Kutoka Bungeni Mbunge Shabiby Ashauri Bima ya Afya Itumike Serikali za Umma Pekee

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
45,828
53,027
Moja ya kundi linalosababisha hasara ya mfuko wa Bima ya Afya ni Hospital Binafsi.

Sasa Ili kukabiliana na wizi huo wa kalamu Mbunge Ahmed Shabiby ameishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kufuta matumizi ya bima Hospital Binafsi badala yake bila iwe Kwa Hospital za Umma pekee.

---
Wabunge hatuna fedha.

Mbunge wa Gairo, Ahmedy Shabiby amesema mishahara yote ya wabunge inaishia kwa wananchi kwa kuwachangia fedha za matibabu pale wanapougua kutokana na wananchi wengi kukosa bima za afya.

Shabiby amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

"Wananchi wanatupa tabu kwa ajili ya kuugua. Watu wanasema wabunge wana mishahara mikubwa lakini ukifikiria fedha zote zinaishia kwa wananchi. Mfano wewe Spika nikiangaliaga hela unazotumia kwenye jimbo huwa nakuonea huruma na siku ukija kutoka kwenye ubunge utakuja kuvaa kandambili, moja nyekundu moja ya kijani. Utakuwa umeshachanganyikiwa," amesema Shabiby.


Swali.
Tupe maoni Yako.
 
Tatizo gharama za hospital ni kubwa sana ,yaani kumuona Dr ni 30,000/= huu si usanii? Kuwe na Mamlaka ya kudhibiti gharama za hospital nchini....Serikali inunue Mashine nyingi kila mkoa kwa ajili ya kupimia wagonjwa na iwe na bei rafiki ,hizo mashine zinunuliwe ktuoka kwenye tozo ,tozo lengo lake lilikuwa kujenga madarasa lakini mpaka sasa bado zinaendelea kukatwa ,hizo tozo sasa zielekezwe kwenye kununua mashine za mahospitalini ambapo bei yake iwe ya chini kupima wagonjwa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Sema kuna ka ukweli. Ukienda hosp binafsi na kadi ya bima hata kama unapiga chafya tu utaandikiwa dawa za alergy zile expensive za kutosha pengine hata hukuziitaji. Waboreshe huduma hosp za uma. Raia wapewe bima.
 
Sasa kwa nini wao waamue juu ya michango (pesa) yetu.
Tatizo wanafikiri hiyo bima ni bure kumbe watu wanachanga. na kwa sababu hatuwezi kuumwa wote kwa pamoja ndio hivyo tunasaidiana indirectly kupitia pesa zetu.
Ni jukumu lao, harafu umeambiwa private sector inafilisi bima
 
yeye mwenyewe siku mavirusi yake yamechachamaa anakimbilia India na Ulaya kubadilisha damu, hapo kapewa mic anajitia kubwataaaaaa, kweli wajinga ndio waliwao.
Dialysis inafanyika Mikoani aende India kufanya nini?
 
Ukweli usemwe,Hospitali binafsi pamoja na kusaidia serikali kutoa huduma za afya lakini wizi mkubwa unafanyika huko kwa kushirikiana na watumishi wa NHIF lakini ukweli huo ukisemwa kuna watu kwa sababu ya maslahi yao binafsi uwa wanakuja juu sana.
 
Jamani watanzania sisi tumewakosea nini hawa watawala wetuu? kila uchao hakuna wakujaribu kututafutia unafuu? mweee!
 
Back
Top Bottom