Hivi mishahara ya madaktari na watumishi wengine wa afya katika hospitali za umma inalipwa na nini?

Swali hili linaniumiza sana kichwa.

Je watumishi hawa wa sekta ya afya mishahara yao inalipwa na bima ya afya au ni kutokana na bajeti kuu ya serikali inayotokana na kodi mbalimbali?

Kama mishahara yao inatokana na bima ya afya basi serikali haina budi kurekebisha, mishahara ilipwe kutokana na kodi ili kumpunguzia mwananchi gharama za matibabu.

Na kama mishahara yao inatokana na kodi mbalimbali (mapato ya Hazina), kwa nini gharama za matibabu ni kubwa kiasi hiki?

Ukweli ni kuwa watu wengi sana wako majumbani wagonjwa hawawezi kwenda hospitali kwa sababu ya kutomudu gharama.

Chonde chonde Serikali punguza gharama za matibabu Taifa linaangamia!
Jamaa wanataka wananchi waendelee kuugua na kufa ili watoto wao waje watutawale
 
Sawa ni gharama kwa nini serikali isiweke ruzuku ya kutosha ili wananchi wavipate kwa gharama nafuu. Vifaa tiba vyote vinanunuliwa kwa kodi, majengo na miundombinu ya hospitali ni kodi, mishahara ni kodi hivyo hakuna kisingizio!
Gharama inatoka wapi? kipaumbele chao wao ni V8, ufisadi na posho nene
 
Na mimi nipo kazini na kila mwezi nalipwa extra duty allowance. Hatutozi consultancy fee ingawa kuna tozo zingine watu wanalipa na fedha inakwenda hazina.

Hoja yangu ni serikali ichukue jukumu lake la kuhudumia wananchi!
Consultation few siyo pesa ya Daktari. Na hakuna Daktari akiyekaa akaoanga viwango vya pesa ya kumuona Daktari na Wala Daktari hahusiki. Hiyo pesa hupokelewa mapokezi.

Consultation ni sehemu ya gharama za matibabu Kama ikivyo vipimo na Dawa na admission.

HAKUNA mahusiano yoyote Kati ya consultation fee na Mshahara wa Daktari
 
Argument yangu ni kuwa hiyo consultancy fee ifutwe haina tija kwa serikali! Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kugharimia matibabu.
 
Na kama mishahara yao inatokana na kodi mbalimbali (mapato ya Hazina), kwa nini gharama za matibabu ni kubwa kiasi hiki?

Ukweli ni kuwa watu wengi sana wako majumbani wagonjwa hawawezi kwenda hospitali kwa sababu ya kutomudu gharama.
Toka nitozwe fedha kibao kisa "Amiba", nimeamua kutumia majani safi ya mpera, mtuntunu( watu wa Kanda ya Ziwa wanajua wawulizeni), na kashwagara( kiungo mojawapo cha kupambana na korona).

Unatafuna majani hayo na kumnyonya juice ya hayo hayo majani unayotafuna kisha unameza juice na machicha uliyotafuna kabla ya chai Asubuhi, kabla ya chakula cha Mchana na kabla ya chakula cha usiku. Siku mbili umepona kwa dozi hiyo.

Kwa mtu mzima unachukua Jani moja la mpera, moja la mtuntunu, na moja la kashwagara . Kipimo cha mtoto sijui.

Nimejaribu hii mwenyewe na nimepona. Kabla ya kuitumia tiba hii kapime kwanza kujiridhisha unaumwa tumbo kwa sababu ya Amiba ama una matatizo mengine. Usitumie dawa yoyote kabla ya kujiridhisha kuwa unaumwa kitu gani.

Watu wa vipimo nao nawaandalia faili lao.
 
Inaelekea umezaliwa miaka ya 2000! Huduma zote ulizoorodhesha zilikuwa zinalipiwa na serikali na wagonjwa waliolazwa walikuwa wanapata chakula bure na bado huduma zilikuwa za kuridhisha!
Huduma za miaka hiyo ambayo kulikuwa na vipimo vingi hamna unaambiwa huna shida kajaribu tiba mbadala ni sawa na siku hizi halafu iwe bure hio haipo popote pale ukitaka kuzalisha taifa la wajinga ,wavivu wazembe weka kila kitu bure bure waweke bei stahimilivu ila sio bure iendelee hivi hivi watoto bure na wamama wenye mimba sisi wengine tukalime vibarua tukajichanganye na kubeba zege tutunze fedha ili zitusaidie kesho yetu sema labda tupambane tuishauri serikali ijitahidi ishushe viwango vya kuchangia iwe kama Kenya bima iwe mtu kwa mwezi anaweza kuchangia hata elfu kumi kama tu sie vibarua tunachangia nssf zetu ila sio hii ya kila kitu bure ,tulianza bure bure hiyo na mwisho tumetengeneza vizazi na taifa la watu wasiotaka kufanya kazi wanataka bure bure na kudai vya bure mwisho wa siku vitu vinapoteza thamani na thamani ya kazi na kutafuta fedha itapotea kabisa mtu ajue usipofanya kazi na kuhangaika huta mudu maisha hutamudu huduma muhimu watu wafanye kazi na hii ndio maana kuna mataifa tajiri lakini hayaweki bure bure yanauwezo huo ila yanajua ukitaka kujenga taifa la wazembe basi weka kila kitu bure bure hapo utauwa spirit ya innovation na lengo hasa la watu kutafuta hela na kujiendeleza wao na taifa lao ukweli mchungu ila ndio huo na ikizingatiwa hio bajeti yenyewe kwa sasa hatujitoshelezi 100% nyingine tunaikopa au tunasaidiwa halafu tunakuja kutoa vya bure hii kama mimi ningekuwa mwenye nafasi siiruhusu hata kidogo ukakope uje uwape watu vya bure na kujitia madeni yanayoathiri ukuaji wa uchumi ,hii la msingi ni kupunguza gharama kwa kuwavutia wawekezaji walete ajira kwa kujenga viwanda vya madawa na vya vipimo na vifaa vingine ili kupunguza gharama za kuagiza kutoka mbali na pia kuhakikisha vipatikane kwa urahisi na kuwapunguzia kodi wazalishaji wa vitu hivyi ili gharama zake ziwe stahimilivu kwa walaji lakini sio kununua bei juu halafu ukatoe bure hapana sio sawa tukifanya hivyo tutaendelea kuitwa taifa masikini kila kukichwa kisa tu kuridhisha watu kisiasa hizo zitakuwa siasa muflisi.
 
Nani kakudanganya wazungu wanatoa pesa?
Busket funds anatoa baba yako?

Clinic za matunzo na Dawa za UKIMWI na TB unagharamia wewe?

Dawa za waraibu wa madawa ya kulevya unagharamia?

Vipimo vya Maralia na Dawa mseto ya Maralia unalipia?
 
naichukia siasa,hasa hii kunuka ya ccm.

hakuna kitu wanaweza hawa mapanya,sio kukaripiana wala sio kusimamiana,yanachojua ni kuchoresheana michongo ya kupiga zaidi.

hawa wataalam unawezasema hii hela inawahusu,kumbe unapewa risiti na hela yote inakwenda hazina,yanakaa kujadili namna gani ya kununua gari mpya za wabonge matumbotumbo.
 
We jamaa bhana,mbona jamaa anakuelekeza vema tu?
Wananchi tunalipa kodi,kodi hizo ndo zinanunua vifaa tiba na madawa,unasema ni ghali,kwani serikali inajitolea kununua vitu hivyo tajwa?
Madawa na vifaa tiba ni gharama
 
Swali hili linaniumiza sana kichwa.

Je watumishi hawa wa sekta ya afya mishahara yao inalipwa na bima ya afya au ni kutokana na bajeti kuu ya serikali inayotokana na kodi mbalimbali?

Kama mishahara yao inatokana na bima ya afya basi serikali haina budi kurekebisha, mishahara ilipwe kutokana na kodi ili kumpunguzia mwananchi gharama za matibabu.

Na kama mishahara yao inatokana na kodi mbalimbali (mapato ya Hazina), kwa nini gharama za matibabu ni kubwa kiasi hiki?

Ukweli ni kuwa watu wengi sana wako majumbani wagonjwa hawawezi kwenda hospitali kwa sababu ya kutomudu gharama.

Chonde chonde Serikali punguza gharama za matibabu Taifa linaangamia!
Gharama za matibabu kubwa ukilinganisha na nini? Unajua unafanya cost sharing? Ukitaka ujue gharama halisi za matibabu ulizopaswa kulipa njoo Aga Khan.
 
Gharama za matibabu kubwa ukilinganisha na nini? Unajua unafanya cost sharing? Ukitaka ujue gharama halisi za matibabu ulizopaswa kulipa njoo Aga Khan.
aga khan hata panadol sio hizi za kenya na TZ za 200 unataka kusema nini kwa mfano???
 
Sawa ni gharama kwa nini serikali isiweke ruzuku ya kutosha ili wananchi wavipate kwa gharama nafuu. Vifaa tiba vyote vinanunuliwa kwa kodi, majengo na miundombinu ya hospitali ni kodi, mishahara ni kodi hivyo hakuna kisingizio!
Hizo dawa na vifaa tiba havina kodi. Hata uuze kwa bei ya kiwandani, bado gharama za hivyo vitu ni kubwa.

Gharama za matibabu nchini Tanzania zipo chini sana. Tena kuwa chini kwake kunafanya huduma zetu za afya zisikue. Maana hospitali zinapata kipato kidogo, zinashindwa kujiendeleza.
 
Nani kakudanganya wewe. Wanatoa mbinguni? Unadhani kwa nini Aga Khan bima ndogo za NHIF hawazitaki? Prices za NHIF zinafanana na cost sharing.
ndio nikuulize wewe,kama wanatoa hapo hapo nairobi na hapo jeti hizo dawa nini kinafanya wauze bei zao peke yao???
 
We jamaa bhana,mbona jamaa anakuelekeza vema tu?
Wananchi tunalipa kodi,kodi hizo ndo zinanunua vifaa tiba na madawa,unasema ni ghali,kwani serikali inajitolea kununua vitu hivyo tajwa?
Unalipa kodi kiasi gani? Mahitaji ya nchi ni kiasi gani?unadhani kodi tunayolipa inatosheleza kila kitu kama ni hivyo mbona kusingekua na mikopo wala shida kwenye nchi hii.
 
Kumbuka consultancy fee ni kubwa kwa wananchi wengi kumudu. Ikiondolewa wananchi wengi wataweza kuwaona madaktari na kupata matibabu sahihi kuliko hivi sasa ambapo watu wanaenda pharmacy moja kwa moja.
Uko sahihi kuwa consultation fee ni kubwa, lakini hiyo haileti uhalali wa kuiondoa, labda useme ipunguzwe.

Unachotakiwa kuelewa ni kuwa, consultation fee ni moja ya chanzo muhimu cha mapato kwa hizi hospitals kwani serikali haighalimii kila kitu kwa 100%. Maana yake ni kuwa, ikiondolewa pale hospital itapelekwa sehemu nyingine na lazima wananchi tuilipie tu. Kama ni ugumu wa maisha utaendelea kuwa pale pale. Ni kama vile development Levy ilivyoondolewa ikawekwa kwenye bidhaa ikasababisha bidhaa kupanda bei. Au kodi ya nyumba ilivyowekwa kwenye umeme ikasababisha umeme kupanda bei.

Kiufupi uendeshaji wa hospitals kama zilivyo taasisi nyingine una gharama sana ambazo ukisema serikali izilipe zote kutoka kwenye makusanyo ya kodi moja kwa moja watu watalia zaidi.

Suluhisho hapa ni matumizi sahihi ya rasilimali zetu ili tukuze uchumi wetu. Ndio hapo serikali itaweza kulipa vizuri hizi gharama zote. Lakini kwa mwendo wetu huu, we've a long way to go.
 
Unalipa kodi kiasi gani? Mahitaji ya nchi ni kiasi gani?unadhani kodi tunayolipa inatosheleza kila kitu kama ni hivyo mbona kusingekua na mikopo wala shida kwenye nchi hii.
Tambua kodi ninayolipa ndiyo inayowafanya wanasiasa wanunuliwe V8 mpya,zero Km,wezi mbalimbali wa fedha za umma wanachota kodi ninayolipa,watu wanalipana sitting allowances nono kutoka kwenye hiyohiyo kodi yangu n.k
Hiyo mikopo inayoombwa nje ya nchi,ikija inatumika kiasi,na kiasi kinafujwa.Tatizo hapo ni usimamizi mbovu wa kodi yangu kwa wale waliopewa dhamana,ndomaana unaona kodi yangu haitoshi.
 
Uko sahihi kuwa consultation fee ni kubwa, lakini hiyo haileti uhalali wa kuiondoa, labda useme ipunguzwe.

Unachotakiwa kuelewa ni kuwa, consultation fee ni moja ya chanzo muhimu cha mapato kwa hizi hospitals kwani serikali haighalimii kila kitu kwa 100%. Maana yake ni kuwa, ikiondolewa pale hospital itapelekwa sehemu nyingine na lazima wananchi tuilipie tu. Kama ni ugumu wa maisha utaendelea kuwa pale pale. Ni kama vile development Levy ilivyoondolewa ikawekwa kwenye bidhaa ikasababisha bidhaa kupanda bei. Au kodi ya nyumba ilivyowekwa kwenye umeme ikasababisha umeme kupanda bei.

Kiufupi uendeshaji wa hospitals kama zilivyo taasisi nyingine una gharama sana ambazo ukisema serikali izilipe zote kutoka kwenye makusanyo ya kodi moja kwa moja watu watalia zaidi.

Suluhisho hapa ni matumizi sahihi ya rasilimali zetu ili tukuze uchumi wetu. Ndio hapo serikali itaweza kulipa vizuri hizi gharama zote. Lakini kwa mwendo wetu huu, we've a long way to go.
Uko sahihi lakini kinachotuangusha kama nchi ni serikali kuwa na usimamizi dhaifu wa rasilimali tulizonazo, ubadhilifu, rushwa, Ubinafsi na anasa.
 
Uko sahihi lakini kinachotuangusha kama nchi ni serikali kuwa na usimamizi dhaifu wa rasilimali tulizonazo, ubadhilifu, rushwa, Ubinafsi na anasa.
Mkwamo wetu kama taifa na Africa kwa ujumla uko hapo
 
Daaah ila hali ni mbaya life limekuwa gumu mno mtu anaona bora kubaki nyumbani asubiri kufa tuu maana hana nauli, pesa ya kula, pesa ya matibabu pesa ya dawa.

Inauma sana Mungu angalia wanao humu dunian wanateseka sana
Viongozi saidieni wananchi wenu ipo siku mtaenda kujibu kwa Mungu

Hicho cheo ni dhamana tuu ni cha muda mfupi lkn wasaidieni watu wenu
Yani unaiambia serikali ya CCM chonde chonde??
 
Back
Top Bottom