Hivi yule anayelia kwenye tangazo la "Wamekataaa" anazungumza nini?

Solita

Member
Nov 29, 2010
47
4
Jamani hivi yule mtu anayelia kwenye tangazo linalojulikana kama "wamekata" huwa anazungumza kitu gani maana najitahidi ili nielewe kuhusu hilo tangazo hasa kwenye hicho kipengele lakini siambulii kitu, anayeelewa anijuze! karibuni
 
Sipendi kabisa kulisikia hilo tangazo, ni la kipuuzi kabisa, nashangaa kama kuna kampuni zinafanya commercial advertisement za kipuuzi na namna hii na kampuni zinawalipa pesa. upuuzi mtupu.
 
hahaha yule analia wamekata ada yake......anasema "wamentumia ada ya shule.....wamekata" hua nacheka sana nikisikia hilo tangazo
 
yaani makampuni ya simu ukituma hela kutumia mfumo wao unakatwa gaharama ya kutumia huduma yao. so yule walikata hela ya fee so akawa analia. mia
 
Airtel wana ponda Voda hao tuu watakatajeee.... haha basi sina mbavu
 
airtel wao ukitumiwa hela au ukituma ni bure, lakini voda na tigo wanakata, i mean unachajiwa gharama za huduma,
ndo tangazo limekaa ki ivo......huwa nacheka sana tangazo lile, kwani matangazo mengine yamekaa ngono tu,hebu tangazo la habari leo kuna haja gani yule dada kupekua pekua mipaja yake
 
Lile tangazo hata mtoto wangu anajua nalipenda sana,
Maana linawekwaga asubuhi wakati nampeleka shule.
Akisikia tu anaanza kunitania, "Baba Mwanao huyo" (nimsikilize), nami namtania kua ndio yeye, basi full kicheko.

But kiufupi kuna ka-ambiguity pale, kwani ukituma School Fees ya Tshs 300,000/- ukakatwa Tshs 2,000/- unaweza kuijazia from pocket money na isilete effect kubwa sana kwa transaction ambazo zinatokea occasionally/rarely!!,
So wametuingiza mkenge!!
 
Sipendi kabisa kulisikia hilo tangazo, ni la kipuuzi kabisa, nashangaa kama kuna kampuni zinafanya commercial advertisement za kipuuzi na namna hii na kampuni zinawalipa pesa. upuuzi mtupu.
Ni kweli tangazo limekaa kipuuzipuuzi tu. Airtel wanawezaje kumlipa mtu kihiyo namna hiyo asiye na mvuto!!!
 
Sipendi kabisa kulisikia hilo tangazo, ni la kipuuzi kabisa, nashangaa kama kuna kampuni zinafanya commercial advertisement za kipuuzi na namna hii na kampuni zinawalipa pesa. upuuzi mtupu.

Nilifikiri ni mimi tu, yaani linakera mpaka ninalazimika kufunga radio kwa muda!
 
Lile tangazo hata mtoto wangu anajua nalipenda sana,
Maana linawekwaga asubuhi wakati nampeleka shule.
Akisikia tu anaanza kunitania, "Baba Mwanao huyo" (nimsikilize), nami namtania kua ndio yeye, basi full kicheko.

But kiufupi kuna ka-ambiguity pale, kwani ukituma School Fees ya Tshs 300,000/- ukakatwa Tshs 2,000/- unaweza kuijazia from pocket money na isilete effect kubwa sana kwa transaction ambazo zinatokea occasionally/rarely!!,
So wametuingiza mkenge!!

Nakubaliana na wewe kwani enzi zile za kutuma pesa kwa basi ilikuwa ni gharama kubwa hapo bado hujahesabu muda mrefu unaotumika na wakati mwingine pesa kupotea.
 
Lile tangazo ni kiburudisho changu nilickia me hoi kwa kucheka......"Wamaentumia ada ya shule Wamekataaaaaaaa!!!!!
 
Back
Top Bottom