Hivi Rais Samia yuko serious kweli katika kuunda Kamati Maalumu ya Corona? Mbona haoneshi mfano wa kutilia maanani ugonjwa huu?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,231
113,609
Rais wetu huyu mpya majuzi katangaza kuwa ataunda sijui kamati ya Corona. Bado sijaelewa hasa lengo na madhumuni ya hiyo kamati yatakuwa ni yepi. Sasa ni zaidi ya mwaka na ushee tokea dunia ikumbwe na hili janga.

Kwa jinsi mwelekeo wa hali unavyoonekana, janga hili ni kama vile linaelekea elekea ukingoni sasa hususan baada ya upatikanaji wa ‘chanjo’.

Licha ya hivyo, nadhani kwa sasa nitakuwa sawa nikisema kuwa ‘tunajua’ kiasi cha kutosha kuhusu ugonjwa huo.

Sasa, kama kweli Rais Samia ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya corona, kwa nini mpaka sasa walau haonyeshi mfano kuwa kweli anautilia maanani ugonjwa huo kwa kuzingatia hata zile tahadhari zilizo za msingi kama kuvaa barakoa na kukaa ama kusimama mbalimbali na watu?

Leo kampokea waziri Amina Mohammed kutoka Kenya aliyekuwa katumwa na Rais Kenyatta. Bi. Amina kaingia ikulu ya Dar akiwa amevaa barakoa. Samia yeye hakuwa kavaa.

Waziri Mulamula naye mwanzoni alionekana kavaa. Baadaye wote walipokuwa wanaongea na waandishi wa habari, wote wakaonekana hawajazivaa.

Hivi ni kweli Rais Samia yupo serious au alikuwa anaongea tu siku ile ili kuridhisha baadhi ya watu kwa maneno tu lakini hakuwa na nia ya dhati kuonyesha kimatendo kuwa anamaanisha anachokisema?

Yeye kama raia namba moja si ndo anapaswa kuonyesha mfano wa kimatendo, au nakosea? Au Watanzania walio wengi hawana muda na matendo bali wanapenda tu kusikia maneno yawapendezayo masikioni mwao?
 
32FC0EEB-0473-4CAD-8134-B09E2338616E.jpeg
 
Au Watanzania walio wengi hawana muda na matendo bali wanapenda tu kusikia maneno yawapendezayo masikioni mwao?
Kweli kabisa.

Watanzania wengi wanapenda kusikia maneno yawapendezayo bila kupima ukweli wake.

Ni kama mwendazake alivyokuwa akitutangazia sisi ni matajiri dona kantri na miradi yote tunaitekeleza kwa fedha zetu za ndani.

Mataga wakawa wanamshangilia kwa nguvu zote wakitaka aongezewe muda atawale milele.

Bila ya kupima ukweli wa maneno ya mwendazake.

Hao ndo watanzania.
 
Yaani bado hajaamua chochote mpaka hio kamati itakapoundwa na kuleta mapendekezo kwa rais.

Nadhani hio ndio kitu anasubiri.

Kwa hio tusimseme kwa sasa maana bado mapema sana!
 
Hizo cable za umeme kwenye background ya picha zimeharibu unadhifu wa ikulu, hakukua na namna ya kuzificha?

P.S.

Nionavyo mimi Rais anataka kufanya maamuzi sasa kuhusiana na jambo hilo kwa kutegemea ripoti za kitaalam ili kujiweka katika usalama zaidi , kwamba critics wakose cha kulaumu kwani basis ya decision itakua imetokana na matokeo ya mawazo ya wataalam.
 
Nina hoja tatu juu ya hiki ulichoandika:

1. Lengo lako ni kutaka kuonesha kwamba Rais anapovaa hatakiwi kuivua? Kama ni hivyo huoni kwamba atakuwa anaonesha mfano mbaya kwa watoto ambao wataamini hawatakiwi kuvua hata kama itawaletea tatizo katika kupumua?

2. Je, unataka Rais aoneshe kweli Corona ipo na kamati itakayoundwa ije na majibu kwamba Corona ipo hata kama hakuna?

3. Je, ni wapi Rais alipowahi kusema watu lazima wavae barakoa kujikinga na Corona mpaka ionekane kutokuvaa kwake ni kwenda kinyume na agizo lake mwenyewe?
 
Rais wetu huyu mpya majuzi katangaza kuwa ataunda sijui kamati ya Corona!

Bado sijaelewa hasa lengo na madhumuni ya hiyo kamati yatakuwa ni yepi...
Sasa anavaaje Barakoa wakati Tanzania Corona hakuna.

Io kamati ikimwambia kuna Corona ndio Atavaa.
 
Yaani bado hajaamua chochote mpaka hio kamati itakapoundwa na kuleta mapendekezo kwa rais
Nadhani hio ndio kitu anasubiri
Kwa hio tusimseme kwa sasa maana bado mapema sana!
Mpaka kamati iseme vaeni barakoa ndo naye ataanza kuvaa?

Aisee!!!
 
Ngoja aendelee kuibipu, halafu tuje tuambiwe Mama yuko Nairobi Hospital kupitia kwa Kigogo 14

Huyo Amina keshachanjwa anaogopa kuambiwa kuwa yeye ndie kamletea Mama mzigo wa Mauti ndo maana kavaa barakoa.
 
Mpaka kamati iseme vaeni barakoa ndo naye ataanza kuvaa?

Aisee!!!
Sio mbaya
Maana wataleta muongozo mpya nini serikali inatakiwa kufanya
Mkuu halafu kingine
Kumbuka mwendazake alikua hataki mambo ya korona yatajwetajwe
Sasa isingekua vyema huyu kaingia mpya na kuanza kuhimiza watu kuvaa barakoa
Ingeonekana walikua wanatofautina na mwendazake hivyo ingeleta picha mbaya
 
Back
Top Bottom