mwanateknolojia
JF-Expert Member
- Nov 17, 2014
- 1,027
- 1,750
Aisee ni kweli mkuu, hata mimi nimegundua yafuatayo:
1.Watu wanakufa iwe kwa ugonjwa au ajali yote ni ili kupisha nafasi kwa viumbe vipya vinavyozaliwa.
2.Unapokuwa unatafta mchumba mwanzoni utaona kama wanapatikana kwa shida sana lakini siku ukimpata tu unaanza kuona ni kama wapo tele na kama mmeshapanga na kufunga ndoa basi kuna sauti flani inaanza kukuita ikisema umekosea kuchagua, muache ukamuoe flani!
3.Siku ukiwa na pesa mfukoni utaona ndani kama vile mmejaa kila kitu! Lakini ukipigika tu hata mswaki unafuta huuoni!
4.Ukiwa masikini au mtumishi wa cheo cha chini, utawaona matajiri au watumishi wa vyeo vikubwa kama ni watu wabinafsi na wasiojali wengine wenye kipato duni, lakini siku ukitajirika au kukwaa cheo cha juu, unaanza kuwaona wale wa chini kama ndio kero!