UDOM KUNA SHIDA SAUTI YA WANAFUNZI INAPASWA KUSIKIKA
👉Kero ya Kwanza: Madeni Yasiyoeleweka na Kufukuzwa Chuo
Wanafunzi hawadaiwi ila wanawekewa madeni kwenye akaunti zao kwa makusudi pesa ambazo hawaelewi chanzo chake na matokeo yake huwekewa "withheld". Baada ya muda mrefu, hutolewa barua ya kuachishwa chuoni (disco) moja kwa moja kwenye mfumo na kushindwa kuendelea na masomo. Idadi kubwa sana yaani sana mno mno ya wanafunzi wanaacha au kuachishwa chuo kwa njia hii, bila ufafanuzi wa kutosha, na hii inaharibu ndoto zao kabla hazijatimia.
👉Kero ya Pili: Carry Over kama Chanzo cha Kutoza Fedha
Kuna malalamiko makubwa sana: baadhi ya walimu huwapa wanafunzi carry over kwa makusudi kabisa, ili kuongeza mapato ya chuo na hata marupurupu yao wenyewe. Hebu fikiria nusu ya darasa la wanafunzi 70 wote wabebeshwa somo moja. Kinachotokea mwaka unaofuata? Mwalimu yule yule anawabeba hao hao tena, kwa makusudi, na hata anasema waziwazi bila hofu wala aibu yoyote ile.
Kulipa zaidi ya shilingi 100,000 kwa kila somo moja la carry over ni mzigo mzito usioweza kuvumilika hasa mtu anapojikuta na masomo mengi yaliyobebeshwa. Mbaya zaidi, ada ya usajili sasa inatozwa kila mwaka kwa kiasi kikubwa, badala ya kulipwa mara moja kama ilivyokuwa zamani. Haya yote kwa pamoja yanazidisha sana ugumu wa kifedha kwa kila mwanafunzi.
👉Kero ya Tatu: Haki na Upendeleo
Walimu wengi hawasahihi kazi kwa uadilifu hufanya makadirio na kutoa alama ndogo kwa wanafunzi wa kawaida, wakati mwingine hata wanaweka wanafunzi wengine kusahihisha kazi za wenzao. Kwa upande mwingine, viongozi wa serikali ya chuo na wale wanaofahamika hupata alama za juu kwa upendeleo wa wazi. Hii si haki, inakatisha tamaa, na inapunguza uaminifu wa elimu inayotolewa hapa.
👉Kero ya Nne: Mashtaka ya Ulaghai wa Mfumo Bila Ushahidi
Mamia ya wanafunzi wamewekewa mashtaka ya kuhack mfumo wa SR2 na kuachishwa masomo bila sababu za msingi. Inaumiza sana mtu anapokuwa katika mwaka wa mwisho wa masomo akabambikiziwa kesi isiyo na kichwa wala mkia, na kuchukuliwa fursa ya kumaliza masomo aliyoitumia muda mwingi kuyasomea. Hii ni haki iko wapi?
👉Fikiria mwanafunzi anayepokea mkopo wa laki sita anatoa nusu kwa ajili ya usajili na michango mbalimbali, halafu abaki na kiasi kidogo cha kulipa ada, kununua chakula, na kulipa carry over ya kila somo.
👉UDOM ni miongoni mwa taasisi muhimu sana kwa taifa hili inatakiwa kuzalisha watumishi wenye uwezo, sio kuwahujumu vijana. Watoto wa familia za hali ya chini ndio wengi hapa, na haifai wakabebeshwe mizigo isiyo na maana kwa ajili ya raha za wachache ofisini. Serikali na wizara husika zisikae kimya zifanye uchunguzi wa haraka, zifuatilie kila kero hii, na zihakikishe mazingira ya masomo UDOM yanakuwa ya haki, salama, na yenye kuwezesha kila mwanafunzi kufanikiwa.
👉UDOM KUNA SHIDA Hii ni aibu kwa taifa, na inapaswa kurekebishwa sasa hivi.