Kiujumla sina haja ya kusema chuo kipi Ni bora na kipi si bora. Ninachoweza kusema Kwa kuzingatia kuwa mie Ni mdau wa elimu ya juu Ni kwamba Vyuo vikuu vya Tanzania vimepoteza Dira. Misingi kikuu mitatu ya Ufundishaji, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam imefinyangwa finyangwa. Wahadhiri wanafanya kazi katika mazingira magumu, madarasa makubwa ya wanafunzi na wanafunzi wasio na uwezo kiakili (mfano darasa Lina wanafunzi 1200 Kwa Course moja). Wanafunzi wasioweza Hata kuandika sentensi moja ya Kiingereza iliyosahihi, n.k.
Jukumu la Utafiti katika Taasisi hizi halina uzito tena kutokana na TAASISI zenyewe na Viongozi wake kutokulitilia kipaumbele katika mipango na maamuzi. Mfano, fedha za utafiti hakuna, tafiti za wahadhiri wa vyuo hivi zimekuwa Ni zile zisizo na IMPACT katika Uchumi na teknolojia zaidi ya theoretical research. Tatu, hakuna research grants and awards katika Taasisi hizi na zile Chache zinazopatikana zinaendeshwa kimasilahi na kimaghumashi. Professors na Senior academician hawana muda wa kufanya research and consultancy mentorship Kwa young academician zaidi ya kuwabebesha makaratasi ya kusahihisha na kuendesha tutorials.
Siasa zimevamia sana uendeshaji wa vyuo. Ukuzaji wa intellectual mind hasa Kwa wanataaluma ukizingatia misingi ya Justice, Integrity, openness and Inquisitive mind haupo tena. Top universities management hawahitaji changamoto na mikikimikiki ya Kitaaluma kama ya Enzi za akina Chachage, Baregu, etc. Wote wenye kuenenda na misingi hii wanakuwa labeled kama wakorofi na mizengwe mingi sana inawaandama. Kiujumla Taasisi hizi zimekuwa na miungu watu fulani.
Mwisho, ushawishi wa siasa katika Taasisi hizi Ni mwiba Kwa mustakabali wa ustawi wake. Mabavu na utemi wa wakuu wa Taasisi hizi vina mkono wa wanasiasa mfano hao wa UDOM na Hata UDSM (Tukumbuke issues za Kitila na Baregu).
Ni dhahiri shairi (hasa Kwa wanataaluma) kuwa sasa Universities nyingi za Tanzania Ni Extended secondary schools. Ufundishaji katika mazingira magumu ndio kazi kuu ya wanataaluma. Hakuna fedha za utafiti, mikutano, semina wala warsha. Ila fedha za POSHO za vikao zipo tele.