😀😀😄😄 Huwa nadaka neno la mwisho alaf najichekesha chekesha nahamisha mada ni ngumu sana kujua kama nilikua sikusikilizi
ok
Umenena vyema mkuu safi sanaNi kukosa adabu na heshima tu. Unapoishi na mwenzako tambua vitu ambavyo hapendezwi navyo halafu jiwekee tu mkakati wa kuishi nae bila kumkera.
Utaona hata yeye ataanza kukuheshimisha pia. Na atafurahia uwepo wako ukiwa karibu yake
[emoji23][emoji23][emoji23] tunazidi kupata shuhuda, hebu endelea dada mkubwa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee unakosa amani ya maisha Yani usipopokea simu tu anakujia live na waraka masaa matatu had manne haachi kitu na wanajua kupanga Kwa mtiririko kweli wazee wa ngenga[emoji23][emoji23]
Usiombe mkutane bahatmbaya njiani iyo siku umemkera utasimama had utaamua kuchuchumaa [emoji23][emoji23][emoji23]
Huo ni utoto aisee na mapenzi ya chuo. Hicho kitu ni kero!Napenda kumsumbua mpenzi wangu nisipo msumbua yeye nikamsumbue nani ??
au nmekosea kuimba? 😂[emoji23]
😂😂😂Habarini.
Hivi umeshawahi kuishi na mtu msumbufu ambaye hana adabu?
Anaweza kuwa ni mkeo au mumeo huyu mtu. Mfano anaamka asubuhi alfajiri ya saa kumi na moja anawasha simu anaanza kucheka mwenyewe vitu anavyotazama mtandaoni.
Au anaamka anaanza kukuongelesha ongelesha story za kipuuzi ambazo hazina maana muda huo una usingizi mzito haupo kwenye mood ya kuongea hata na nafsi yako.
Au, unaweza kuwa unapenda utulivu yeye anaweka mziki wa sauti ya juu halafu anatoka nje anaacha mziki unakupigia wewe kelele hadi unabakia kujiuliza hivi huyu yupo sawa sawa kichwani kweli?!
Au mfano unakuta ni mwanaume anarudi kazini mna mtoto mdogo wa miezi mitatu kwa mfano. Mama umebembeleza mtoto amelala kasinzia mwanaume anafika anaanza kumbusu busu na kumuongelesha hadi mtoto anastuka halafu akianza kulia anamrudishia mama yake "eti mchukue analia". Matako yako ulimkuta analia,si umemuamsha na ufala fala wako hapo?[emoji34]
Wapo pia wanawake wasio na adabu kwa watoto tena mara nyingi ni zile sampuli za wanawake ambao wanakwenda kazini. Mtoto anabembelezwa na kulelewa na house girl yeye akija ni kumnyonyesha tu. Anakuta mtoto amelala anafika eti muamshe nimsalimie mtoto, wewe mtoto wa miezi sita au saba au mwaka unamuamsha ili umsalimie huyo mtoto anaongea huyo, kwan huwezi kuendelea na shughuli zingine mtoto alale apumzike akiamka utacheza nae wewe unamkatisha mtoto usingizi. Aisee hii kitu mimi huwa inanikera aiseee huwa natamani kumtusi mtu kabisa sababu sio adabu aisee.
Umetandika zako kitanda yeye anakuja analala anavuruga halafu anaamka anaenda jikoni anachukua chombo anatumia anaacha mezani. Anatoa juice, maziwa au maji kwenye friji halafu hayarudishi anaacha mezani. Au umefagia yeye anakuja anaingia na viatu as if haoni kuwa sakafu ni safi na haitakiwi kuingia na viatu.
Unakaa unatazama zako movie au upo zako Jamii Forum, mwanamke kazi kulazimisha kukuongelesha sababu kaona attention yako ipo kwenye simu au Tv. Mara ajipitishe pitishe hapo mbele yako halafu anakutazama,anakuongelesha story ambazo hazina kichwa wala miguu.
Ukimwambia akungojee kidogo umalizie unachofanya anakuwekea ile sura ya "haya baba samahani kwa kukusumbua".
Kwann watu huwa wanakuwa wasumbufu hivi aisee. Kimsingi kuna watu ni wasumbufu aiseee. Yaani wanakuwa ni kero kwa matendo yao.
😂😂😂😂🙌Huyo ni chaguo lako 🎶
msiwachoke wenzenu kisa vijitabia, hakuna alie mkamilifu😂😂😂😂🙌
hukuliona hilo mwanzo au ulitaka pasua kichwaKuna machaguo pasua kichwa
Hakika bromsiwachoke wenzenu kisa vijitabia, hakuna alie mkamilifu
Hahahahah poleni sana wazee 😀😀😀 ila kiukweli lililonigusa ni hilo la simu na jf. Nikiwa nimerudi home nimekaa tu hakuna story naamua nishike simu niperuzi hapo ndio story zinaanzishwa sasa. Usipozingatia story kelele yani we na hio simu huko jf wakupe mshahara sasa. 🤣 🤣 🤣 Watu hata hatuwezi ongea tukaskilizana.Yaani ni utumwa, nikitoka kazini eti niwe nanyata nisije muamsha mtoto, nikimkuta anacheza ni lazima nimbebe akinililia la sivyo huyo mtoto wa mwaka mmoja ataambiwa mambo kama mtu mzima...
"Unamlilia lialia babaako na wakati hupendwi"..
"Hebu baki hapo acha kiherehere huoni kama hupendwi"
"Baba fulani hebu mbebe mtoto huoni nipo busy".
yaani bora mtu ubakie huko job hadi usiku wamelala ndipo urudi nyumbani usiku
Hahahahah kweli mtu kukuongelesha ni kawaida.Kama mnapendana kweli hayo ni mambo madogo madogo ya kuongea na kurekebishana ama kuishi nayo tu kwa kuvumiliana, sasa unanuna mtu kukuongelesha ukimkuta anaongeleshana na jirani si utalia wewe
Unachat na malaya zako eeh 🤣dah hawa viumbe lakini. Mungu tupe ujasiri tu.wahenga walipomaliza kusema misemo yao na wahuni tukasema
"Mwanamke hakuchoshi akiwa Anaishi kwa Baba yake tu"
Maana anaweza kukukasirikia hata kwa kosa la wewe kuwa mstaarabu na kujishusha, ukikaa kimya utaskia "kwahiyo mi nakuongelesha we umenyamaza ila wanawake zako unawajibu"
Hahahah njoo nikuvuruge nywele kidogo maana sipendi mandari yake 😀😀😀Usiombe uwe unapenda vitu vikae kwenye mpangilio mzuri mandhari safi na tulivu halafu mwenzako awe mvurugaji na rafu. Aise inakera mno
Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app