Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 5,707
- 11,956
Kiukweli shirika takataka lisilo na faida kwasasa tukiachana na TTCL basi ni Tanesco. Hakuna na wala binafsi sioni faida ya hili shirika ambalo linaendeshwa kipigaji kuendelea kuwapo huku likisababisha hasara na usumbufu kwa watanzania as if tunapewa umeme bure.
Hivi inafaida gani kwa miezi 5 mfululizo kuwa na mgao usiokwisha kwa kisingizio cha matengenezo yasiyoeleweka na yasiyoisha.
Hatukatai kwamba maswala ya umeme huhitaji marekebisho ya mara kwa mara ili kuboresha huduma ya usambazaji wa umeme ila kwa kinachoendelea sidhani kama ni ajenda ya matengenezo bali ni uhujumu uchumi.
Kama tunakubali kucheka na huu uendeshaji wa kimasihara wa shirika nyeti la nishati ya umeme, uendeshaji wa masihara wa uingizwaji wa nishati ya mafuta, then tujiandae kama taifa kushuka kiuchumi kadiri siku zikienda.
Kwann TANESCO wasiwekwe benchi tu ili wabia wengine wa nishati waingie tupate umeme kwa bei ya chini na umeme wa uhakika kuliko hivi sasa umeme unakatwa kila dakika bila hoja za msingi wala ratiba ya kueleweka, halafu tunacheka nao.
Aiseee hii kitu inakera sana. Pale Tabata umeme kila siku kuanzia majira ya asubuhi huwa haueleweki unakatwa kwasababu gani. Na ukikatwa hiyo asubuhi basi unarejeshwa kama sio kuanzia saa moja jioni basi saa mbili hadi saa tatu ya usiku.
Sasa hayo ni maisha gani aisee.
TANESCO ifutwe haina maana kwasasa, ifutwe tenda wapewe watu binafsi.