Hivi umeshawahi kuishi na mpenzi msumbufu?

Hivi umeshawahi kuishi na mpenzi msumbufu?

Habarini.

Hivi umeshawahi kuishi na mtu msumbufu ambaye hana adabu?

Anaweza kuwa ni mkeo au mumeo huyu mtu. Mfano anaamka asubuhi alfajiri ya saa kumi na moja anawasha simu anaanza kucheka mwenyewe vitu anavyotazama mtandaoni.

Au anaamka anaanza kukuongelesha ongelesha story za kipuuzi ambazo hazina maana muda huo una usingizi mzito haupo kwenye mood ya kuongea hata na nafsi yako.

Au, unaweza kuwa unapenda utulivu yeye anaweka mziki wa sauti ya juu halafu anatoka nje anaacha mziki unakupigia wewe kelele hadi unabakia kujiuliza hivi huyu yupo sawa sawa kichwani kweli?!

Au mfano unakuta ni mwanaume anarudi kazini mna mtoto mdogo wa miezi mitatu kwa mfano. Mama umebembeleza mtoto amelala kasinzia mwanaume anafika anaanza kumbusu busu na kumuongelesha hadi mtoto anastuka halafu akianza kulia anamrudishia mama yake "eti mchukue analia". Matako yako ulimkuta analia,si umemuamsha na ufala fala wako hapo?[emoji34]

Wapo pia wanawake wasio na adabu kwa watoto tena mara nyingi ni zile sampuli za wanawake ambao wanakwenda kazini. Mtoto anabembelezwa na kulelewa na house girl yeye akija ni kumnyonyesha tu. Anakuta mtoto amelala anafika eti muamshe nimsalimie mtoto, wewe mtoto wa miezi sita au saba au mwaka unamuamsha ili umsalimie huyo mtoto anaongea huyo, kwan huwezi kuendelea na shughuli zingine mtoto alale apumzike akiamka utacheza nae wewe unamkatisha mtoto usingizi. Aisee hii kitu mimi huwa inanikera aiseee huwa natamani kumtusi mtu kabisa sababu sio adabu aisee.

Umetandika zako kitanda yeye anakuja analala anavuruga halafu anaamka anaenda jikoni anachukua chombo anatumia anaacha mezani. Anatoa juice, maziwa au maji kwenye friji halafu hayarudishi anaacha mezani. Au umefagia yeye anakuja anaingia na viatu as if haoni kuwa sakafu ni safi na haitakiwi kuingia na viatu.

Unakaa unatazama zako movie au upo zako Jamii Forum, mwanamke kazi kulazimisha kukuongelesha sababu kaona attention yako ipo kwenye simu au Tv. Mara ajipitishe pitishe hapo mbele yako halafu anakutazama,anakuongelesha story ambazo hazina kichwa wala miguu.

Ukimwambia akungojee kidogo umalizie unachofanya anakuwekea ile sura ya "haya baba samahani kwa kukusumbua".

Kwann watu huwa wanakuwa wasumbufu hivi aisee. Kimsingi kuna watu ni wasumbufu aiseee. Yaani wanakuwa ni kero kwa matendo yao.
Nikikutana na Binti mmoja mzuri mpambanaji hatari nikamuelewa na yy akanielewa shida ndo huo usumbufu, Yaani muda wa kulala anataka mpige story mkishazagamuana anataka story ataleta mazungumzo yasiyo rasmi na anataka umsikilize tofauti na hapo anadai humpendi mara ooh samahani ooh nimekukosea Nini unamweleza jamani tulale huu muda wakupunzika haelewi ooh umeshinda KAZINi Sasa ni muda wangu kuongeza na ww hata kama ni pointless jamani ! Nikaanza kuchelewa KAZINi na nikifika nakuwa na usingizi balaa naweza nikakaa kwenye kti usingizi ukamichukuwa Kwa sababu ya usumbufu wa huyo dada muda wa kulala ukifika ! Nikaamua kumpiga chini baada ya kusafiri kwenda msibani mkoa Fulani hivi Kila akidai nitumie nauli nikawa stumi ukifika usiku katapiga simu hata saa 8 usiku kuniongelesha aisee kalikuwa kanajua mapenzi lakini nilikablock Kwa sababu ya usumbufu!
 
Inabidi umchague mtu mnayeendana akili nje ya hapo utaona ndoa kuzimu.
Ni ngumu sasa babu. Kuna tabia zinakuja baadae baada ya kuzoeana. Mfano nitajuaje kama mwanamke ni mzembe kwenye eneo la mtoto kabla ya kuzaa nae.
 
[emoji4] na hapo ndipo binadamu tumetofautiana.
Mi sipendi nimelala mtu aje afungue mlango na awashe taa huwa nasikia kumtafuna.
Kingine asikilize video zake za kwenye simu kwa sauti inayonifikia.
You see. Hii ni exactly kero kwangu aisee. Au kuongea na simu mfano anaongea na shost yake au mama yake au dada yake sim ya masaa asiee nenda kakae hata sebuleni huko uongelee huko mimi sitaki kusikiliza mazungumzo yenu.

Au mtu anaingia chumbani mwenzako kalala unawasha taa. Aiseee hiyo kitu huwa inanikata balaa. Naweza nikakuchukia hata kama ni manzi nakuelewa.

Unatumia simu vaa earphones sikiliza upuuzi wako mwenyewe . Why sasa unaweka loudspeaker halafu unataka sote tusikilize.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]muhesabu visa,haliwezi penzi.
Mmmmmmhmn kwahiyo wewe uliyenae hana kero hata kidogo, au unadate na watoto wa wale malaika walio angushwa kutoka mbinguni?
 
Nikikutana na Binti mmoja mzuri mpambanaji hatari nikamuelewa na yy akanielewa shida ndo huo usumbufu, Yaani muda wa kulala anataka mpige story mkishazagamuana anataka story ataleta mazungumzo yasiyo rasmi na anataka umsikilize tofauti na hapo anadai humpendi mara ooh samahani ooh nimekukosea Nini unamweleza jamani tulale huu muda wakupunzika haelewi ooh umeshinda KAZINi Sasa ni muda wangu kuongeza na ww hata kama ni pointless jamani ! Nikaanza kuchelewa KAZINi na nikifika nakuwa na usingizi balaa naweza nikakaa kwenye kti usingizi ukamichukuwa Kwa sababu ya usumbufu wa huyo dada muda wa kulala ukifika ! Nikaamua kumpiga chini baada ya kusafiri kwenda msibani mkoa Fulani hivi Kila akidai nitumie nauli nikawa stumi ukifika usiku katapiga simu hata saa 8 usiku kuniongelesha aisee kalikuwa kanajua mapenzi lakini nilikablock Kwa sababu ya usumbufu!
Aisee usumbufu unakera sana. Hii tabia ya wanawake kuleta mazungumzo baada ya mwanaume kupiga bao na kumaliza mechi huwa hawajui namna inakera.

Ule muda huwa sitakagi kuongea na mtu yoyote nataka nipate utulivu wa kama nusu saa hivi nilale usingizi mzito then ndio niamke kuwa macho. Ndio maana mimi muda wangu wa kupiga mashine ni kuanzia saa mbili usiku kuendelea ili nikipiga show yangu ya saa kadhaa tukimaliza ni kulala hadi asubuhi safi kabisa.

Hizi show za asubuhi au mchana mimi huwa sipendi unless iwe hatuendi popote baada ya kupigana mashine.
 
Back
Top Bottom