Hivi kwanini wanasheria huwa wanaitana wakili msomi

Hivi kwanini wanasheria huwa wanaitana wakili msomi

Ushamba tu,wakili msomi kuna wakili hajasoma?
Hana confidence.
Ukiona mtu anajipakia mavyeo kibao mahd sijui jua hii ndaza hii

Mawakili ambao hawajasoma ni wachache sana.

Mfano, marehemu Mtikila alikutunukiwa uwakili bila kusomea uwakili. Kwa hiyo akikuwa wakili ambaye hakusoma.
 
Acha kulisha watu matangopori, nyinyi vilaza

Sasa hivi hata Chatgpt inaweza kunitengenezea defence legal document nikiilisha taarifa sahihi

Absolutely! I can help you draft a legal document for criminal defense. To tailor the document to your needs, could you please provide the following details:
  1. Type of Legal Document: What specific type of legal document do you need? (e.g., a motion to dismiss, a memorandum of law, a response to a motion, an affidavit, etc.)
  2. Case Details: Provide a brief summary of the case, including charges, key facts, and any relevant legal issues.
  3. Client Information: Basic information about the client (name, address, case number).
  4. Jurisdiction: The court and jurisdiction where the case is being heard.
  5. Legal Arguments: Any specific legal arguments or defenses you wish to include.
  6. Precedents: Any case law or statutes you want to reference.
  7. Additional Information: Any other details that might be relevant to the document.
Once you provide this information, I can create a draft for you.
Sawa, lakini huwezi kuwa wakili.

Utaishia Google tu.
 
Mwansheria ni mtaalamu wa kila sekta.

Kila sekta ina sheria, na hivyo mwanasheria anawajibika kuzifahamu.

Pia sekta zote zina kesi na hivyo mwanasheria anahusika nazo.

Ina aminika kwamba, mwanasheria ni mtaalamu anayeongoza kwa kuwa na elimu pana kuliko taaluma zote duniani.

Hii ndiyo sababu sisi Wanasheria kuitana wasomi yaani Learned lawyer/Advocate.
Wanasheria wa Tanzania hamjui kuzungumza kiingereza vizuri. Ushahidi ni kesi tunazoshindwa kila mara. Role model wenu ni Prof Ndalichako.
 
Hata watu wa IT wanalazimika kusoma kila kazi wanayotaka kuifanya, katika Ulimwengu wa leo katika fani zote mifumo yao inatumika wala hawaitani wasomi.
 
Ni kutokana na
1. Nafasi na mchango wao katika Muhimiri wa Mahakama, huchukuliwa ni miongon mwa watumishi wa Muhimiri husika wenye jukumu la kuionesha na kuiongoza mahakama ipite wap, ichukue/isichukue kipi katika kufikia maamuzi ya kesi husika. Katika kuhakikisha hili, inawalazimu kurejea sheria, kanuni na mamuzi ya Mahakama kuu au ya Rufani. Ikumbukwe, hizi sheria, kanuni na maamuzi hubadilika mara kwa mara. Hvyo kusoma kila iitwapo leo hakuepukiki ili wakili husika asipitwe na mabadiliko husika.

2. Kwakua sheria na kanuni ndizo silaa pekee zitumikazo kusimamia na kuongoza mambo yote ya kijamii, siasa na uchumi. Kutokana na hili utaona ni kwa wigo gani mwanasheria inampasa kusoma sana ili kuwa na ufahamu katika maswala mbalimbali.
Muhimiri = mhimili, silaa = silaha
 
Ni hivi, mfano, wewe ni Engineer maana yake wewe unafahamu sheria za ujenzi kwa undani.

Halafu mimi ni mwanasheria, maana yake ninazifahamu sheria zifuatazo:

1. Sheria za ujenzi.

2. Sheria za mazingira

4. Sheria za kazi

5. Sheria za uvuvi

6. List inaendelea.

Sasa hilo gap nililokupiga hapo, ndipo usomi wa mwanasheria unapoingia.
Bado haileti hoja kuitwa wakili msomi mkuu, engineer nae si msomi vile vile au tuwatafutie jina " mjuaji" si anajua vingi😅😅
 
Wanasheria wa Tanzania hamjui kuzungumza kiingereza vizuri. Ushahidi ni kesi tunazoshindwa kila mara. Role model wenu ni Prof Ndalichako.

Siyo kazi ya mwanasheria kushinda kesi.

Katika majukumu ya mwanasheria ama wakili yeyote, kushinda kesi siyo jukumu lake.

Jukumu kuu la mwanasheria ni kutafuta haki, yaani kaana yake mteja ndiye hupoteza kesi mahakamani na siyo wakili.

Wakili ni afisa wa mahakama mwenye jukumu la kuisaidia mahakama kufanya maamuzi na siyo kushinda.

Kwa hiyo msitubebeshe jukumu ambalo halijawahi kuwepo na halitakuwepo.
 
Bado haileti hoja kuitwa wakili msomi mkuu, engineer nae si msomi vile vile au tuwatafutie jina " mjuaji" si anajua vingi😅😅

Kila mtu ashinde mechi zake mkuu.

Jiite Injinia Msomi na mimi nijiite Mwanasheria Msomi halafu tuone.
 
Sioni kama kuna ubaya kwenye tathinia ya sheria kujiita wakili msomi.Nitaaluma yao kulingana na kazi yao.Hivyo basi tusilazimishe tufanane wote,kwa lugha nyepesi tunaweza tukasema hii ni misimu ndani ya sheria watu wengine tusio husika ni vigumu kuwaelewa.
 
Siyo kazi ya mwanasheria kushinda kesi.

Katika majukumu ya mwanasheria ama wakili yeyote, kushinda kesi siyo jukumu lake.

Jukumu kuu la mwanasheria ni kutafuta haki, yaani kaana yake mteja ndiye hupoteza kesi mahakamani na siyo wakili.

Wakili ni afisa wa mahakama mwenye jukumu la kuisaidia mahakama kufanya maamuzi na siyo kushinda.

Kwa hiyo msitubebeshe jukumu ambalo halijawahi kuwepo na halitakuwepo.
Kama jukumu lenu sio kushinda kesi si mtafute kazi nyingine ya kufanya? Nchi inaingia hasara kwenye kesi kila leo huku kuna wangese wanajiita wakili wasomi..!!
 
Muhimiri = mhimili, silaa = silaha

Nimeyapokea masahihisho husika. Nikiri wazi, athari za lugha mama ni changamoto. Kwakupitia mchango wako, wengi tutajifunza na kukinyoosha kiswahili chetu kwa mujibu wa kanuni zake. Asante sana.
 
Ni hivi, mfano, wewe ni Engineer maana yake wewe unafahamu sheria za ujenzi kwa undani.

Halafu mimi ni mwanasheria, maana yake ninazifahamu sheria zifuatazo:

1. Sheria za ujenzi.

2. Sheria za mazingira

4. Sheria za kazi

5. Sheria za uvuvi

6. List inaendelea.

Sasa hilo gap nililokupiga hapo, ndipo usomi wa mwanasheria unapoingia.
Ukijua sheria za injinia tayari umekuwa Injinia ? Mfano wako hauendani na wa kwanza. Wewe ni msomi wa kila fani au unajua sheria za kila fani ?
Kama wewe mwanasheria unatakiwa ujue sheria zote huo usomi wako unakujaje ? Hio si ni taaluma yako ? ie kukariri sheria tena hata hamzitungi( nyie ni kasuku)
Wanasheria wengine hueleza tofauti na wewe ulivyoeleza. Kama tu mnatofautiana kwenye mana ya hilo neno mnakuwaje wasomi?
 
Ni kutokana na
1. Nafasi na mchango wao katika Muhimiri wa Mahakama, huchukuliwa ni miongon mwa watumishi wa Muhimiri husika wenye jukumu la kuionesha na kuiongoza mahakama ipite wap, ichukue/isichukue kipi katika kufikia maamuzi ya kesi husika. Katika kuhakikisha hili, inawalazimu kurejea sheria, kanuni na mamuzi ya Mahakama kuu au ya Rufani. Ikumbukwe, hizi sheria, kanuni na maamuzi hubadilika mara kwa mara. Hvyo kusoma kila iitwapo leo hakuepukiki ili wakili husika asipitwe na mabadiliko husika.

2. Kwakua sheria na kanuni ndizo silaa pekee zitumikazo kusimamia na kuongoza mambo yote ya kijamii, siasa na uchumi. Kutokana na hili utaona ni kwa wigo gani mwanasheria inampasa kusoma sana ili kuwa na ufahamu katika maswala mbalimbali.
No 1. Kuna tofauti gani na walimu waundao mtaala ambso hushauri mtaala uubdwe vipi nini kifundishwe nini kisifundishwe nk.
2. Nuie mnasoma sana kuliko Dr wa binadamu na mifugo ?
Nyie mnasoma sana kuliko Injinia ?
Kwanza nyie huwa mnanukuu sheria kama kanisani au msikitini.
Daktari huingua kufanya operation bila kunukuu mahala. Huo usomi we u upo wapi ?
Nyie wasomi wa sheria mmeshindwa kutunga sheria nzuri na kiondoa sheria kandamizi.
Hamba lolote wanasiasa wamewakalia kichwani na hio hadhi ya USOMI mnastahili kunyang'anywa .
Halafu mnatetea hata majitu iliodhihirika kuvunha sheria waziwazi. Mnaweka maslahi ya PESA mbele badala ta haki.
Hata mtu akidhulumu nyumba nyie mnamtetea ili mpate pesa dhuluma iendelee.
Wanasheria and the co. Ni agents wa dhulma badala ya haki.
 
Kama jukumu lenu sio kushinda kesi si mtafute kazi nyingine ya kufanya? Nchi inaingia hasara kwenye kesi kila leo huku kuna wangese wanajiita wakili wasomi..!!
Huyu mwanasheria kaniacha hoi
Anasema wanasheria siyo
Jukumu lao kushinda kesi 😄

Ova
 
Ukijua sheria za injinia tayari umekuwa Injinia ? Mfano wako hauendani na wa kwanza. Wewe ni msomi wa kila fani au unajua sheria za kila fani ?
Kama wewe mwanasheria unatakiwa ujue sheria zote huo usomi wako unakujaje ? Hio si ni taaluma yako ? ie kukariri sheria tena hata hamzitungi( nyie ni kasuku)
Wanasheria wengine hueleza tofauti na wewe ulivyoeleza. Kama tu mnatofautiana kwenye mana ya hilo neno mnakuwaje wasomi?

Kwa taarifa yako hata neno "law" hatuna msimamo wa pamoja lina maana gani.

Sheria inahusina na haki moja kwa moja.

Kwenye law hakuna jibu la moja kwa moja.

Halafu unaweza pia ukachangia bila kashfa na ukaeleweka.
 
Huyu mwanasheria kaniacha hoi
Anasema wanasheria siyo
Jukumu lao kushinda kesi 😄

Ova

Ninarudia tena kwa herufi kubwa HAKUNA MWANASHERIA ANAYESHINDWA AU KUSHINDA KESI MAHAKAMANI BALI MTEJA NDIYE HUSHINDA AU KUSHINDA KESI HIZO. PIA KATIKA MAJUKUMU YA MWANASHERIA, KUSHINDA KESI SIYO MOJA YA MAJUKUMU YA MWANASHERIA.

Kama hutaki kuelewa acha broo!
 
Back
Top Bottom