Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Unajua kitu kimoja ni kwamba kuna mambo na hisia ambayo yanakutambulisha wewe ni mtu wa namna gani. Kuna vitu ambavyo vitakutambulisha wewe kuwa mtu mstaarabu au mwenye roho mbaya ya kishetani sana.
Wewe ni mtu wa hivyo, mwenye roho mbaya ya kishetani?
- Kwa mfano, chukulia kibaka amekamatwa akijaribu kupora simu yako. Watu wenye hasira wanaamua kumchoma moto na anaungua akfa huku akilia kwa uchungu. Je utafurahia na kuchekelea? Ukifanya hivyo wewe una roho ya kishetani sana.
- Au, chukulia ulikuwa na mume au mke mkaachana kwa sababu hakuwa mwaminifu. Huko nje akaendelea na tabia yake na baadae unasikia ameambukizwa VVU. Utafurahia na kuchekelea kuwa amepatikana? Ukifanya hivyo wewe pia ni mtu mwenye roho mbaya ya kishetani.
- Sasa chukulia raisi wa nchi ambae humpendi na hukumpigia kura unasikia akiwa safarini ndege yake ilipata ajali ikaanguka na akapoteza maisha. Utafurahia kifo cha huyo raisi ambae sio wa chama chako, hukumchagua wala kumpenda? Basi wewe pia una roho mbaya ya kishetani sana
- Sasa, chukulia Lissu katika harakati zake za kuongoza Chadema, inafikia anawekwa rumande na kuwa mbali na familia yake na kunyimwa uhuru wa kuchanganyika na watu kwa muda wote huu, japo bado hajapatikana na hatia. Utafurahia labda kwa kuwa wewe ni wa cama tawala au chenye ushindani na Chadema? Basi wewe pia una roho mbaya ya kishetani sana.
Wewe ni mtu wa hivyo, mwenye roho mbaya ya kishetani?