Hivi umeshawahi kuishi na mpenzi msumbufu?

Hivi umeshawahi kuishi na mpenzi msumbufu?

Sasa wewe hiyo imekaa sawa kwako?! Mfano unamtoto ambae anasumbua sana kulala halafu umebembeleza amelala anakuja jamaa yako anamuamsha halafu hakai nae hata dakika kumi anakurudishia mtoto macho makavu amenza kulia tena na muda huo una kazi nyingine, wewe hiyo imekaa sawa?

Kwann asimuache mtoto alale amtazame tu kimya kimya asubirie akiamka atakaa nae acheze nae.
Hii ni kero sana. Mi mme wangu alikua na hizi mambo akija akikuta kitoto kimelala haridhiki mpaka akishike shike mashavu akisemeshe. Basi hapo mtoto akijigeuza mara mbili kashaamka. Utaskia njoo mnyonyeshe naishia tu kuvuta mdomo. Na kuna hii mtoto kila akilia anakuambia mnyonyeshe kwani muda wote mtoto anataka kunyonya tu. Ye akimbeleza kidogo tu "mchukue".
 
Hii ni kero sana. Mi mme wangu alikua na hizi mambo akija akikuta kitoto kimelala haridhiki mpaka akishike shike mashavu akisemeshe. Basi hapo mtoto akijigeuza mara mbili kashaamka. Utaskia njoo mnyonyeshe naishia tu kuvuta mdomo. Na kuna hii mtoto kila akilia anakuambia mnyonyeshe kwani muda wote mtoto anataka kunyonya tu. Ye akimbeleza kidogo tu "mchukue".
Ni huyo mimi 🤣
 
[emoji23][emoji23]Aisee unakosa amani ya maisha Yani usipopokea simu tu anakujia live na waraka masaa matatu had manne haachi kitu na wanajua kupanga Kwa mtiririko kweli wazee wa ngenga[emoji23][emoji23]

Usiombe mkutane bahatmbaya njiani iyo siku umemkera utasimama had utaamua kuchuchumaa [emoji23][emoji23][emoji23]
Mwanaume hapendezi kuwa muongeaji sana. Unasema kidogo halafu unaacha.
 
Hata we una vijitabia ambavyo watu wanakuvumilia na ili uishi na watu lazima ujue ku-blend in japo kwa kiasi fulani. Kila mtu anakuwa na malezi aliyopewa huko alikotoka cha muhimu ni kuelezana zile kero za mara kwa mara kwa utulivu atasikia.
Ungekuwa unanifahamu in person usingesema hayo maneno. Nipo very attentive na privacy yangu na privacy za wengine. Ni ngumu sana mimi tabia zangu kuwaathiri watu wengine na hata ikitokea huwa wanajua ni kutokufahamiana tu ndiko kumesababisha na haitajirudia.

Mimi naongelea zile kero za kujirudia yaani unakosea mtu anakwambia au anakuelekeza unajirekebisha kwa muda then unarudia tena unamtengenezea mazingira muhusika kuwa akukubali kwa namna ulivyo tu.
 
Aisee mtoto amelala yeye amuamshe amsalimie watoto ni wasumbufu akilala ndipo mama anapata muda wa kupumzika na kufanya shughuli zingine
Kuna watu wanaongea tu hapa ila hawana experience. Aiseee mtoto akiwa ndio wale ambao hawapendi kusumbuliwa wakilala na akiamka basi anataka bendi imuimbie "Go to sleep my sweet baby" ndipo alale, aisee utatamani ardhi ipasuke.
 
Yeah, niko hivyo mimi unaweza unifanyie jambo kubwa nikatafuta sababu za kujustify actions zako then nikaelewa, ila tuvitu tudogodogo huwa tunaniondoshea amani kabisa, na kama uzi uliotuunganisha ni mwembamba ndio inakuwa kwa heri.
Raia hawaelewi tu. Mtu unaweza kufeli mahusiano sababu unalala vibaya tu usiku mtu akakuona tatizo maana anajiuliza huyu mtu mimi ndio nakwenda kuoa au ndio mtu ataolewa nae halafu ana ulalaji wa hovyo hivi, mtu anageuka hovyo usiku unashangaa amekuwekea limguu la shingo, unatoa mara kidole cha jicho, mara haujakaaa sawa anakupumulia usoni kama dragon, bado anakoroma kama meza inasogezwa kwa kuburutwa.

Hapo mapema sana nasign out maana nitakuwa nateseka mimi wewe unalala usingizi mnono, aisee sitaki kero kitandani.
 
Napenda kumsumbua mpenzi wangu nisipo msumbua yeye nikamsumbue nani ??
Sio jambo zuri badala ya kutumia muda wenu kufanya mambo ya kupeana raha unamkera akikuchoka unasema shetani kafanya nini nini sijui kumbe ni wewe mwenyewe na kero zako.
 
Hiyo sector naiweza sana hata nikikutana na marafiki wanao ongea sana huwa naitikia bila kuelewa wameongea nini saa hiyo mawazo nimehamishia sehem nyingine, shida huwa inakuja pale anaponiuliza swali linalo hitaji jibu huwa nashindwa hata nijibu nini maana sijaelewa hata kimoja alichoongea
Tatizo anakuongelesha halafu utasikia anakuuliza , "mbona haunisikilizi?" Ukiwambia " nakusikiliza mbona endelea" utaskia , "Nilikuwa nasemaje au nimeongelea nini mara ya mwisho?"

Hizi Quiz mimi huwa sizipendi aisee.
 
Kuepuka yote hayo ishi tu peke yako, mbona simple!
Siwezi ishi pekee yangu wakati kuna Potential compatible spouses wapo huko nje, so ikibidi napiga chini anatafuta mwingine wa kublend nae.
 
Hii ya kuamsha mtoto wanawake karibia wote nadhan tena hujamuona siku nzima anaamshwa [emoji23][emoji23][emoji23] saa nyingine mtoto analala muda mrefu weee unapata wasiwasi unaona bora umuamshe tu
Aaaah mtoto muache alale bana. Ukitaka kucheza nae omba ruhusa kazini ushinde nae siku nzima.
 
Hakuna kitu kinakera kama kuweka simu mezani alafu 'wife' anachukua na kuanza kuperuzi kwenye meseji.
Hii tabia inakera sana. Anakufanya unakuwa na mashaka kama unapita airport na madawa.
 
Back
Top Bottom