Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,470
2,000
Nimeathirika na haka kaneno mpaka baadhi ya watu weanza kuniita mkuu........ Hata baadh ya jamaa zangu hapa chuo nishawaamishia haka kajina........ Lakini hakachuji
 

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,071
1,250
wakuu wote waliochangia topiki hii nawaheshimu sana.
salamu kwenu wakuu na heshima kwenu wakuu.
 

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,071
1,250
binafsi naitumia mkuu kuzuia offence kwa watu...kwa sababu hatujuani umri na jinsia naamua kulitumia mkuu kumtaja mtu..ndo hivo mkuu
mkuu umenifurahisha kwa majibu yako ya busara.
utakuta mtu anaanza kwa kumwita mwenzake mburura, sijui paka shume na mengine mengi. lakini kwa busara hata kama umekwazika na hoja ya mwenzako ukianza kumuita mkuu kwa kumtambua kuwa naye ana heshima na utu yanayofwata huwa na busara na ustaarabu.
heshima kwako mkuu.
 

mdeki

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
3,304
1,225
Asanteni wakuu nimeelewa vizuri sana na si kuwa jina linanikera kama mchangiaji mmoja alivyohisi laa! Ni katika kutaka kujua tuu, kazi njema, na tujitume katika kufanya kazi yoyote ile si lazima uwe ofisini hata ya kwako binafsi
 

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,306
1,250
Silipendi neno hili wengi wanaliita kwa kukebehi kuwa makini angalia usilishobokee
 

yuppie boy

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
216
0
Ishakuwa hutaratibu sasa wa JF, lakini si unajua kuna kitu kinaitwa rejesta nlisomaga loong tym kwa mfanô wale wa dodoma wanahitana waheshimiwa so na si ni wakuu
 

Madiba

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
419
250
Hilo jina "Mkuu" asili yake ni jeshini. Waliopitia JKT ya zamani kabla haijarudishwa hivi karibuni wanalijua sana. Recruits walikuwa wanawaita wakufunzi wao "Mkuu" au "Afande". Hivyo ikatokea recruits nao wenyewe kwa wenyewe wakawa wanaitana "Mkuu" kwenye maongezi yao ya kila siku, na wakaendelea kulitumia hata baada ya kumaliza JKT na kuingia vyuo vikuu na kazini. Na ni kwa mtindo huo jina hilo lilitua huku JF. Members wakongwe, au siyo?

Amandla awethu, all power to the people.
 
Top Bottom