ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,456
- 41,378
Kuna jambo huwa linanichanganya sanaš¤
Je, elimu imekuongezea akili au imekuondolea upumbavu?
Kwa sababu nimeona watu wenye elimu za juu sana, vyeti vingi na majina marefu, lakini baadhi ya maamuzi yao yanakufanya ujiulize kama kweli elimu peke yake inatosha kumfanya mtu awe na akili
Unakuta mtu ni kiongozi ameshika nyadhifa mbali mbali ila ukitazama maamuzi yake unabaki na alama ya mshangao heh huyu si ni msomi?
Unajiuliza huyu elimu haikua na msaada kwake ?
Mbona anaamua,anaongea kama mjinga?
Wakati huo huo unakutana na mtu ambaye hakusoma sana au hakupata nafasi ya kusoma kabisa, lakini ana uwezo mkubwa wa kufikiri, kutatua matatizo na kuona mambo kwa upeo mpana kuliko hata baadhi ya wasomi
Hapo ndipo nikajiuliza, ni nini hasa kinachomfanya mtu aitwe genius na ni nini kinachomfanya aonekane mpumbavu?
Je, ni kiwango cha elimu?
Je, ni uwezo wa kufikiri?
Je, ni maamuzi anayofanya kila siku?
Au ni namna anavyojifunza kutokana na makosa yake?
Kwa mtazamo wangu, elimu inaweza kuongeza maarifa, lakini si lazima iondoe upumbavu
Maana kuna wasomi wapumbavu(hapa nisamehewe)
Na kutosoma sana si lazima kumfanye mtu akose akili
Wewe unaonaje?
Tofauti ya mtu mwenye akili nyingi na mpumbavu unaiona wapi?
Na elimu imekusaidia nini hasa kwenye hilo?
Chombezo( ni kua hata wapumbavu huzeeka)
ShesRise_1 š¤
It's Furahi deiiiiiiš