Kuna bwana mmoja mjanja mjanja sana na anapenda kutumia vyombo vyake vya matangazo ikiwa ni pamoja na TV,Radio na magazeti.
Ni mjanja sana wa kukimbilia media pindi anapobanwa kwa hoja.
Ni mnafiki kwelikweli na ametumia makundi ya kijamii yenye shida kujijengea umaarufu asiostahili.
Amejidai ni mwenye nguvu ya media yenye uwezo wa kuangusha serikali!
Amewalaghai hata chadema kwa kujidai kurusha mikutano yao.
Ni mlaghai mno na mjanja sana wa kufuata upepo.
Ninachomuhurumia ni kwamba mwaka huu amaingia pabaya(wrong turn)
Kosa la kujiunga na kambi ya kifisadi ni kosa atakalojutia maishani kwani kwa mara ya kwanza ATASHINDWA na hapo ndio itakuwa kikomo cha UNAFIKI wake.
Bado majuma kama mawili tu kitaeleweka.
Unakokwenda hauko sahihi.
Chama cha Mapinduzi kinamilikiwa na watu milioni saba waliojiwekea utaratibu wao
wa kupata wagombea wa nafasi za uongozi katika nchi yetu.
Nafasi ya Urais, kwa utaratibu wa CCM, wagombea hujadiliwa na Kamati Kuu.
Nimemsikia mwalikwa wa Dar kwenye Star tv akilalama kunyimwa nafasi ITV kuwajadili watia nia.
NAWAPONGEZA SANA ITV. Nawapongezapia Star tv kwa kutimiza matakwa ya kimaadili ya vyombo vya habari.
Hakuna mwanaCCM mwenye mamlaka ya kunyakua au kubaka mamlaka ya CC-CCM.
Mmejiuliza kuwa huyo mgombea mnayeshirikiana naye kutishia Watanzania kuwa watahama nchi
ataishije kama hatakuwa mgombea wa CCM?
Kama hamkubaliani na utaratibu wa CCM, uwanja hapa Tanzania ni mpana sana.
Acheni kuwatisha Watanzania.