Hivi, uislamu uliwahi kuleta nini?

Hivi, uislamu uliwahi kuleta nini?

Neno swahili,ni neno la kiarabu,maana yake ni Pwani.Ushahidi tosha wa kuwa Kswahili(Sahili),ni lugha iliyoanzishwa na waarabu.
Kiswahili kilikuwepo, ila kimechukua maneno toka lugha zingine ikiwemo kiarabu, ni jambo la kawaida kwa lugha yoyote ile.
Mfano wako wa neno (Sahili) ni wa kitoto sana .

Nakufananisha na mwanafunzi wa Fizikia wa form one,

anayeanza na kujifunza definition ya physics ,

anayeshangaa KWANINI SHILINGI inazama BAHARINI, lakini meli inaelea ikiwa na mzigo wa makontena 1000 😅😅😅😅

Tuondolee UTOTO wako, a huu Mjadala upo nje ya upeo wako, nakushauri kachezee na watoto huko FACEBOOK.
 
Umejibu vizuri na wakumbuke kuna miji mikubwa ilizariwa kutokana na Uisilamu, kama vile Kilwa ikiwa na ustalabu wa kutosha,mfano Vasco dagama alipofika Kilwa aliikuta ni Inchi ikiwa na muundo wa utawala wa selikari pamoja na hera yake,yaani kulikuwa na ustarabu wa kutosha, na ilikuwa ikifanya biashara na inchi za mbali lakini walipokuja wazungu wenye wivu kama wewe mleta maada waliiangamiza ile miji ili kufuta historia zake waweze kutuletea huu ujinga ambao unaitwa demokrasia,
Wakati mjerumani anaivamia bara kutoka zanzibar aliwakuta kina Abushiri,Milambo,Mkwawa na wengine wakiwa wanajua kuandika na kusoma kwa lugha ya kiarabu na wamestarabika na huo ustarabu ulitokana na Uisilamu,ila walioandika histori yetu waliipotosha ili ioneka walikuta watu wajinga kama wewe mleta maada,
Zanzibar ilikuwa na kila kitu mpaka na ubalozi,Treni,Shule,Vyuo, Vitabu maghorofa, hiyo sababu ya Uisilamu,lakini hapo Mzizima Daresalam yalikuwa mapori yakiwa na simba,kumbuka Sultani ndiye aliyekuja kujenga Ikulu ya Daresalam hapo magogoni badaye sanaaa,
I
Hivyo vililetwa na Waarabu au Uislamu!? Je, majengo waliyojenga , ule ni Uislamu au tamaduni ya ujenzi ya Kiarabu!? Mimi naamini kuna upotoshaji hapo.
 
Ukizikiliza lugha Kidigo,Kisambaa,Kigiriama,Kibajuni,""Kichimbalazi" ambayo ni lugha ya Wabarawa Kizaramo nk. utagundua Kiswahili ni mchanganyiko wa hizo lugha na lugha za kigeni kama kiarabu na kihindi kiajemi kn.
 
Ali Sykes , Abdul Wahab Sykes walianzisha TAA wakamkaribisha Mwalimu Nyerere na kumpa kadi namba moja wao wakichukua namba mbili na tatu, hao ni waislam.

Huwezi kuuongelea uhuru wa Tanganyika bila ya kulitaja kundi kubwa la waislam wenyeji wa Mkoa wa Dar, kina Mshumi Kiyate. Mzee Tambaza, Kaluta Abeid na Hamza Aziz na wengine wengi.

Kuhoji waislam walifanya nini ni kuonyesha kutokuifahamu historia ya Tanganyika. Tatizo la utoto wa mleta mada.
Basi tuachane nacho haka katoto ka kigalatia
 
Kanisa lilihusika na Utumwa hiko West Africa sisi tunaongelea Pwani ya Afrika ya Mashariki.
Unaongeza urefu/upana wa magoli, kufit narrative yako...
Hao wassionari waliokuja hapa huku wakipeleleza na kutoa taarifa kwa ili wakolon waje kuvamia, walikuwa ni dini gani ?

 
Hebu nielekeze kwenye spika algebra inaingia wapi baada smaku na wire na box.

Au unaongelea spika za msikitini?
Hesabu zinapanda ?
Unajua maana ya algebra kwa upana zaidi? au ileile unayojua ya kujibia mitihani ?
Unaweza kujibu swali hilo hapo chini?
Na tuone kama hakuna aljebra itatumika hapo ???????

1743259705796.png
 
Uislamu Upo Karibia Miaka 1000 Pwani yetu na sehemu nyinginezo, hivi kipi haswa kimeletwa na uislamu kwa maana ya civilization na maendeleo ya jamii?

Hata tu mazao labda kuna zao gani ambalo lililetwa na uiaslamu hapa kwetu?
Kuna watu wanapenda chokochoko
Uislamu Upo Karibia Miaka 1000 Pwani yetu na sehemu nyinginezo, hivi kipi haswa kimeletwa na uislamu kwa maana ya civilization na maendeleo ya jamii?

Hata tu mazao labda kuna zao gani ambalo lililetwa na uiaslamu hapa kwetu?
Uislam Umeleta warabu ili tuwatumikie tena kwa mara ya pili. 😛
 
Hesabu zinapanda ?
Unajua maana ya algebra kwa upana zaidi? au ileile unayojua ya kujibia mitihani ?
Unaweza kujibu swali hilo hapo chini?
Na tuone kama hakuna aljebra itatumika hapo ???????

View attachment 3287061
Algebra haitumiki kwa kila kitu Mapiramidi ya Misri ya kale yalijengwa bila "Aljebra".
 
Uislamu Upo Karibia Miaka 1000 Pwani yetu na sehemu nyinginezo, hivi kipi haswa kimeletwa na uislamu kwa maana ya civilization na maendeleo ya jamii?

Hata tu mazao labda kuna zao gani ambalo lililetwa na uiaslamu hapa kwetu?
Ulileta Tende na Halua
 
Dr.David Livingston alikuwa ni Mmisionari wa Kikristo na ndiye aliyeloby serikali ya Uingereza ipige Stop biashara ya utumwa katika Bahari ya Hindi na Afrika ya Mashariki.
Soma wewe kuondoa kichocho kichwani mwako,unaandika kama umekunywa mataptapu
 
Mimi ni atheist mtu nisiyeamini katika dini wala Mungu.

Na kwa sababu hii, labda ninaweza kuwa mtu mzuri sana wa kujibu swali hili bila kasumba ya kutetea dini.

Uislamu umeleta mengi mazuri na mabaya, lakini moja kubwa zuri Uislamu umeleta utamaduni wa kusoma na kuandika.

Kuna watu wengi wa Afrika Mashariki walijua kusoma na kuandika kwa kupitia Uislamu. Watu walifikia muda mpaka kuandika Kiswahili kwa maandishi ya Kiarabu.

Hivyo, kujibu swali lako, Uislamu ulileta utamaduni wa kusoma na kuandika huku kwetu ambako hatukuwa na utamaduni wa maandishi.
Mabaya hujataja mbona?? Hahaha 😂 😂 😂 😂 naanza la kwanza ugaidi
 
Back
Top Bottom