Tatizo la Watanzania walio wengi ni wanafiki na mara zote wanachukua visingizio vilivyopitwa na wakati kuharalisha udhaifu wao. Kuanzia kwa Rais mstaafu Mwinyi yeye aliingia madarakani kwa kupora nafasi ya Salim Ahmed Salim akafikiri nchi ni kuongoza kama familia. Alikuta viwanda-basic industries vilivyokuwa vimejengwa na Mwalimu ili vizalishe bidhaa ya kutumika katika viwanda vingine. Akakuta viwanda vya nguo ambavyo kwavyom nchi nyingi ziliendelea. Sasa badala ya kuviboresha kwa nguvu zote na kuvilinda akafungua pandora box ya ajabu. Vidhaa hafifu ikashamiri soko letu kuanzia vijiti vy a kuchokonolea meno, nguo za mitumba, viatu vya kuendea kwenye sherehe uku unatembea unakilinda kiatu badala ya kukulinda wewe maana ukitembea kwa kishindo sole unaiacha hapohapo. Viwanda vyetu vya nguo ndio uliokuwa mwisho wake pamoja na viwanda vingine. Lakini kibaya zaidi ni kutokulipa kodi maana uchumi wetu unategemea sana mapato ya kodi. Serikali ya awamu ya pili ilikubali masharti toka mashirika ya fedha ya kimataifa moja ikiwa nikuacha kuwekeza kwenye elimu. Tulichovuna ni kushindwa kuwa na sustainable sucession system ya wataalamu. Vyuo vilivyokuwa vinawapika wataalamu kama Chuo cha TANESCO Morogoro, Bandari DSM, Posta na Simu Dar es Salaam, Chuo cha Maji na vingine vingi vikabaki maghofu ya kujifichia ngochiro, paka na nyoka.
Na alipoona hiyo haitoshi akaliua Azmio la Arusha na kuasisi Azmio la Zanzibar ambalo mpaka leo halikuwahi kuandikwa na yeye pamoja na viongozi waliofatia wanaona aibu kulitaja. Acha hayo yote wakati anaacha madaraka alituachia zigo la rada ya ndege ambapo kiasi cha pesa kilichalipwa, IPTL na madeni kibao ya nje na ndani, rushwa iliyokithiri, ubadhirifu wa mali ya umma, utoroshaji wa wanyama hai kwennye mbuga zetu na watu wasije wakasahau kuwa skendal ya twiga hai ya juzi ni jambo jipya na fragile social fabric ya mihadhara ya kashfa ya dini. Sijui wachambuzi watatausaidia legacy ya mzee Mwinyi ni dini katika nchi yetu.
Kingine alituachia kitu kibaya nacho ni intellectual dependence pale ambapo tunajiona hatuwezi kufanya chochote bila kuambiwa na wazungu. Tuna raslimali za kutosha lakini tunatembeza bakuri la ombaomba hata vitu vidogovidogo. Wenzetu wa Kenya wanajitegemea na raslimali za nchi zinatika koboresha uchumi. Uchumi wao unaadaliwa na Wakenya kakini sisi bajeti mpaka tuambiwe na watu wa nje kwa masharti ili wapate kuifinance. Kila jambo lina mwanzo na haya chanzo chake ni ruksa.
Marais waliomfatia wamerithi viatu vya ruksa. Rais Mkapa alijaribu kusahihisha ya makosa ya kushindwa kukusanya kodi. Akaunda mamlaka ya mapato japo ilikuwa ni maelekzo ya nchi wahisani lakini naye ameendeleza kaugnjwa ka riksa kwa kuwasujudu wageni kwa kigezo cha Foreign Direct Investment ambapo wawekezaji wa kigeni walikja wakachukua mashirika na mabenki kama njugu na wakasamehewa kodi zote. Na tax leave ikiisha wanabadilisha majina kwa kujifanya kampuni imenunuliwa na watu wengine ili waendelee kuenjoy tax holiday. Makampuni ya ya madini yanachukua madini yetu yalivyo bila auditing yoyote na kupelekwa nje tunabaki uambulia asilimia ya mrahaba. Ni aibu sana maana na hii inatoka na kile walichotangza kama faida ambapo hatuna uwezo kuaganlia vitabu vyao vya kihasibu kila siku. Tunaambulia kiduchu, tunaachiwa maandaki, uharibifu wa udongo, hewa, vyanzo vya maji mfano mto Tigeti. Ingawa Mkapa siye wa kwanza kuuza migodi ilianza na Mzee Mwinyi na MheshiwaKikwete akiwa waziri wa madini bado alikuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko lakini wapi.
Sasa mchezo wa kupokezana vijiti ukamkuta Rais Kikwete. Na yeye ameendeleza kile ambacho wenziwe walikiasisi-intellectual dependence. Hatuamini katika uwekezaji wa ndani bali wa kutoka nje na kusamehe kodi kwa wawekezaji hao. Kiasi kikubwa cha pesa kinaamishwa na wawekezaji hao kupitia faida, likizo, wataalamu toka nje na mengine. Lakini chini ya serikali hii safari za nje zimekuwa ni nyingi kwa kisingizio kuwa asiposafiri tutakula mchicha. Lakini hiyo mboga nzuri zaidi ya mchicha tumeshuhudia mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na huduma muhimu maana kwenye safari hizo tunaamisha fedha ya kigeni kupeleka huko nje.
Nchi zote duniani zimeendelea kwa kutumia elimu bora.Zimewekeza ktk elimu ya sayansi na ufundi. Chini ya serikali hii tumefanya vioja kwa kuanzisha sekondari kama uyoga za kata lakini tukazinyima walimu, vitabu, mahabara na maktaba. Wengine wanasema ni bomu la kulipuka, voda fasta, yebeyeba na majina kejeli mengi. Watawala wanazisifia lakini watoto wao nandugu zao wako ktk shule bora za ndani na nje ya nchi. Lakini wakineda kwa wafadhili wanawapa takwimu na wakipokea nishani wanakuja wanashangilia. Shule ambazo wanafunzi wanafika form IV hawajui kusoma na kuandika. Hawa ndio tunategemea waende vyuo vikuu tulivyovianzisha kwa fujo. Hivi ktk fragility hii utajenga flyovers? Kwa wizi na ubadhirifu unaofichuliwa kila uchao toka Buzwagi, Richmond, Meremeta,Loliondo, Utoroshaji wa twiga, kusamehe kodi, kuwepa kodi, kuua reli ya kati na Tazara na kuwapa waharabu tenda za kusafirisha bidhaa hata za umma utajenga uchumi imara wa kuwafaidi wananchi kama Kenya. Historia itasema