na serikali

Ukishaanza kuona "ingeuzwa" maana yake ni uongo....bei ni 70,000 na mafaida yao kibao ndani...mbolea kiuhalisia ni chini ya hiyo 70,000/=

Mama Samia kaweka hela,and blah blah....uongo mtupu
 
Ila kubwa zaidi tungejipanga kama taifa kuwekeza kwenye viwanda vingi vya kuzalisha hizo mbolea ili bei iwe chini zaidi na yenye ahueni kwetu wakulima na itakayoleta faida zaidi tukiuza kwenda nchi jirani
 
Mh Rais wetu anaupiga mwingi Sanaa, Hakika anaipenda nchi hii na kuwajari wananchi anaowaongoza, amekonga nyoyo za wakulima, Amegusa maisha yao, Amewapa fulaha na matumaini makubwa Sana, Ni shujaa wa watanzania, Ni shujaa wa wakulima, Ni shujaa wa watanzania wazalendo, Ni shujaa wa uchumi shirikishi,
Aliyepandisha bei nani? Nipandishe mimi nishushe mwenyewe
Ndo kuupiga mwingi?
 
Back
Top Bottom