Tangazo la kujiunga JKT kwa mujibu wa sheria 2023

TrueVoter

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
2,207
1,785
Wanabodi na wapiga kura wenzangu

Nimeguswa na kushangazwa niliposoma tangazo kutoka kwa Mkuu wa JKT akitoa maelezo kwa vijana watakaojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2023..maana yangu ni njema, kutaka ufafanuzi kwa jambo hili kulingana na maelezo yaliyotolewa.

Inakuwaje serikali inashindwa kutoa pesa kugharimia mahitaji ya vitu vilivyoorodheshwa kwenye tangazo kwa ajili ya vijana wa nchi hii wanaojiunga JKT kwa mujibu wa sheria 2023..na hii sasa imekuwa kawaida, kuna tatizo gani kila inapotokea jambo linahusu vijana/ watoto wa nchi hii serikali inarusha jukumu hilo kwa wazazi/ walezi, huko waliko maliza kidato cha sita, pamoja na serikali kuondoa ada, michango ambayo wazazi/ walezi wamechangia kwa shule walizokuwa hawa vijana kwa miaka hiyo miwili ni zaidi mara mbili au tatu ya ada iliyofutwa! kwani hela wanayolipa wazazi kupitia kodi kugharimia mambo ya serikali na nchi kwa ujumla ni vibaya au haiwezi kupangiwa kugharimia mambo ya watoto wetu wenyewe? ila kununua magari mapya kwa viongozi ni sahihi..kwa nini inakuwa hivi. Serikali inaweza kutaja sababu kwa nini haiwezi kugharimia mahitaji yaliyowekwa kwa hawa vijana?

Huo uzalendo na moyo wa kulipenda taifa lao utajengwa vipi kwa mtindo kama huu kwa serikali kuwakana hawa vijana halafu inatumia hela kwa mambo mengine yasiyo na maana yoyote? Ni wapi serikali imeonyesha kuelewa thamani ya vijana hawa kwa taifa hili kama inakwepa kubeba gharama ndogo hizi za mahitaji kujiunga JKT?

Serikali wanaweza kugharimia safari ya timu kwenda kucheza ugenini lakini hawako tayari kugharimia nauli za watoto kwenda na kutoka kambini..inakuwaje mambo haya? au kwenda JKT ni hisani? na hivyo si lazima kuwagharimia mahitaji hawa vijana, kama ni hivyo kwa nini kusema ni kwa mujibu wa sheria? Tafadhali sana, nawasihi na hasa Mh.

Rais Dkt. Samia Suluhu tendeni vile inapaswa kwa serikali kutendea watoto/vijana wa nchi hii..naiomba serikali ibebe hizo gharama za mahitaji yote ya kujiunga JKT kwa mujibu wa sheria 2023. Hivi likizuka la kuzuka hapa, au janga lolote lile..Mungu apishe mbali, vijana hawa ndio watetezi wetu!

Inakuwaje hatuonyeshi kama tunajua mambo haya? Au sisi Tanzania ni maalum sana kwa Mungu na hivyo hakuna lolote baya linaweza kutupata? Vijana mahali popote ndiyo fahari ya nchi! Hupaswi kuwatendea hivi!
 

Attachments

  • en-1685002495-Barua Mujibu wa Sheria 2023.pdf
    704.3 KB · Views: 21
Kwani lazima? Nisipompeleka atakatazwa kwenda chuo? Atakosa mkopo chuo? Gharama nyingine za kujitakia?
 
... kwa mujibu wa sheria halafu ni wachache wameitwa! Sijui sampling imetumia vigezo gani. Na ukichunguza most likely ni makapuku wameitwa huko.
 
Ni aibu na ni dhuruma sana serikali kumbebesha mzazi gharama za kumpeleka kijana JKT kama vile anakwenda kwa hiari yake na siyo kwa mujibu wa sheria. Kwenye mahitaji wanayotakiwa kwenda nayo wamesahau tu kuweka na mess tin, berrets, boot, mkanda wa kijeshi na SAR lakini kwa mwendo huu itafika wakati serikali itawataka vijana wajinunulie vitu hivyo na kuripoti kambini wakiwa navyo.
 
Mnapojiunga shule za umma na mahitaji huwa mnapewa bure?

Acha visingizio, nenda Jeshini badala ya kushinda Instagram faida zake utaziona baadaye.
Jibu hoja we mburura. Hela zote zinazoliwa kwenye ripoti ya CAG wanakosa fungu la kulipia vijana wajiunge Bure JKT
 
Jibu hoja we mburura. Hela zote zinazoliwa kwenye ripoti ya CAG wanakosa fungu la kulipia vijana wajiunge Bure JKT
Mburura ni baba yako ambaye angekumbuka kutumia condom asingeleta taahira kama wewe duniani.
 
Back
Top Bottom