Hivi TANESCO hawawezi kuunda app ya kununua umeme na kuingiza?

Wazo zuri mkuu, hakika kwa wale wataalamu wa Programming, wazee wa code wanaweza wakafanya kitu hapa

Hakika mkuu umetoa mawazo Chanya
 
Ununue na kuingiza kupitia simu, hutu tududu twao twa kuingizia umeme huwa tunanikera sana. Inawezekana?
Mi naona hamna sababu ya kuunda app, wanachotakiwa kufanya ni kuwezesha ukinunua umeme iwe kwa simu, banki au wakala, umeme wako uingie moja kwa moja kwenye mita yako na siyo kwenda kubinya binya unaingiza namba za luku kwenye mita
 
Shida yao hawatakagi kuunda mifumo yao wanategemea sana third parties. Hii inapelekea zoezi la integration kuwa gumu. Huwezi kuwa na taasisi inayoendelea kama utakuwa wa aina hii:

1. Mfumo wa HR unanunua kwa ABC COMPANY
2. Mfumo wa uhasibu unanunua kwa JD COMPANY
3. Mfumo wa billing za wateja unanunua kwa HK ENTERPRISES
4. Mfumo wa kudhibiti power cuts unanunua kwa XYZ INC
5. ETC

Huu mfumo wa manunuzi kutumia luku nadhani wanatumia wa maxcom na ku intergrate huo na mfumo wa billing na power use control wanayoitumia nadhani ni zoezi pana sana linawashinda kwa sasa.

Ukija kuambiwa ufanye integration ya hiyo mifumo ili iweze kupokelezana inakuwa issue.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Hii ingekuwa poa zaidi.
 
kazi sana, kwa hiyo meter zote ziwe na line ya simu
 
Laini ya simu ya nini wakati tayari kuna waya wa umeme? Wanaweza tumia same cables kupeleka signals pale mtu anapokuwa amelipia. Cha msingi ile meter iwe na backup power kama ni betri ambayo umeme ukiwepo inajichaji. Ukikatika inaweza kupokea signals from servers na ikaconnect ama kudisconnect umeme.

Saivi ilivyo ni kwamba meter ina module ya kucount down matumizi yakifika zero inakata umeme. Hii ni client side module ambayo hardware na software za kuregulate umeme znakuwa kwenye box moja ya meter. Wanaweza tumia same technology ikawekwa ya server side module ambapo server ndio ikawa inatunza data na kupeleka signals za kukata ama kurudisha umeme.

Sijui upande wa intergration na maxmalipo ndio labda inaweza kuwa hawajaweza kutafuta namna ya kuiweka sawa.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Shida yao hawatakagi kuunda mifumo yao wanategemea sana third parties. Hii inapelekea zoezi la integration kuwa gumu. Huwezi kuwa na taasisi inayoendelea kama utakuwa wa aina hii:

1. Mfumo wa HR unanunua kwa ABC COMPANY
2. Mfumo wa uhasibu unanunua kwa JD COMPANY
3. Mfumo wa billing za wateja unanunua kwa HK ENTERPRISES
4. Mfumo wa kudhibiti power cuts unanunua kwa XYZ INC
5. ETC

Huu mfumo wa manunuzi kutumia luku nadhani wanatumia wa maxcom na ku intergrate huo na mfumo wa billing na power use control wanayoitumia nadhani ni zoezi pana sana linawashinda kwa sasa.

Ukija kuambiwa ufanye integration ya hiyo mifumo ili iweze kupokelezana inakuwa issue.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
UDSM wana project pale COICT inashughulika na hili. Members wapo humu, wajibu hii ngwalangwala
 
Laini ya simu ya nini wakati tayari kuna waya wa umeme? Wanaweza tumia same cables kupeleka signals pale mtu anapokuwa amelipia. Cha msingi ile meter iwe na backup power kama ni betri ambayo umeme ukiwepo inajichaji. Ukikatika inaweza kupokea signals from servers na ikaconnect ama kudisconnect umeme.

Saivi ilivyo ni kwamba meter ina module ya kucount down matumizi yakifika zero inakata umeme. Hii ni client side module ambayo hardware na software za kuregulate umeme znakuwa kwenye box moja ya meter. Wanaweza tumia same technology ikawekwa ya server side module ambapo server ndio ikawa inatunza data na kupeleka signals za kukata ama kurudisha umeme.

Sijui upande wa intergration na maxmalipo ndio labda unaweza kuwa hawajaweza tafuta namna ya kuuweka sawa.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

Yani unataka waya wa power ubebe signal?? signal gani inayoweza safiri abt 2Kms??

Af iyo signal inaenda wapi?? maana source ya wire ni kwenye transformer ya LV. af signal ikifika pale nn kinafuata??

Simply unachosema ni kigumu sana. current kuna mita za EDMI ambazo zinatumia simcard ila sio LUKU ni postpaid Mita inarecord uses na kutuma taarifa kwenye kwenye serves so hakuna haja ya meter readers. So ni suala la kuweka relays ambazo zitakuwa zinapokea command kwa njia ya GSM/ GPRS kuwasha na kuzima

Japo sio njia poa italeta usumbufu. just imagine kuwa na servers za kuhandle two way communication kwa mita zoto TZ

Simply ni ngumu
 
Ofcourse kila kile ambacho watanzania hatukijui huwa tunasema ni kigumu sana. But wenzetu nje wanafanya sana tu. Both wired and wireless zinawezekana kabisa.

Skuizi hadi kuna simu mawasiliano yanapitia kwenye waya hizo hizo za umeme (Jose Soares Augusto's answer to Can communication signal be transmitted through a power cable? - Quora).

Cha msingi ni kuwa na kifaa cha kumodulate kwenye transformer tu.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Hata hivyo mengine tuyavumilie tu mana hadi sasa hata marekani kuna smart meters na old school meters.

Smart meters ukinunua tu inawaka. Old school meter ukinunua mpaka ukabofye bofye kwenye meter. Asilimia kubwa ya wamarekani bado wanatumia old school meters. So sio sie tu bongo.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mi naona hamna sababu ya kuunda app, wanachotakiwa kufanya ni kuwezesha ukinunua umeme iwe kwa simu, banki au wakala, umeme wako uingie moja kwa moja kwenye mita yako na siyo kwenda kubinya binya unaingiza namba za luku kwenye mita
Mita ikija kufeli?
 
Back
Top Bottom