Hivi mishahara ya madaktari na watumishi wengine wa afya katika hospitali za umma inalipwa na nini?

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,155
3,798
Swali hili linaniumiza sana kichwa.

Je watumishi hawa wa sekta ya afya mishahara yao inalipwa na bima ya afya au ni kutokana na bajeti kuu ya serikali inayotokana na kodi mbalimbali?

Kama mishahara yao inatokana na bima ya afya basi serikali haina budi kurekebisha, mishahara ilipwe kutokana na kodi ili kumpunguzia mwananchi gharama za matibabu.

Na kama mishahara yao inatokana na kodi mbalimbali (mapato ya Hazina), kwa nini gharama za matibabu ni kubwa kiasi hiki?

Ukweli ni kuwa watu wengi sana wako majumbani wagonjwa hawawezi kwenda hospitali kwa sababu ya kutomudu gharama.

Chonde chonde Serikali punguza gharama za matibabu Taifa linaangamia!
 
Daaah ila hali ni mbaya life limekuwa gumu mno mtu anaona bora kubaki nyumbani asubiri kufa tuu maana hana nauli, pesa ya kula, pesa ya matibabu pesa ya dawa.

Inauma sana Mungu angalia wanao humu dunian wanateseka sana
Viongozi saidieni wananchi wenu ipo siku mtaenda kujibu kwa Mungu

Hicho cheo ni dhamana tuu ni cha muda mfupi lkn wasaidieni watu wenu
 
Tatizo swali lako hujaeleweka mkuu. Maana watumishi wote wanalipwa moja kwa moja kutoka hazina kupitia makusanyo ya kodi ya TRA
Sawa! Lakini swali langu nataka kufahamu je ile fedha ya kumuona daktari (consultancy fee) ndiyo inayotumika kuwalipa mishahara yao? Na kama wanalipwa moja kwa moja na makusanyo ya TRA basi consultancy fee ifutwe kwa sababu watumishi wote wanalipwa mishahara yao kutokana na makusanyo hayo.

Kumbuka consultancy fee ni kubwa kwa wananchi wengi kumudu. Ikiondolewa wananchi wengi wataweza kuwaona madaktari na kupata matibabu sahihi kuliko hivi sasa ambapo watu wanaenda pharmacy moja kwa moja.
 
Uendeshaji wa shughuli ndogo ndogo pale hospital,pesa inatoka wap? Watumishi wanalipwa pesa ya masaa ya ziada,kulipa vibarua n.k.
 
Sasa gharama za matibabu na mishahara ya madaktari na watumishi wengine wa afya vina uhusiano gani?
Kama madaktari na watumishi wengine wa afya wanalipwa mishahara kwa makusanyo ya TRA (Kodi) kwa nini gharama za matibabu kwenye hospitali za umma ziwe ghali kiasi hiki? Kwa mfano mashine zote za upimaji kama X Ray's, MRA, MRI, CT scan nk zinanunuliwa kwa kodi kwa hiyo tayari wananchi wamechangia.

Lazima serikali itafakari kwa makini suala hili!
 
Madawa na vifaa tiba ni gharama
 
Sawa ni gharama kwa nini serikali isiweke ruzuku ya kutosha ili wananchi wavipate kwa gharama nafuu. Vifaa tiba vyote vinanunuliwa kwa kodi, majengo na miundombinu ya hospitali ni kodi, mishahara ni kodi hivyo hakuna kisingizio!
Ruzuku ya kutosha ndio changamoto
 
Sawa! Lakini swali langu nataka kufahamu je ile fedha ya kumuona daktari (consultancy fee) ndiyo inayotumika kuwalipa mishahara yao? Na kama wanalipwa moja kwa moja na makusanyo ya TRA basi consultancy fee ifutwe kwa sababu watumishi wote wanalipwa mishahara yao kutokana na makusanyo hayo.

Kumbuka consultancy fee ni kubwa kwa wananchi wengi kumudu. Ikiondolewa wananchi wengi wataweza kuwaona madaktari na kupata matibabu sahihi kuliko hivi sasa ambapo watu wanaenda pharmacy moja kwa moja.
umeongea point kubwa sana master
 
Gharama zote unazotozwa hospitali ndizo zinazotumika kuendesha hivyo vituo vya Afya.

Mapato yanatokana na:

- Cash ( pesa wanazolipa wasio na Bima ikiwemo kumuona Daktari/consultation.

  • Bima
  • Pesa ya wafadhili/Wazungu.

Hizo pesa ndio:

  • Zinanunua Dawa
  • Zinalipa vibarua wa mocuwari, usafi, walinzi etc
  • Zinalipa wafanyakazi masaa ya ziada
  • Zinaweka Mafuta kwenye magari ikiwemo ambulance
  • Kuweka internet
  • Kulipa umeme na maji

Madaktari na wafanyakazi wote kwa ujumla wanalipwa kutoka hazina, ambayo ni makusanyo ya Kodi na mapato yote ya Serikali.

Una swali lolote uliza.

Unaweza kuona makusanyo ya hazina yanakotoka👇👇
 
Attachments

  • IMG_20230810_185040.jpg
    IMG_20230810_185040.jpg
    480.6 KB · Views: 5
Gharama zote unazotozwa hospitali ndizo zinazotumika kuendesha hivyo vituo vya Afya.

Mapato yanatokana na:

- Cash ( pesa wanazolipa wasio na Bima ikiwemo kumuona Daktari/consultation.

  • Bima
  • Pesa ya wafadhili/Wazungu.

Hizo pesa ndio:

  • Zinanunua Dawa
  • Zinalipa vibarua wa mocuwari, usafi, walinzi etc
  • Zinalipa wafanyakazi masaa ya ziada
  • Zinaweka Mafuta kwenye magari ikiwemo ambulance
  • Kuweka internet
  • Kulipa umeme na maji

Madaktari na wafanyakazi wote kwa ujumla wanalipwa kutoka hazina, ambayo ni makusanyo ya Kodi na mapato yote ya Serikali.

Una swali lolote uliza.

Unaweza kuona makusanyo ya hazina yanakotoka👇👇
Naona unaleta siasa za ukada katika maisha ya watu!
1. Angalia bajeti ya wizara ya afya kila mwaka kuna fedha imetengwa ya madawa, je huwa fedha hii haitolewi?

2. Wizara zote zina vibarua, walinzi, over time na extra duty allowances, internet, zinatengeneza magari yao na kununua mafuta, zinalipa maji na umeme nk ikiwemo makao makuu ya wizara ya afya kwa kupata fedha za kodi kutoka Hazina. Je kwa nini hospitali ambazo ndizo zinatoa huduma muhimu kwa wananchi zisipate hizo fedha au zisitengewe bajeti kwa matumizi hayo?

Badala yake serikali kila mwaka inafanya matumizi ya hovyo yakiwemo ununuzi wa magari ya kifahari, kulipa posho zisizo za lazima, viongozi kufanya safari ambazo hazina tija. Pia Rais anapata mwanya wa kuunda vyeo ambavyo haviko kikatiba kwa kuwa anaona kama kuna fedha zisizo na kazi zipo zipo tu nk.
 
Back
Top Bottom