Hivi umeshawahi kuishi na mpenzi msumbufu?

Hivi umeshawahi kuishi na mpenzi msumbufu?

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
10,999
Reaction score
23,528
Habarini.

Hivi umeshawahi kuishi na mtu msumbufu ambaye hana adabu?

Anaweza kuwa ni mkeo au mumeo huyu mtu. Mfano anaamka asubuhi alfajiri ya saa kumi na moja anawasha simu anaanza kucheka mwenyewe vitu anavyotazama mtandaoni.

Au anaamka anaanza kukuongelesha ongelesha story za kipuuzi ambazo hazina maana muda huo una usingizi mzito haupo kwenye mood ya kuongea hata na nafsi yako.

Au, unaweza kuwa unapenda utulivu yeye anaweka mziki wa sauti ya juu halafu anatoka nje anaacha mziki unakupigia wewe kelele hadi unabakia kujiuliza hivi huyu yupo sawa sawa kichwani kweli?!

Au mfano unakuta ni mwanaume anarudi kazini mna mtoto mdogo wa miezi mitatu kwa mfano. Mama umebembeleza mtoto amelala kasinzia mwanaume anafika anaanza kumbusu busu na kumuongelesha hadi mtoto anastuka halafu akianza kulia anamrudishia mama yake "eti mchukue analia". Matako yako ulimkuta analia,si umemuamsha na ufala fala wako hapo?[emoji34]

Wapo pia wanawake wasio na adabu kwa watoto tena mara nyingi ni zile sampuli za wanawake ambao wanakwenda kazini. Mtoto anabembelezwa na kulelewa na house girl yeye akija ni kumnyonyesha tu. Anakuta mtoto amelala anafika eti muamshe nimsalimie mtoto, wewe mtoto wa miezi sita au saba au mwaka unamuamsha ili umsalimie huyo mtoto anaongea huyo, kwan huwezi kuendelea na shughuli zingine mtoto alale apumzike akiamka utacheza nae wewe unamkatisha mtoto usingizi. Aisee hii kitu mimi huwa inanikera aiseee huwa natamani kumtusi mtu kabisa sababu sio adabu aisee.

Umetandika zako kitanda yeye anakuja analala anavuruga halafu anaamka anaenda jikoni anachukua chombo anatumia anaacha mezani. Anatoa juice, maziwa au maji kwenye friji halafu hayarudishi anaacha mezani. Au umefagia yeye anakuja anaingia na viatu as if haoni kuwa sakafu ni safi na haitakiwi kuingia na viatu.

Unakaa unatazama zako movie au upo zako Jamii Forum, mwanamke kazi kulazimisha kukuongelesha sababu kaona attention yako ipo kwenye simu au Tv. Mara ajipitishe pitishe hapo mbele yako halafu anakutazama,anakuongelesha story ambazo hazina kichwa wala miguu.

Ukimwambia akungojee kidogo umalizie unachofanya anakuwekea ile sura ya "haya baba samahani kwa kukusumbua".

Kwann watu huwa wanakuwa wasumbufu hivi aisee. Kimsingi kuna watu ni wasumbufu aiseee. Yaani wanakuwa ni kero kwa matendo yao.
 
Yaani ni utumwa, nikitoka kazini eti niwe nanyata nisije muamsha mtoto, nikimkuta anacheza ni lazima nimbebe akinililia la sivyo huyo mtoto wa mwaka mmoja ataambiwa mambo kama mtu mzima...

"Unamlilia lialia babaako na wakati hupendwi"..

"Hebu baki hapo acha kiherehere huoni kama hupendwi"

"Baba fulani hebu mbebe mtoto huoni nipo busy".


yaani bora mtu ubakie huko job hadi usiku wamelala ndipo urudi nyumbani usiku
 
Habarini.

Hivi umeshawahi kuishi na mtu msumbufu ambaye hana adabu?



Ukimwambia akungojee kidogo umalizie unachofanya anakuwekea ile sura ya "haya baba samahani kwa kukusumbua".

Kwann watu huwa wanakuwa wasumbufu hivi aisee. Kimsingi kuna watu ni wasumbufu aiseee. Yaani wanakuwa ni kero kwa matendo yao.
Ndoa Ni kuvumiliana Ni msalaba wako huo
 
Back
Top Bottom