Hivi ni kwanini UDOM inadharaulika kiasi hiki?

UDOM inachukiwa na watu wenye mtazamo hasi na serikali inayotawala. Hii ni kwa sababu ya nguvu kubwa iliyotumika katika kukijenga chuo hicho wakati wa vuguvugu la kisiasa za vyama hasa CDM. Kwa hiyo kutupiwa dharau za kila aina kwenye chuo cha UDOM ni "DISPLACEMENT DEFENSIVE MACHENISM" (kwa wale waliosoma elimu ya saikolojia nadhani wananielewa).
Pamoja na sababu zingine za watu binafsi lakini hilo la kisiasa ndilo kubwa. Katika taasisi yoyote ya elimu ya juu changamoto hazikosi. Ni chuo kipi kilichokuwa perfect kwa kila kitu?? Never on Earth!
Na kwa hilo tangazo la kazi (kama ni kweli lilitoka) utakuta waliolitoa ni walewale wenye mtazamo hasi na serikali na si vinginevyo!! Na kwa yeyote anayekazana kuponda UDOM, kama unamfahamu personally mchunguze utaniambia, jaribu hata kufuatilia michango yake ktk thread za watu wengine zilizowahi kugusia shughuli za serikali kwa njia moja ama nyingine, utakuta ukweli wa ninalosema.
 
Unajua unapo amsha mada kama hii uwe na ushaidi wa kutosha.UDOM ni chuo bora kabisa na kinatoa wahitimu bora na wenye uwezo na hii ni kwa uthibitisho ufuatao: 1 Kinachukua au kinasaili wahitimu wenye ufauru mzuri, 2 Kinatoa elimu ambayo inaendana na mahitaji ya jamii, 3 Wanafunzi wenye uwezo mdogo huchujwa mapema na hudisco.,4 Ni chuo chenye uadilifu kuanzia mavazi hadi matendo, 5 Kinapee sana kwenye mambo ya siasa na utamaduni.Kama unabisha njoo na uthibitisho halafu nkutumie ushahidi mkubwa wa haya.
 
KIFUSO,UDOM ya 2007 siyo hii ya sasa,UDOM inakua kwa kasi jaman tuongee ukwel chuki binafsi c nzur,mwogopeni Mungu !

Kama zilivyo st. Kayumba secondary schools ndivyo ilivyo St. Kayumba University yaani UDOM.
 
mkuu Excel namuuliza bwana Mpigamsuli kama yupo aonekani kabisa anga hizi mada kama hili lingemfit sana upo wapi kijana.
 
Last edited by a moderator:
tatizo tunalinganisha udom na udsm. itachukua muda kwa udom kuwa juu kama udsm kwa sababu hata udsm nayo ilianza kama udom. lakini cha ajabu unakuta mtu anasoma sauti au tumaini halafu anajilinganisha na wa udom ambae ana sifa zote za kusoma chuo bora tanzania(udsm). wanafunzi wengi wa udom waliomba chuo kama udsm na mzumbe kutoka na kukidhi vigezo vyao sema kilichowabana ni intake capacity ya chuo husika ila kiukweli wanafunzi wa udom ni wale waliofahulu vizuri pia advance na o-level.
 
Francis,acha kutunga mambo,mwogope Mung.Do not make us delusional!u have prejudice to our lovely university!
 
Acha unafiki mleta mada! Hii issue imekaa kisiasa sana kutaka kuwafanya wana Udom kujihisi inferior! Hii inafanana na usipo shabikia chama --- unaitwa mjinga, hujitambui, sio msomi na vtu kama hivyo! Mkiishiwa sera mnaleta vijambo vya ajabu hapa, weka ushahd tafadhali
 
By the way mi ni mhitimu mtiifu wa UDOM na ktk interview ya watu 34 tulipita wawili mi na kaka mmoja ambae b4 alikuwa anafanya kaz katika kampuni lingine, So usitake kuniaminisha wana UDOM tunadharaulika! Afu wewe mleta mada nahisi ndo yule uliye disco tukiwa mwaka wa 2 ukataja chuon kutaka kupigana na walimu!

Wapi ndugu yangu Dreadnought njoo chungulia huku.
 
promo nzuri. yaani watu hamjui kadri mnavyoponda udom ndo waajiri wanaajiri wengi wa huko ili wajishuhudilie utendaji wa wahitimu wa UDOM. wahitimu wa dom nao wanajitahidi wasiharibu ili kuwakata midomo. ushauri wangu ni kwamba, wanaopitia hii changamoto waiangalie in +ve way. msitokwe povu.
 
By the way mi ni mhitimu mtiifu wa UDOM na ktk interview ya watu 34 tulipita wawili mi na kaka mmoja ambae b4 alikuwa anafanya kaz katika kampuni lingine,
unaona. mi nahs ningekuwa mwajiri lazma ningemwangalia graduate wa dom kwa jicho la ziada. yaani pamoja na challenges zote walizoziface na mtu ameweza maliza fresh ujue huyo ni jembe. lol
 
unaona. mi nahs ningekuwa mwajiri lazma ningemwangalia graduate wa dom kwa jicho la ziada. yaani pamoja na challenges zote walizoziface na mtu ameweza maliza fresh ujue huyo ni jembe. lol

Husnadom mzima?
 
unaona. mi nahs ningekuwa mwajiri lazma ningemwangalia graduate wa dom kwa jicho la ziada. yaani pamoja na challenges zote walizoziface na mtu ameweza maliza fresh ujue huyo ni jembe. lol


Mkuu watu wanafkiri chuo knakutengenezea competence, unaeza maliza Oxford university na bado ukawa mbulula, kuna watu wamemalza shule za kata na wakapata division 1 ya point 7 je hapo ni muujiza gan umetendeka! Seriousness and self control ndiyo kila kitu.
 
Back
Top Bottom