Hivi Wakenya wametushinda nini?

Hivi Wakenya wametushinda nini?

Ukikutana nao nje ya nchi wana confidence za kufa mtu. wakiwa kwao hawataki longo longo na kama hawaelewani watapigana mikwaju kisha wanadeliver

Tazama KTN au KBC picha ziko clear, news zimetulia, watangazaji wametulia

Soma gazeti la NATION au Standard...huwezi fananisha na lile gazeti la Michuzi (daily nyuz) au lile la copy and paste (guardian)

sisi tuna watu wengi zaidi, rasili mali nyingi zaidi, wanasiasa wengi zaidi, vyama vya siasa vingi zaidi, magazeti mengi zaidi, JF ndio zaidi, cabinet yetu kubwa kuliko ya kwao, katiba yao (na mahakama ya kadhi ndani) ndio walipitisha, sasa kwa nini hawa wana deliver na sisi hatuna kitu?

I've tried to hate them lakini nimeshindwa, cant hate their ambition esp based on their national interest.

Halafu wao kujenga li Superhighway kama hili ili iweje?

ahh sisi hata kuthubutu tunashindwa sijui kwa nini

7293527580_6750ff3295_b.jpg
wametushinda kilakitu, .........sio dhaifu!!
 
WAMEPATA ELIMU YA KWELI. Wako serious,wanajua wanacho kitaka and they are focused.kwao wao politics zao uongo na hadaa kama zetu hawana.hawana mchezo na elimu na ndio maana hukuti shule yenye walimu half cooked kama hapa kwetu. uliona wapi dunia hii darasa la chuo kikuu lina wanafunzi 2000?? no seriousness.
 
kenya ni kubwa! Hasa Nairobi. Imesambaa kweli! Mandhari ya Nairobi ni nzuri sana. Hali ya hewa perfect. Nairobi ina magari mengi. Watu wengi wa Nairobi wanajua kufanya shopping. % 70 ya products zilizo kwenye supermarkets ni zao la Kenya. Ni wakenya wenyewe ndio utawakuta kwa wingi sana wakinunua kwenye hayo masoko.

Nairobi ina majengo mazuri makubwa, na mengi ni ya ghorofa na apartments. Zimetapakaa jiji zima na ziko katika mpangilio fulani wa kupendeza. Maji ni mengi na hayakatiki. Umeme hausumbui. Kenya wamejaa watu wa mataifa mengi ya Afrika na nje yake. Wengi wamefuata elimu. Haya ni ya Nairobi btw.

Kingine ninachoona kwenye mji huu ni pia ni wingi wa maisha ya kati na duni. Traffic very disorganized. Kilicho kibovu kabisa na ambacho naisifu Tanzania kwa hilo ni usafiri wa umma. Kenya zinatumika matatu(vipanya), tena ndani ya jiji. Vimeshona muda wote, vimechakaa, ngumu kupata usafiri wa umma. Sijaona dcm wala costa wala eicher, wala yale mabasi makubwa ya kichina. Usafiri hovyo kabisa. Hapo ndio tumewapiga bao. Mengine najua wametuacha
 
sasa inasemekana kuwa viongozi wao wanakuja kuficha pesa zao kwa viongozi wetu

so hawajatushinda kila kitu
 
Wako kikazi zaidi na si wavivu wa kufikiri kama Wabongo wengi tulivyo, hawaruhuru watu wengine wafikirie badala yao. Bora umeliona hilo!!!
Wametuzidi katika matumizi ya "The latest Export Version 5" ya Opera System...Walianza enzi za Aloha, wakaja juu kwenye interface yake, Micros-Galileo, na baadaye kwenye Micros-Fidelio. Ni wataalamu katika wizi kwenye Point Of Sales za aina yeyote ile.

 
Pamoja na hayo Wa TZ ni nomaa kwanza hatuko pride na nchi yetu na pili ni wa binafsi ndio maana hakun maendeleo na hakutakuwa na maendeleo kwa vile hatupendani sisi kwa sisi
 
Ni wataalamu katika wizi kwenye Point Of Sales za aina yeyote ile.


Na sisi utaalamu wetu uko wapi? Kumwita mchina machinga pale kariakoo kuwa ni "mwekezaji" na mtz mmachinga wa kawaida kuwa ni "mzururaji"?
 
Mbona kama manzese tu, mi nilifikiri flyover kumbe! Hata kama nchi yangu inaniuma sana lakini siwezi kutoa sifa za kijinga. Kwanza walipigana dr. Kikwete ndie alie wapatanisha. Wanajua kupigana tu lakini sio kupatana. Hata kofii alomide alishindwa kuwapatanisha.
 
Mbona kama manzese tu, mi nilifikiri flyover kumbe! Hata kama nchi yangu inaniuma sana lakini siwezi kutoa sifa za kijinga. Kwanza walipigana dr. Kikwete ndie alie wapatanisha. Wanajua kupigana tu lakini sio kupatana. Hata kofii alomide alishindwa kuwapatanisha.

THIKA ROAD

troad.jpg
 
Nyie wavivu sana kufanya kazi, nenda kwenye mashirika yenye wakenya hapa Tanzania utakuta wabongo wanalia lia eti wanaonewa! mmekalia uvivu tu

Kwa kuongezea tu, sie wabongo tunapenda njia za mkato ambazo hazina kichwa wala miguu katika utendaji kazi. Ukizoea shortcut in life lazima utalalamika tu kwa kusema unaonewa mara ufanyapo kazi na wachapa kazi kama wakenya.
 
Wakenya walituacha kipindi cha ukoloni na wakazidi kutupita kipindi cha mapambano ya uhuru wa afrika (1960-1980s) bila kusahau sera ze2 za ujamaa na ubepari.
 
Napenda sana JF ingetawaliwa na mabishano kama haya kinyume na yale ya kusakamana sisi kwa sisi yasiyo na kichwa wala miguu... Yaani leo mminikuna kweli kweli...
Kimsingi hawa jamaa hawana cha kutushinda kiutajiri wa nchi, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Kiuchumi ingawa wao wako juu lakini ni wazi kwamba uchumi wetu ndio una potential maradufu kuliko wao. Uchumi wetu umekua unakua kwa wastani wa 7% tangu mwaka 2000 wakati wa wakenya unasua sua vibaya mno kama mapigo ya moyo ya mtu aliyepigwa tofari la kifuani, ukuaji wa uchumi wao ulishawahi kufikia 1.5% mwaka 2008 na chini ya 1% mwaka 2002 kama sijakosea, Kwa wasioelewa ukuaji wa uchumi unamaanisha kwamba uchumi unapotential au utajiri kiasi gani...

Yaani pamoja na kujutahidi sana ukuaji wa uchumi wa Kenya mwaka jana ulifikia 5% wakati sisi hadi Disemba 2012 ukuaji wa uchumi wetu ulifikia 7.1% hii inamaanisha kwamba uchumi wetu unakua haraka zaidi kuliko wa Kenya na tutakuja kuupita uchumi wa Kenya ndani ya miaka kadhaa, hasa ukizingatia utajiri wa kiuchumi tulio nao ukilinganisha na wakenya. kwa uchache tu sisi tuna mvua nyingi pamoja na Ardhi inayolimika kuliko Kenya, tuna mafuta, madini n.k... katika ripoti zao kila siku wanasema uchumi unadorora sababu ya ukame.... na huwa nashangaa katika VISION 2030 yao wanasema wanataka uchumi wao ukue kwa 10%, lakini hawana uwezo huu....ila kinachonishangaza zaidi sisi katika VISION 2025 yetu tunasema tunataka uchumi wetu ukue kwa 8% wakati unaweza na una potential ya kukua kwa 10% na zaidi tukawafikia na kuwazidi hawa jamaa mwaka 2015 tu.... na rekodi inaonesha hivyo..... tunachokosa sisi ni AMBITION, jamaa hawana uwezo lakini wana ambition kubwa hao ndio kinachowabeba beba.... lakini sisi tukipata viongozi madhubuti, hawa jamaa watakua hawana cha kutambia mbele yetu.... uongozi wetu wa sasa una porojo nyingi sana, hauna ambition na uwajibikaji....Tuanzia kutatua tatizo hapa!...
Besides Kenya ina maskini wengi kuliko Tanzania (angalia CIA world factbook) na ripoti nyingine zote za World Bank, IMF, African Development Bank. Besides wao kila kukicha na Elshabab sisi hatuna hizo insecurity issues!.....

Pia nafurahia namna serikali yetu inavyoyapoke na kufanya maamuzi ya mambo yanayohusu jumuiya ya Afrika mashariki... Wakenya wanataka tuharakishe kuingia katika federation, monetary union etc wakati wakati muafaka kufanya hivyo haujafikia, wanajua watafaidika na potential yetu....

Sanasana kinachowabeba wao ni SERVICE INDUSTRY tu, mambo ya huduma za usafiri wa ndege, fedha, IT etc ambayo ni lazima yabebwe na uwepo thabiti wa resources/comodities ambazo sisi tunazo zaidi ya Wakenya...

Tukiamua hakuna Mkenya anayeweza kuleta fyokofyoko. Natamani niendelee kuturirika ila ngoja niishie hapa kwa leo, hii kitu inastahili uzi wake mwingine!.....
 
Ujamaa ulikuwa na faida nyingi sana kuliko unavyofikiri wewe. Hata kiswahili ni lugha inayotuunganisha. Tatizo hapa ni watu kukosa uzalendo. Hasa nyie mnaoenda nje ya nchi hamkumbuki nyumbani.

Mi nadhani tatizo ni nyinyi wa nyumbani mnawapigia kura mafisadi
 
siasa ya ujamaa ukichanganya na joto la dar imechangia sana kuharibu akili zetu

Mkuu siasa ya ujamaa unaitafsiri vipi? Hakuna siasa ya ujamaa kwenye nchi ambayo viongozi wake, watu wake, ni wabinafsi wanajilimbikizia mali ambayo hawawezi kuimaliza katika life span yao, yaani ufisadi uliopitiliza.
Tusipoangalia tutaendelea kulaumu siasa ya ujamaa wakati mafisadi wanazidi kuneemeka.
 
Mbona kama manzese tu, mi nilifikiri flyover kumbe! Hata kama nchi yangu inaniuma sana lakini siwezi kutoa sifa za kijinga. Kwanza walipigana dr. Kikwete ndie alie wapatanisha. Wanajua kupigana tu lakini sio kupatana. Hata kofii alomide alishindwa kuwapatanisha.
kweli mkuu! hahahahahaha!
wana kila kitu ila wamekosa utu! ukabila utawamaliza...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom