Hivi Rais Samia yuko serious kweli katika kuunda Kamati Maalumu ya Corona? Mbona haoneshi mfano wa kutilia maanani ugonjwa huu?

Sio mbaya
Maana wataleta muongozo mpya nini serikali inatakiwa kufanya
Mkuu halafu kingine
Kumbuka mwendazake alikua hataki mambo ya korona yatajwetajwe
Sasa isingekua vyema huyu kaingia mpya na kuanza kuhimiza watu kuvaa barakoa
Ingeonekana walikua wanatofautina na mwendazake hivyo ingeleta picha mbaya
Hmm....na cha ajabu tokea jamaa afe, nyuzi za tanzia humu JF nazo ni kama zimeisha!

Watu hawafi tena kwa matatizo ya upumuaji!

Curious...
 
Simuelewi Mama, umri 60s. Mtu katoka Kenya huko kwenye 3rd wave. Ni hatari sana, tunaweza hata kutegeshewa mtu ana Covid akaja kwa Mama yetu.

Mkuu,Wanawake hawafi Sana na COVID19,Labda atakuwa anajivunia hili🤔🤔🤔🤔
 
Yes, mpaka kamati atakayounda ije na mapendekezo ya kuvaa barakoa ndio ataanza kuzivaa, rilaxx, at the moment still no Corona in Tanzania.
 
Simuelewi Mama, umri 60s. Mtu katoka Kenya huko kwenye 3rd wave. Ni hatari sana, tunaweza hata kutegeshewa mtu ana Covid akaja kwa Mama yetu.

Kabisa Mkuu...
Kenye wana 3rd wave...
Salam gani wakati walikuja Dodoma?
Isijekuwa Wanamletea Mama Magonjwa Aiseee Mi wakenya Siwaamini Kabisa!
Magu alipokuwepo walikuwa hata Mguu hawasogezi!
Nimeona Sijui Kashika Bahasha!ujumbe...
YaanibSijui kwanini Nimekuunga Mkono mkuu kwa mawazo yako!
Mama angejifanya Kabda yuko tighty ili Huyo Mama aonane na Mwingine...
Walivyokuwa wajanja wakenya Wakamtumia Mwanamke mwenzake ndo aje!
MUNGU atusaidie...
Kipindi Hiki hakuna Kumwammini mtuu!angepokelewa na Ummy tuu!
Then wakachukua Tahadhari zote kabla!
Anyway inawezekana tumewaza sivyo lakini Mawazo huru hujenga!
 
Japo hatuwezi kusema corona imeisha nchini lakini kwa dalili nizionazo mtaani na hospitalini hapa nilipo naona kama peak ya corona imepita.

Lakini tujiulize kwa nini huko Ulaya na Marekani wanakochanja watu cases mpya haziishi? Juzi nilicheki Marekani cases mpya zilikuwa 50 thousands na ushee lakini jana zimeongezeka zaidi ya hapo. Vifo navyo vivyo hivyo. Nachelea kusema kwamba huu ugonjwa bado sana "kujulikana".
 
Nadhani siasa na biashara zimezunguka huu ugonjwa.
 
Rais wetu huyu mpya majuzi katangaza kuwa ataunda sijui kamati ya Corona!

Bado sijaelewa hasa lengo na madhumuni ya hiyo kamati yatakuwa ni yepi.

Sasa ni zaidi ya mwaka na ushee tokea dunia ikumbwe na hili janga.

Kwa jinsi mwelekeo wa hali unavyoonekana, janga hili ni kama vile linaelekea elekea ukingoni sasa hususan baada ya upatikanaji wa ‘chanjo’.

Licha ya hivyo, nadhani kwa sasa nitakuwa sawa nikisema kuwa ‘tunajua’ kiasi cha kutosha kuhusu ugonjwa huo.

Sasa, kama kweli Rais Samia ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya corona, kwa nini mpaka sasa walau haonyeshi mfano kuwa kweli anautilia maanani ugonjwa huo kwa kuzingatia hata zile tahadhari zilizo za msingi kama kuvaa barakoa na kukaa ama kusimama mbalimbali na watu?

Leo kampokea waziri Amina Mohammed kutoka Kenya aliyekuwa katumwa na Rais Kenyatta.

Bi. Amina kaingia ikulu ya Dar akiwa amevaa barakoa. Samia yeye hakuwa kavaa.

Waziri Mulamula naye mwanzoni alionekana kavaa.

Baadaye wote walipokuwa wanaongea na waandishi wa habari, wote wakaonekana hawajazivaa.

Hivi ni kweli Rais Samia yupo serious au alikuwa anaongea tu siku ile ili kuridhisha baadhi ya watu kwa maneno tu lakini hakuwa na nia ya dhati kuonyesha kimatendo kuwa anamaanisha anachokisema?

Yeye kama raia namba moja si ndo anapaswa kuonyesha mfano wa kimatendo, au nakosea?

Au Watanzania walio wengi hawana muda na matendo bali wanapenda tu kusikia maneno yawapendezayo masikioni mwao?

Kujikinga na Covid-19/Covid-21 si kwa barakoa peke yake...
Zingatia social distance, kutokushikana mikono, kukwepa misongamano na kunawa mikono mara kwa mara.
Barakoa ni njia mojawapo tu... Na utafiti unaonesha wavaaji wengi wa barakoa hawazingatii matumizi yake ikiwemo kupuuzia tahadhari nyinginezo!
Itoshe kusema kuwa Covid-19 au Covid-21 ni ugonjwa wa mapafu kama mafua unajikuta tu unao haijalishi umevaa barakoa au hujavaa!
Wenye underlying health conditions wajihadhari zaidi!

#Tuzingatie usafi!
#Tuzingatie ventilation
#Tukwepe misongamano isiyo lazima
 
Sawa.

Hujaona kama Amina na Samia wamepeana bahasha with their bare hands?

Kulikuwa na social distancing hapo?
 
Back
Top Bottom