Ni jambo gani kubwa ulilopitia ambalo kumbukumbu zake zimegoma kufutika?

kovidii

JF-Expert Member
May 4, 2020
277
264
Nakumbuka ilikuwa Jumapili ya mwisho ya Oktoba, 2009, siku hyo ilikuwa ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Siku hiyo muungwana mimi nilipanga kujitoa uhai kisa na mkasa cha kutaka kujitoa uhai ni kwamba umri unaenda lakini mipango haiendi.

Nakumbuka nilivyokuwa Sekondari nlishajipangia kwamba nikifikia umri fulan inabidu niwe na mtoto wa kwanza (nikiwa na mama yake kwenye mahusiano rasmi).

Miaka mitano inayofuata inabidi niwe na nyumba yenye hati ya jina langu,bila kujali nimejenga tofali kwa tofali au nimenunua.

Miaka mitano mingine ni ya kutafuta gari ya ndoto zangu. Kipindi hicho my dream car was Mercedes Benz convertible.

Miaka mitano mbele niwe na biashara endelevu ambayo inanipa uhakika wa kusogeza siku za maisha yangu na familia yangu bila mawazo yoyote, yaani hata nikienda kwenye mahoteli ya daraja la kwanza niagize vyakula vya kimataifa bila kuathiri pocket yangu, ikija menu niwe naangalia kushoto (kwenye aina ya chakula na sio kulia (kwenye gharama/thamani ya chakula hicho)

Baada ya kuona time inakata,halafu sijatimiza japo lengo moja nikaona ni heri nirudishe namba tu,coz sikuona sababu ya kuendelea kurandaranda duniani nikiwa sina mbele wala nyuma zaidi ya nyeti zangu. Maandalizi ya kujitoa uhai yalianza mwezi mmoja kabla, nilienda kuungama dhambi zangu zot (I'm Catholic)then nikajipa mwezi mmoja wa kuishi kitakatifu (bila kutenda dhambi yoyote)

Basi ilipofika tarehe husika kiukwel nililia sana kuona nawaacha wote niwapendao,japo moyo ulikuwa radhi kabisa kwa Safari niliyoipanga japo mwili ulitaka kuleta udhaifu kwa maswali kwamba niendako sipajui,je hatma yangu itakuaje? Lakini nikajipa moyo kwamba kwa yote niliyopitia, hustle, mateso, kunyanyaswa niliamini Mungu mwenyewe anaona na atanisamehe kwa kujirudisha ghafla ghafla coz mapito yangu yote aliyaona.

Basi baada ya kuangua kilio nilienda ibadani, nako nilikua nalia tu hasa zikiimbwa nyimbo zinazonigusa. Baada ya misa nikiona watu wanatoka Kanisani mimi nabubujikwa tu,coz najua this is my last time nahudhuria ibada. Nlivyotoka church sikuwa na mood hata ya kula,yaani nilikuwa tayari kwa sSafari asilimia zote

Iikafika mchana karibu na jionu nikanunua sumu ya panya ile nyeusi ya chenga chenga pakti nyingi kiasi cha kufikia gram150. Basi nikajisogeza hadi Buguruni (shell pale kwenye stendi kama unaenda Ubungo). Nlivyofika pale stendi nikanunua juice ya sayona ya kopo nikakaa kwenye banda la abiria kusubiri basi. Nikaanza kunywa kidogo ili kupata space ya kuweka mzigo nilionunua.

Nlipouweka nikaanza kutikisa chupa ili sumu iyeyukie kwenye juisi ile,dakika kadhaa nikaona inanichelewesha nikaipiga fasta (japo ilikuwa chungu sana) ilivoisha macho yakaanza kulenga machozi kama mtu alofakamia pombe haraka haraka(walevi wananielewa).Basi nikiwa pale pale kwenye banda la abiria najiskilizia na sikutaka niondoke coz nlipanga kufarikia hapo hapo.

Nikaanza kuhisi mate yote mdomoin yamekauka yaan hakuna unyevu nyevu wowote, ile hali ilinipa ugumu kidogo kuhimili. Kumbuka hapo ni kama dakika10 zipepita tangu niinywe ile sumu. Ikabid nitoke pale nilipokaa niende mbele kidogo ambako kulikuwa na jamaa anauza machungwa, nikanunua moja(sikudai chenji).

Basi jamaa alivyonikatia nilipoweka tu mdomoni na kumeza yale maji maji ya chungwa nikahisi kizunguzungu cha kiwango cha lami....yaani nilihisi kama nimekumbwa na upepo mkali sana ulionizungusha mara moja tu na kunitupa chini. Basi hapo chini nikaanza kuhisi maumivu makali ya tumbo ambayo hayasimuliki(naamini ni makali zaidi ya uchungu wanaosikia wazazi wetu wakati wa kujifungua). Nikaanza kupiga kelele kubwa kwa maumivu niliyokuwa nasikia.

Lile tukio liliendelea kwa dakika kama 5 hivi huku watu wakiwa wamenizunguka wakishangaa tu, hapakua na hata wa kunigusa. Basi baada ya muda alitokea msamaria(Mungu amuweke,coz simjui hata nikikutana nae leo) akachukua bajaji hapo kituoni nikapelekwa hospitali kwa Mnyamani.

Huduma niliyopata pale ni duni plus makusudi ya watoa huduma. Nakumbuka nilivyofika tu wale walionileta walisepa, kulingana na mazingira walioniokota so sikuwa na ndugu. Nliwekwa kitandani huku mhudumu akiendelea kuchezea simu yake.

Dakika kama 5 ndani ya maumivu makali ya tumbo pale kitandani nikaanza kutapika na kuharisha kwa kasi ya ajabu(sujawahi kuharisha vile aisee). Basi yule mhudumu akanishusha chini na kuniamuru niende chooni, kwa kuwa sipajui alinielekeza kwa mkono tu.

Hadi hapo sikuwa na nguvu japo ya kusimama, nilielekea chooni kwa mwendo wa kutambaa huku nikiendelea kutapika na kuharisha non stop

Nilivyofika choonisikuweza japo kuchuchumaa, nilijilaza hapo hapo sakafunu huku nguvu zikiendelea kupungua. Nguvu zilielindelea kupungua hadi muda fulani (sikumbuki kwa kweli kama nilichukua muda gani pale sakafuni choon).

Wakaja wanaume kuniinua pale na kuniweka kwenye wheel chair moja kwa moja hadi kwenye ambulance. Ving'ora vikaanzia hapo kuelekea Hospitali ya Amana. Sikumbuki logistics za kunipokea pale zilikuaje ila nikajikuta nipo ward no2 pale Amana. Pia sikumbuki kilitokea nini lkn nikakuta mama yangu mzazi yupo pembeni yangu pamoja na mama mwenye nyumba aliyokuwa kapanga mama yangu(alikuwa kapanga maeneo ya malapa)

Basi bwana hadi wakati huo nazinduka pale kitandani nilikuwa nimeshaharisha na kutapika vya kutosha sana, pia usiku ulikuwa umeshaingia. Nilivyoamka nikajikuta viungo vyote vimenikamaa, tumbo lote limeingia ndani,huku mbavu zote zikihesabika, mikono ilijikunja kwenye kiwiko na vidole kukakamaa kama uma. Sikuwa tena na control na mwili wangu. Sikuweza kunyoosha mkono wala vidole japo nilikuwa macho na nikiamini nipo konshaz lakini ilishuhudia ngozi ya tumbo langu ikiingia ndani kabisa kiasi cha kutengeneza kitu kama shimo tumboni mwangu.

Nikamwita mama yangu na kumnong'oneza kumweleza ukweli wa nilichokifanya nikiamini nimeshafikia point of no return so sina cha kupoteza.

Nikaanza kutapika matapishi ya kijani,machungu kama shubiri, mama yangu akaanza kulia na kusema "mwanangu sasa anatoa nyongo nampotezaaaa"nikamwambia mama nifunue shuka, akasema mwanangu huna nguo nyingne ndani,nikamjibu siku unanizaa nilikuwa uchi na leo nataka nisepe uchi. Mama akataka kubisha, nikajikuta namkaripia miksa kumtukana kwa nguvu ikabidi anifunue na mwili wote kuwa hadharani bila kipande chochote cha nguo. Wakati huo wagojwa wengne wenye afadhali wamenizunguka wakistaajabu ya Musa.

Baadaye nikajikuta napoteza nguvu zote na kuzima! Sasa ikaanza Kama ndoto naota nmepaishwa juu hadi kufika sehemu naona kama imebaki mita mbili kufikia paa la huko nilikopaishwa, then nikaona watu wawili wananigombea kushoto na kulia kwangu,kila mmoja akisema"wakwanguu.... wakwanguu".

Wakati huo huo huku kitandani nikiwa kwenye hali kama mawenge ya usingizi ila ni kama naona dhahiri kabisa upande mmoja wa mlango wa Ward hiyo namuona paka mkubwa kama mbuzi, wakati huo huo upande mwingine kuna mlango mwingine pia wa kuingilia wodini humo namuona Yesu akija(wote wakisogelea kwenye kitanda nilicholazwa). Yaani hapa niseme wazi nilikuwa ninaona picture clearly kabisaa!!

Basi bwana yule paka alikuwa yuko fasta kuja kwangu kuliko Yesu niliyekuwa namuona. Hapo hapo nikaanza kuzungumza kwa nguvu nikimhimiza Yesu kumwambia ikimpendeza ni vema anichukue. Maumivu niliyopitia kwa masaa machache haya siwezi kuyahimili tena!

Wakati huo namtunaka yule nyau(tena kwa sauti ya juu na matusi kabisa hayo hayo unayoyajua) Nikiendelea hivyo hivyo,nikimsihi Yesu anibebe ama anitolee haya maumivi huku nikimkanya yule nyau asinisogelee. Basi ile hali iliendelea hadi nikaanza kuhisi fahamu zimenirudia.

Cha kwanza nilianza kusikia sauti ya injini ya 14b (injin hii mara nyingi hufungwa kwenye ma-dcm,mafundi magari wananielewa). Ule mlio wa gari ikiunguruma kwa nguvu kwa mbaali ukanigutusha. Kufumbua macho najikuta nimezingirwa na watu kibao, kujiangalia eti nipo uchi wa mnyama(miksa sijanyoa).

Basi dah! bonge na noma,coz mbali na mama yangu, alikuwepo mama mwenye nyumba wake na wahudumu wengine wa kike.

Basi hapo nikajikuta naweza kukusanya shuka na kujisitiri muda huo tayari kunakaribia kupambazuka. Basi baada ya kuona kama fahamu imerudi wakaanza kuja wale wagojwa wenzangu walokuwa wamenizunguka na kuanza kunisifu kwa jinsi nilivyokuwa nakemea shetani,huku wakiahidi urafiki pindi tukifanikiwa kutoka wodini.

Basi pale nikaendelea na tiba hasa dripu kwa siku kama mbili hivi then nikaruhusiwa.

Kiukweli nikiivuta hiyo picha huwa naiogopa sana japo imenipa uhakika wa life after death ila ile juisi niliyoilumangia kwenye sumu hadi leo nikiiona mwili unanisisimka, sijawahi kuinywa tena wala sitak kuisikia achilia mbali kuiona

Nimeona nishee nanyi wakuu kwa Jambo hili ambalo siwezi kulisahau nikiamini pia kila mmoja wetu ana jambo lake japo lisiwe katika muktadha huu.

Nawasilisha!!
 
🙄😲😲
Nitaacha nature iseme nami sio niisemeshe cha kunitenda!
Pole na najua hautakuja rudia.
 
Duuu ni hatari sana.
Vipi lakini sasa hivi ushamiliki vyote ambavyo ulitaka kuvimiliki.?
 
Nina swali moja kwako huyo unaesema ulimuona na umempatia jina yesu!,alikuwa na muonekano gani..?
Na ulijuaje kuwa ni yesu..?
 

Nitaacha nature iseme nami sio niisemeshe cha kunitenda!
Pole na najua hautakuja rudia.
Dah!nw Niko na family.im looking after them.yaan namuomba mungu aniweke hd hawa watoto niwaweke pazur,af nikifikia mama Yao atakua anashirik tendo na kidume kingine!!!!dah!yan I wish nisisepe kbsa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kila mara ninaota sijui kama ninaweza kusahau aiseee.
 
Mimi kila mara ninaota sijui kama ninaweza kusahau aiseee.
Punguza mawazo jaribu kuwa unafanya mazoezi,michezo ya akili na mwili soma vitabu au makala n.k ukienda kulala kichwa kitakuwa bize kusinzia tu hayo mengine yatakuwa yanakuja Mara mojamoja kwa wazamini wa kipindi cha usingizi wako..😉
 
Nina swali moja kwako huyo unaesema ulimuona na umempatia jina yesu!,alikuwa na muonekano gani..?
Na ulijuaje kuwa ni yesu..?
To be honest, upande anatokea alikua na vazi jeupe juu mpaka chini kias sion nyayo zake...halaf kulikua na miale mikali sana imemzunguka(yaan km umeamka ghafla usingizin af ukapigwa full lights

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Punguza mawazo jaribu kuwa unafanya mazoezi,michezo ya akili na mwili soma vitabu au makala n.k ukienda kulala kichwa kitakuwa bize kusinzia tu hayo mengine yatakuwa yanakuja Mara mojamoja kwa wazamini wa kipindi cha usingizi wako..😉
👏👏
 
Jambo fulani..sidhani kama nitakuja kulisahau..nikisema niandike nitalia bure.
 
Back
Top Bottom