Hivi pesa inapatikana wapi?


Kama vitabu havikusaidii wewe kichwa ngumu basi vimemsaidia mwingine.
 
Kama vitabu havikusaidii wewe kichwa ngumu basi vinamsaidia mwingine.
 
Nimeenda migodini nimepiga veni na kanyero za kutosha sijapata pesa

Nimeingia porini kata miti na mbao sikupata pesa

Nimesoma hadi chuo pia olaa

Biashara ya uwakala, mitumba, viatu, viwanja, nyumba kote sijapata pesa

Oya pesa inapatina wapi mazee
Mkuu kuna utajiri wa punje za mahindi njoo dm na laki 5 tu mkuu
Utanishukuru πŸ€—
 
Inategemea kwakweli mtu na mtu mi nimesoma vichache hivo hivo vichache vimenipa maarifa ambayo sikua nayo na nimeviapply baadhi ya sehemu naona matokeo...... Ngekua msomaji konki bila shaka ngekua na mengi kichwani
Sawa huenda kila mtu na akili yake, mimi ni mmoja wa watu wenye IQ kubwa tu na nimekuwa katika mazingira mazuri sana lakini siri za mafanikio nimezishuhudia kwa watu wasio na uwezo wa akili au kusomasoma sana, ndio maana nikahitimisha na hilo neno langu.

Utajiri wa pesa nyingi ni nje ya kile unachofikiria wewe yaani naweza kusema wenye hiyo bahati ni wachache sana.
 
Sipo hapa kubishana na mtu, kibongobongo hela nyingi za ukwasi huzikuti kama umetokea familia masikini hakuna mwenye gari au nyumba za kurithi bila kujiongeza...

Yawezekana umenizidi kiumri ila mimi toka nikiwa mdogo nimefatilia sana hiyo mifumo ni aidha uzaliwe kwenye utajiri au uwe na bahati ya kupata pesa kwa mkupuo kama Marley Dollars alivyopata mtipweshi ya msumbiji bila hivyo ni kudunduliza mpaka unakufa hautakuwa na maajabu yoyote ya kumtisha mtu hapa bongoland... Evelyn Salt
 
Hapa mleta mada anazungumzia pesa za kutikisa jamiii yaani unaita wanakijiji kuwasaidia unawagawia pesa na bado zinabaki wenye hiyo jeuri ni wachache sana hapa Tanzania..

Nimekaa na watu wa hivyo akiwemo Marley Dollars na amefanya jeuri kama hizo na bado hela anazo na anasumbua sana toka azipate ni zaidi ya miaka 15, hapa hatuzungumzii hela za kula, kununua ist sijui toyota nadia na kusomesha watoto st kunani naomba unielewe.
Evelyn Salt
 
Bora umwambie mkuu sasa yeye si kavisoma atupe tu chimbo sisi tukavune pesa
Halafu dogo ananiita mimi kichwa kigumu wakati hanijui simjui, huku mtandaoni watu tunachukuliana poa tu lakini tukisema tuweke siku ya kukutana kuna watu wataomba msamaha kama sio kutukimbia maana hawataamini watu watakao kutana nao! πŸ˜‚πŸ˜
 
Mkuu hutaki ujinga yanπŸ˜‚
Motivation speakers ni wengi mkuu hawatoi code wapi pesa wanachota humu kuna maboss kiongozi ni vile tu hawataki kutoa miongozo
 
Hivi wanaojibu hapa nataka kufahamu wao wanahizo pesa ama na wenyewe wanazitafuta maana watu wanaandika mara zimejificha kwenye shida za watu mara matatizo ila nafanyaje sasaa?
Wengi wana pesa za madafu milion 20 au 50 za bongo kushuka chini
 
Mkuu kuna ambao washapitia hizo stage zote wakazipata watuelekeze the final stage sisi tukachukue acheni ubinafsi
 
Mkuu kuna utajiri wa punje za mahindi njoo dm na laki 5 tu mkuu
Utanishukuru πŸ€—
Sina pesa ndio maana nataka unipe muongozo wapi nitapata pesa nyingi zaidi ya hiyo laki tano

Mkuu kuwa serious vijana tunasubiri code fungueni code jinsi mlivyopata ukwasi wenu nasisi tufuate miongozo
 
Mkuu wewe umeelewa vyema wachangiaji hawataki kutoa code ni wabinafsi
 
Mkuu nakubali argument zako ila ungefanya mpango wa code namimi nishike mapesa maana unaonekana ushatoboa unajua hazina ilipo
 
Aaaaah sa pesa za hivyo si aende huko kwa wazee wa kikinga mbona hata hapa jf atatugawia
 
Sina pesa ndio maana nataka unipe muongozo wapi nitapata pesa nyingi zaidi ya hiyo laki tano

Mkuu kuwa serious vijana tunasubiri code fungueni code jinsi mlivyopata ukwasi wenu nasisi tufuate miongozo
Mimi nilizamia nikaenda "uruthi" kufika huko "uruthi" nikawa nakwangua saruji kwenye nyumba za watu basi ndo nikatajirikia hapo makutupora Monetary doctor Intelligent businessman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…