DOKEZO Tumeomba ajira Polisi tumelipishwa Shilingi 30,000, hivi zinaenda wapi hizo fedha?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hivi karibuni kulitokea nafasi ya ajira za Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi ambapo zaidi ya Wananchi 1,000 walituma maombi ya ajira.

Lakini wakati mchakato unaendelea, sisi tuliopata nafasi ya kuomba ajira na kuitwa kwenye mchakato wa usaili, tukatakiwa kutoa kila mmoja shilingi 30,000.

Kwa kuwa watu tupo na kiwewe cha kupata ajira tumelazimika kutoa tu kiasi hicho cha fedha bila kujua tunatoa kwa ajili ya kitu gani.

Nilipojaribu kudodosa kutokana na uzoefu wa kazi yangu nikajulishwa kuwa wale wanaosimamia mchakato wa usaili pia wanalipwa posho ya kila siku (per diem) ya zoezi hilo, sasa hizo Sh 30,000 nazo zimeenda wapi?

Nisiongee mengi nisije nikakosa ajira yenyewe bure ila nimeona nifikishe taarifa hii inaweza kusaidia Serikali kufanya kitu, au kama IGP anajua malipo hayo aweke wazi hadharani kuhusu buku 30 zinapoelekezwa.
 
Polisi wana zile Fedha wanakusanya kila mwaka sijui Stika ya kwenda ya kusalama ni mfuko wa watu ule yaani unalipia Stika mtu anaweka hela kwenye Begi Nchi hii ngumu sana aisee..
 
Back
Top Bottom