Hivi ni kwanini UDOM inadharaulika kiasi hiki?

Japo ni chuo kikubwa na cha kisasa mno barani Afrika
Thibitisha usasa wa chuo kikuu cha Dodoma!

hivi unajua maana ya usasa??

usasa gani hakuna waalimu wa kutosha?

usasa gani hakuna learning material za kutosha?

usasa gani waalimu hawalipwi salaries and wages kwa wakati?

usasa gani chuo kinaanzisha bila kufanyika kwa research nini kinahitajika? yani wanafunzi weeeengi wakati walichofuata hakitoshelezi?

usasa wa UDOM una ukale mwingi sana! kuanzia top level management mpaka chini, mpaka serikalini, ni majanga tu!
 
Nilipo sema usasa nilikuwa namaanisha majengo mapya, makubwa na ya kisasa kabisa..! Em' jaribu kunielewa basi..
 
Japo ni chuo kikubwa na cha kisasa mno barani Afrika chuo hiki kinadharaulika mno kitaaluma. kuna tangazo moja la kazi lilikuwa linasema kwamba.., kigezo moja wapo ili mtu aweze kupata hiyo ajira ni kwamba "ASIWE amehitimu kutoka UDOM" ..!!!!!

Uwepo wa UDOM umesababisha na utaendelea kusababisha watu na makundi fulani waathirike na hata hao ambao waliwahi kusema hawataajiri mtu kutoka UDOM walifanya hivyo kuwaungamkono wadau wenzao ambao uwepo wa UDOM Unawasumbua.
Ukitaka ujue ukweli wa Chuo Cha Dodoma uliza wanaosoma pale na ndio utajua ukweli kuhusu:-

1. Elimu inayotolewa UDOM haipisha na vyuo vingine ukiachia mbali kuwa chuo hicho bado ni kichanga ukulinganisha na vyuo vingine.
2. Elimu ya UDOM sio ILE YA SPOON FEEDING kama baadhi ya vyuo ambavyo watu wengine huvisifia.
 
Hao wanaosumbuliwa ni akina nani.., na wanasumbuliwa kwa lipi...?!
 
ukubwa wa chuo sio majengo na rangi za kupendeza,hicho chuo kina mapungufu mengi likiwemo uwezo mdogo wa wahitimu,ni mpango mahusus sawa na mpango wa sec za kata ambazo wahitimu hawajui kusoma wala kuandika
 
Jamani hebu tuache unafiki wa kuponda kila jambo.ukweli ni kwamba shule za kata na uanzishwaji wa udom unesaidia asilimia kubwa sn kuelimisha kundi kubwa la vijana wa nchi hii hata kama elimu inayotolewa ina mapungufu lkn kuna vijana wamehitimu udom na kuajiriwa na wengine wemejiajiri
.Shule za kata nazo zimetoa muamko kwa vijana hasa ktk masuala ya kisiasa, jamii n.k
 
ukubwa wa chuo sio majengo na rangi za kupendeza,hicho chuo kina mapungufu mengi likiwemo uwezo mdogo wa wahitimu,ni mpango mahusus sawa na mpango wa sec za kata ambazo wahitimu hawajui kusoma wala kuandika

Naomba utaje hayo mapungufu na utueleze ni kwa namna gani wahitimu wake wanauwezo mdogo
 
Jaman naomba maon yenu, ni bora kuwa na wasomi wengi wasio-competent au kuwa na wachache wenye competence?
 
Back
Top Bottom