Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,054
71,337
Mimi banaa, nmekulia kwenye huu ustaharabu wa Kila mtu na Sahani yake.

Lakini napo ilikua inanibidi kumwambia mwanandugu tuchanganye Msosi tule fasta fasta , sio kwamba lengo lilikua nikumpiga KO kama ambavyo wengi wasomaji mwaweza kudhania, la Hasha, lengo ilikuaga ni Ili tuwahi kumaliza Chakula ,Kuna wakati nilikua naamua kumuachia mtu Chakula. Ipo hivi, sipendi kutumia muda mwingi wakati wa Kula yaan najihisi

Napoteza muda, kile kipindi cha ukuaji na usomaji wa shule, nilikua namambo mengi mnoo, mpiraa, kucheza na watoto wenzangu, Kusoma, yaaan Kuna wakati nilikua hata Naskip Msosi, tabia ya kuskip Msosi hata Leo ninayo, yaan ikitokea tuu Nina Ubize mwingi au Nina jambo ambalo linahitaji utulivu wa akili, niwe kazin au Nyumban, aiseee kama Nimeamka nalo Asubuhi , basi ni mpaka nitakapolimaliza vizuri ndio Sasa nikumbuke kula, hapo chai sijanywa, cha mchana sijala.

Kipindi nasoma Sekondari na Hadi Chuo, nilikua kama Nina kazi za kitaaluma, aiseeee Chakula kinakua nje kwanza ya ratiba zangu , ni mpaka nimalize kazi hizo na tena Kwa Njaa Ile, ndio nilikua nikizifanya Kwa umakini sana na vinakaa kichwan sana...Nikija kwenye kula, basi nakula chapuchapu, niwahi kumaliza nifanye mambo mengine!

Mimi naweza kula Nimesimama yaan ilimradi tu nikimbizane na kitu fulani.

Nashukuru Wife wangu ananijua, maana tulitoka naye mbali, ila hata yeye Kila siku lazima nimuache mezani , yeye anajilisha taraaaaatibuuuu. Mimi siwezi.

Sasa Bwana nikiwa ugenini kasheshee bin kasheshee, yaani hapo ili nitumie muda mrefu, inanibidi Nile huku napiga stori vyauongo na kweli. Nile huku natumbua macho kwenye TV na Kujifanya fanya Sina taimu na Msosi kumbe hapo unakuta nazuga tu na nataman muondoke Mara Moja ,Nile chap ,mrudi nikute nimamaliza🤣🤣

👉Sijihisi kushiba. Ebwana eeehhh nikila taratibu taratibu nakua Sijihisi kushiba, yaaan najihisi tumbo langu halipokei kitu kabisaa, Kooo halipitishi kitu kabisaa, na ikitokea Ivo kwenye mazingira Fulani. Basi nitafanya namna niende Mahali nikapige Msosi upya!

Ile tunasema tafuna Chakula kwanza kiwe lojolojo ndio umeze, eeeeehhh hapo Mimi ndio naonaga Napoteza muda, Chakula kikiwa kinywan nakigeuza Moja, mbili ,tatu, ili mradi nimekivunjavunja, basiiiiiiiii namezaa!

Sasa kweli wali, wali jaman niutafune kinywani Kwa muda mrefu,?? Ili iweje ? Wenyewe tu tu tupunje tudogotudogo , wali ni pa paa paa meza, kwanza ukitafuna tafuna sanaaa matokeo yake ndo kutafuna Mawee uanze kulaumu mpishi!

Kuna Siku nmetoka na Bidada wangu Mmoja Boss fulan ivi, basii nikaagiza Nyama ya Mbuzi kilo ya kukaanga na ndizi mkaango na Juice fresh, yeye nikamuagizia Kilo ya Kitimoto na mapombe yake, sasa Mwanangu, Yule Bidada ni Boss alafu Ana cheo Cha kuchaguliwa.

Wakuu nikawa najifanya kula taratibu taratibu , uzalendo ukanishinda nikamchana Laivu, Oyaaa Mimi kula taratibu SIWEZI, ngoja nikipigee chapchap , sema ni vile ma Bidada mabonge hayanaga shida, yenyewe ni kuchekacheka tu basi 🤣🤣 nikala Kwa speed yangu!

Siku hizi sijipi shida, Pesa yangu, tutoke out au ndio Niko mwenyewe, kwann nisile navyotaka?
 
Tatizo ukila polepole chakula kinapoa na mi chakula kikipoa tu kinanishinda
Sasa mie Chakula kiwe na joto la vuguvugu nakifukia dakika mbili paaaaa kimeisha.


Ukitaka nikuone mnoko, Pika Ndizi nyama, alafu pakua zikiwa bado zamoto, Kisha nipakulie Nile ..

Mandizi yanachelewa sana kupoa, na yakiwa yamoto yananiunguza kamdomo kangu, Huwa spendi sana.

Baby watoto wangu yeye ni Mpenzi wa Mandizi , Huwa changu ananipooza kama Cha mtoto mwenye mapengo au anipikie Chakula kingine
 
Sasa mie Chakula kiwe na joto la vuguvugu nakifukia dakika mbili paaaaa kimeisha.


Ukitaka nikuone mnoko, Pika Ndizi nyama, alafu pakua zikiwa bado zamoto, Kisha nipakulie Nile ..

Mandizi yanachelewa sana kupoa, na yakiwa yamoto yananiunguza kamdomo kangu, Huwa spendi sana.

Baby watoto wangu yeye ni Mpenzi wa Mandizi , Huwa changu ananipooza kama Cha mtoto mwenye mapengo au anipikie Chakula kingine
Umeoa muhaya au mchaga...wapenda ndizi hao
 
Kikubwa kula kistaarabu sio unakula mwenyewe kama unagombania, tafuna vizuri unachokula maana mnaokula haraka wengi mnameza bila kutafuna vizuri
Mkuu nikweli, hata hapo kwneye kutafuna, Tena wali, ndo kabisa Huwa na skip hapo kwenye kutafuna.

Nyama yenyewe, nikitafuna Mara mbili nikiona haipondeki, Nina option mbili tu...Kumeza ivoivo au nizuge "Nyama ngumu hiiiiii " kinachofatwa kuweka kwenye sahan ya mifupa.
 
Kikubwa kula kistaarabu sio unakula mwenyewe kama unagombania, tafuna vizuri unachokula maana mnaokula haraka wengi mnameza bila kutafuna vizuri

Mim bib yangu alikuwa akiniambia kula haraka chakula kitapoa kikose ladha,
Ila kuna watu nawafaham wanakula polepole mpaka chakula kinapoaaa wanakula wanapumzika imagine mtu anakula halaf anapumzika
 
Nakula haraka sana , na sijali wala nini . Jana mtu ananishangaa nakula chips za moto kabisa .
🤣🤣🤣 Kuna kicafe fulan, nilikua Kila siku napita kunywa Maziwa fresh yamoto , basi Mimi kitu Cha kunywa hata kiwe chamoto, nakunywa chap ,utadhan Nina ka freezer mdomoni.


Wahudumu wa pale walikua wananishangaaga sana.

Nikaona isiwe nongwa ,nikacha kwenda hapo.

Toka nianze ishi na Baby Mama wangu, aahhh Kila siku jion, lazima nikute chupa ya uji wa lishe, naipigaaaaaa kama nakunywa maji 🤣
 
Back
Top Bottom